Mwigulu: Tozo za miamala zipo kisheria, Waziri hawezi kuzifuta

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba tozo za miamala na muda wa hewani zimepitishwa na bunge hivyo yeye kama waziri hawezi kuziondoa ila anaweza kuangalia kanuni kujua namna ya kurekebisha

Amesema hayo alipohojiwa na BBC Swahili ambapo amesema kwa sasa wananchi wanatakiwa kuelimishwa ili kukubaliana na tozo zinazokatwa kwenye miamala ya simu

Amesema kabla ya kuweka tozo hizo utafiti ulifanyika wa kutosha

Tatizo la Kula Maksai limeanza kuonekana. Huko singida unaweza kutoa Elimu ya Kodi Kwa njia gani Ili Kwa muda mfupi ueleweke?
 
Walimshirikisha mwananchi wa mkoa gani?!Na walilinganisha na wapi tunakofanana,tuanze hapo kwanza mtoa mada.
 
Mahojiano yake na BBC ni kabla au baada ya tamko la rais, mbona mnachanganya habari ?
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt Mwigulu Nchemba tozo za miamala na muda wa hewani zimepitishwa na bunge hivyo yeye kama waziri hawezi kuziondoa ila anaweza kuangalia kanuni kujua namna ya kurekebisha...
Mwendo ni uleule[emoji56][emoji56][emoji56]
 
Sawa

IMG-20210718-WA0139.jpg
 
Wakati wanajadili wanajificha hatuwaoni wakimaliza kupasha viti eti tumejadili tayari bila kushirikisha walipa tozo, Mungu anawaona, halafu 2025 utasikia kapita bila kupingwa, huyo aliye turoga kafukia kichwa tu miguu ipo nje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mjadala wa tozo upo hot naona tunamuonea Mwigulu. Tukumbuke, aliyetoa wazo tukasikia ni Zungu, kamati ya bajeti/fedha wakaiandika na kuileta bungeni, Bunge kibogoyo linalokula bila kulipa kodi likaipitisha, waziri alisoma tu na kutoa mswada na ukapitishwa, Rais akasaini na ikawa sheria. Leo hii tunamshambulia Mwigulu, why? Tatizo ni CCM na mfumo wake!

Naona kikao nacho kimeota mbawa! Tuendelee tu kuumia. Mungu ndo mtetezi wetu, atajibu kwa wakati!
 
Unajua majukumu ya waziri kama waziri?
Hayo mwigulu aliyofanya ni majukumu ya waziri kama mwigulu!
 
Wananchi wamesha delay na pesa zimeshawanogea hao jamaa imetoka hiyo
 
Kwann hawakutushirikisha mwanzo
hatutaki na tunajiandaa kugomea huduma
 
Kwa kawaida utaratibu uliopo ni Bunge kupitisha Sheria then Waziri husika hutungia Kanuni. Dr. Mwigulu hawezi kukwepa kuhusu gharama za miamala kwa sababu yeye kwa kushauriana na Waziri mwenzake wa Mawasiliano ndiye alisaini hizo Kanuni. So kuanza kuwahusisha wabunge sijui na Mheshimiwa Rais ni unafiki mkubwa!
 
..tozo za miamala zimetokana na mapendekezo ktk bajeti iliyowasilishwa na SERIKALI.

..lawama ya kwanza inapaswa kuwa kwa Serikali kuanzia kwa Waziri wa fedha, Raisi, na Cabinet.

..Suala hili ni lazima lilianza wizara ya fedha, likapelekwa kwenye cabinet ambayo mwenyekiti wake ni RAIS.

..Baada ya hapo ndio limepelekwa bungeni na Waziri wa Fedha.

..BUNGE lingeweza kuzuia jambo hilo lakini wabunge wa CCM wanamuogopa MWENYEKITI wao ambaye ni AMIRI JESHI MKUU.
 
Mlalamikiwa ni moja ya zao la bunge lake.
 
Mkuu, hakuna anayepinga kutoa kodi ila kiwango kilichowekwa ni kikubwa mno.
 
Back
Top Bottom