Mwigulu: Tunatumia vibaya mitandao. Kuna watu mitandaoni wakiandika utadhani Mungu kaandika

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, ametoa wito kwa Watanzania kuwa makini na matumizi ya mitandao ya kijamii, akisema baadhi ya watu wanaposhiriki mitandaoni huonekana kama wanajua yote, wakati kwa kweli hawana uhusiano wala ufahamu wa kweli.

Akizungumza katika Misa ya kuaga mwili wa marehemu William Lukuvi, bungeni jijini Dodoma, Dkt. Nchemba amesema:

"Siku hizi tunatumia vibaya mtandao. Sisi hapa mitandaoni, wapo wengine wakiandika utadhani ni Mungu kaandika. Ukimwangalia mtu mwenyewe anayeandika hivyo, ameshadhulumu dhulumu tu; hata sio msafi, ana madeni kibao na utapeli mwingi. Somo la leo, Baba Paroko, limetusaidia sana kuturudisha binadamu, tuone sisi ni binadamu na safari yetu ni moja."

Ameongeza kuwa, kupata masahihisho ya kuweza kujua nani ananufaika au nani amekosea, ni jambo linalobaki kwa Mungu peke yake.

Mnafiki mkubwa huyu
 
Wawe pia na stahaaa...hakuna mtu anatumia mtandao vibaya

Huwa wana majibu ya kunya kunya mna..ndio maana watu wanakuwa Mungu huku mtandaoni..
 
Screenshot_20260312_130823_Chrome.jpg
 
Back
Top Bottom