Mwigulu: Tutaendelea kukopa, deni ni himilivu

Mwigulu: Tutaendelea kukopa, deni ni himilivu

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Mkopo sio Msaada, na Mkopo hutolewa kwa mwenye chanzo cha kulipa. Amesema, "Tutaendelea kukopa ili tutekeleze miradi mikubwa kwa haraka"

Amesema tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Mwezi Novemba inaonesha Deni ni himilivu kwa kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu

Vilevile, ameeleza kuwa sio jambo la kiungwana kusema Rais anakopa akisisitiza Marais hawakopi bali ni Serikali akisema "Hilo si jambo la Familia, ni la Nchi"
 
Huyu Raisi wa mawe ni Bogus kabisa,kwanza atueleze tozo linalotutoa roho na mikopo fedha zinaenda wapi?

Na Uraisi hapati ng'o labda awe raisi wa Shelui.
 
Huyu amekuja kutoa mana ya vielezi, vivumishi na Vikurupushi badala ya kujibu by figures ili watu wajibiwe hoja ilyopo,na yeye akiwa minister mwenye dhamana ya hali fedha na situation ya burden ya nchi anaongelea vitu vyepesi vyepesi ambavyo hata ngumbalu anaweza.!! Hawa ni kati ya Minister mizgo mizgo!!
 
kukupa sio tatizo, ila tatizo ni matumizi ya hiyo mikopo.
Ni aibu na fedheha taifa lenye zaidi ya miaka 60 mnakopa ili kujenga vyoo.

Mmekabidhi taifa kwa malimbukeni waliyozoeya kulala na ng'ombe.
Ni sawa na wewe uende Benki na Business Plan lengo likiwa ni upewe mkopo ili ujenge choo.
 
Waendelee tu Kukopa na kwenye kulipa waendelee kulipa sio Wakati wa Kukopa Hatushirikishwi tunakuja kushituka tu Madeni yanapaa na tunatakiwa kulipa (na tulichofanyia mikopo hiyo hakifahamiki wala kuonekana)
 
Mimi nampenda sana Samia Suluhu Hassan ni kama mama yangu mdogo ila kwakweli kuna mambo hayaendi sawa lazima tuulize.

Samia mama yangu nakupenda sana nakutakia ufanikiwe ndio maana nakukosoa.
Mimi adui yangu alishatangulia kwenye moto wa milele.
 
😘😘😘😘😘

Samia suluhu Hassan.
Huu ndio mwaka wa Mama ajifunge kibwebwe halafu afanye mabadiliko kwenye baraza la mawaziri

Asiingilie kesi ya Mbowe ili Mapolisi wahenyeshwe ili Mwamba atoke bila Criminal record.
 
Kwanini tusilipe madeni yaliyopo ndio tuendelee kukopa..mana tunajua kuongeza madeni wala sio kupunguza.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mkopo ni himilivu kwa nani?aseme uwiano wa deni na Pato la Taifa.
Ccm wapo tayari kusema chochote Ili mradi walinde ugari wao.
Hii hapa chini:
B0673A60-E87D-44C8-A48D-B1956492D6E0.jpeg

7859469A-B848-4A7F-A4B1-498EAA16DB07.jpeg
 
Back
Top Bottom