Mwigulu Nchemba anawatisha kwa kuwa ni “Mr. Clean.” Amefuata nyendo za Magufuli.
Mwigulu amekuwa Waziri wa Mifugo; hatukusikia amejikatia ranch za umma na kuzifanya za kwake. “Mr. Clean.” Alikuwa Waziri wa Kilimo; hatukumsikia akijikatia mashamba ya umwagiliaji na mitambo. “Mr. Clean.”
Amekuwa Waziri wa Fedha kwa miaka mitano; hatujaona akibadilika na kuwa bilionea. Sana sana, ana watoto yatima zaidi ya mia moja na anawasomesha kwa kuombaomba kwa Bakhresa na ASAS. Maana halisi ya “Mr. Clean.”
Kama ilivyokuwa kwa maisha ya Dkt. Mpango, hii ni ishara kwamba fedha hupotelea kwenye wizara za kisekta zinazopokea fedha na kuingia mikataba ya kipigaji.
Sasa wezi, wala rushwa na wapigaji wanasema: “Huyu jamaa anazijua deals zetu na hajashirikiana nasi kwenye hizi deals. Huyu atakwenda kutufumua kama Magufuli alivyofanya.”
Dawa? Tumzuie 2030 asipande. Tutafute mtu mpya tutakayemwendesha.
Dosari pekee aliyonayo Mwigulu ni kwamba huyu ni Magufuli mpya.
Dada Mange ameandika kuwa walitaka kumuua Mwigulu kwa sumu, Mungu akamnusuru. Maria Sarungi naye ameandika kuwa Mwigulu sasa hatakiwi na mtoto na familia, wanamwona ni Magufuli mpya.
Sasa sumu imeshindikana, amesema Simai, huyu anatafutiwa sababu amfuate Nchimbi.
Watanzania tusipuuze, kama tulivyoona kwa Nchimbi, kuwa haiwezekani wanamtikisa tu wakamtoa.