Mwigulu Nchemba: Wahitimu vyuo vikuu rudisheni mikopo

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wahitimu wa vyuo vikuu kurejesha mikopo waliyopata kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ili wanafunzi wengine wasio na uwezo pia wanufaike.

Hotuba ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo kwa niaba ya Dkt. Mwigulu wakati wa mahafali ya 50 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alisisitiza kuwa mikopo hiyo imetolewa inakusudiwa kuzunguka na kuwanufaisha wengine.

Soma pia: Mbunge Kishimba atoa Onyo: Bodi ya Mikopo (HESLB) itafilisika ikiendelea kutoa fedha kwa Elimu Isiyoajirika, Bodi inazitupa hela kwa GPA isiyoajirika

“Naelewa kuwa baadhi yenu mliohitimu leo (Jumamosi) mliweza kufikia hatua hii muhimu baada ya kupata mikopo kutoka HESLB, Hii ndiyo nia ya serikali ya kuwatumikia wananchi wake bila kujali hali zao. Mpango huo ulianzishwa kwa wale wanaohitimu elimu ya juu lakini wanakabiliwa na vikwazo vya kifedha.”

"Niwakumbushe wanufaika wa mikopo ya serikali kuwasaidia wenzao katika kufikia ndoto zao kwa kuanza kurejesha mikopo yao,"

Waziri aliongeza kushindwa kurejesha mikopo hiyo kutaathiri jitihada za serikali za kuwawezesha wananchi wengi kupitia elimu.

Screenshot 2024-12-02 160511.png
 
Msiishie kuwapa vijana mikopo, hakikisheni wakimalizs vyuo wanapata ajira rasmi ili waweze kulipa mikopo yao.

Ninaamini 70% ya wahitimu wa vyuo vikuu na vya kati hawana ajira, sasa wanalipaje hiyo mikopo.
 
Serikali iweke Utaratibu... kila Mwajiri iwe Sekta rasmi au Isiyo rasmi ahakikishe anafanya deduction kutoka kwenye Salary ya Mwajiriwa mpyA.. iwe ni sheria..
Hizi pesa zikirudi ndizo husaidia Watanzania wengine kupata access ya Elimu
 
Wajiajiri, walipe mkopo, NO WAY OUT ! wengi wapo kwenye foleni wanasubiri hizo hela, hamna cha bure
 
Wanarudisha vipi hawana kazi Wala vipato vyakuweza kurudishwa?. Kwanza hata walioajiriwa ilitakiwa wapewe Grace period at least ya Miaka 10 Ili ndio waanze kurudisha.
 
Nyinyi mlisoma bure bila mikopo na ajira mlipata kutwa mpo kuwajadili watoto waliosoma kwa mikopo na huku ajira hawana toeni ajira ili warudishe mikopo yao...
 
Wajiajiri, walipe mkopo, NO WAY OUT ! wengi wapo kwenye foleni wanasubiri hizo hela, hamna cha bure
Basi wasubiri vijana wajiajiri, if you think kujiajiri ni kitu kila mtu anaweza kufanya.
 
hapo wanahaha, maaana waliowengi wamemaliza mikopo mwaka jana na mwaka huu, ajira za idadi ya watu wengi wamemaliza hawana cha kukusanya tena
 
Serikali iweke Utaratibu... kila Mwajiri iwe Sekta rasmi au Isiyo rasmi ahakikishe anafanya deduction kutoka kwenye Salary ya Mwajiriwa mpyA.. iwe ni sheria..
Hizi pesa zikirudi ndizo husaidia Watanzania wengine kupata access ya Elimu
Hicho ndicho kinachofanyika, kila mwaka hupita kwenye mashirika ya binafsi kutafuta waajiriwa wapya...
 
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amewataka wahitimu wa vyuo vikuu kurejesha mikopo waliyopata kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ili wanafunzi wengine wasio na uwezo pia wanufaike.

Hotuba ya Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Stanslaus Nyongo kwa niaba ya Dkt. Mwigulu wakati wa mahafali ya 50 ya Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki alisisitiza kuwa mikopo hiyo imetolewa inakusudiwa kuzunguka na kuwanufaisha wengine.

Soma pia: Mbunge Kishimba atoa Onyo: Bodi ya Mikopo (HESLB) itafilisika ikiendelea kutoa fedha kwa Elimu Isiyoajirika, Bodi inazitupa hela kwa GPA isiyoajirika

“Naelewa kuwa baadhi yenu mliohitimu leo (Jumamosi) mliweza kufikia hatua hii muhimu baada ya kupata mikopo kutoka HESLB, Hii ndiyo nia ya serikali ya kuwatumikia wananchi wake bila kujali hali zao. Mpango huo ulianzishwa kwa wale wanaohitimu elimu ya juu lakini wanakabiliwa na vikwazo vya kifedha.”

"Niwakumbushe wanufaika wa mikopo ya serikali kuwasaidia wenzao katika kufikia ndoto zao kwa kuanza kurejesha mikopo yao,"

Waziri aliongeza kushindwa kurejesha mikopo hiyo kutaathiri jitihada za serikali za kuwawezesha wananchi wengi kupitia elimu.
View attachment 3167408
Na wewe rudisha pesa za serikali ulizotumia kukarabati viwanja vya wizi vya CCM.
 
Aache upuuzi ,waondoe TOZO kwenye miamala waliyoweka kwa ajili ya kujenga madarasa maana inaendelea tu.
 
Nafikiri tatizo kubwa tulilo nalo ni kukosa Elimu inayohusu mikopo ya Elimu ya juu kwa watoto.
Kama wazazi wataelimika na kutambua kuwa, kukopeshwa Ada sio kumsaidia mtoto bali ni kumpa mzigo mkubwa pale atakapo anza maisha yake; Kipaumbele namba moja kingekuwa ni kujitahidi kumlipia kadri familia inavyoweza.
Na hii ingetoa fursa kwa wale watoto waliotokea familia duni wapate mikopo ya kujitosheleza (100%)

Ukifuatilia kwa makini watoto kwa maelf wanaomaliza shule za binafsi, wazazi wengi (JAPO SIO WOTE) wanauwezo wa kulipia watoto wao ada za Elimu ya juu hasa kwa hizi kozi za Arts ambazo ada yake ina unafuu. Unaweza kuta kozi nyingine zinalipiwa ada chini ya kiwango cha ada kinacholipwa shule za kawaida za Sekondari
LAKINI UNAWEZA KUSHANGAA, MZAZI ANAYEJIWEZA KABISA ANASHANGILIA MTOTO WAKE KUPATA MKOPO???
 
Back
Top Bottom