Mwigulu: Tutaendelea kukopa, deni ni himilivu

Mwigulu: Tutaendelea kukopa, deni ni himilivu

Huu ndio mwaka wa Mama ajifunge kibwebwe halafu afanye mabadiliko kwenye baraza la mawaziri

Asiingilie kesi ya Mbowe ili Mapolisi wahenyeshwe ili Mwamba atoke bila Criminal record.
Mbowe kama anatakiwa kuliwa kichwa wacha tu aliwe kichwa.

Uchaguzi ndani ya chama unakaribia ngoja tuzione sarakasi zake.

2025 kisiasa ni mbali sana anything can happen.

Tumwombe Mungu mambo yaende vizuri amani ndio jambo la msingi zaidi na jambo la msingi zaidi ni kuhakikisha mafisadi hayatafuni nchi yetu.
 
CCM wanadharau za muda fupi (kuomba kura kwa wajumbe) dharau za kati (wakati wa kampeni za uchaguzi) na dharau za muda mrefu (baada ya uchaguzi)
 
Rais wa awamu ya 7 kazi anayo.
- Atakutana na katiba mpya
-Deni la taifa lipo kwenye ukomo wa kuweza kukopa!
 
Mbowe kama anatakiwa kuliwa kichwa wacha tu aliwe kichwa.
Yeye anasema hataki 'fujo' kwanini abebe kesi ya Magufuli na trust me itamletea 'fujo' sana.

Mama aondoe mkono Mahakamani ili ifanye kazi yake bila kuingiliwa tuone hiyo kesi ya kubumba inavyoporojeka.
 
Mwigulu Nchemba atuambie kwanza kwa sasa wanakusanya kiasi gani kutokana na tozo na zinatumikaje?
Tumeamua kutoa tozo bila kwenda Bujumbura kama alivyotutaka, ila atuambie mchanganuo wa matumizi ya tozo.
 
Kukopa ni harusi waugwana

Mikopo sio kitu kibaya lakini sio kitu kizuri pia
Nimependa jibu lako, mikopo ni mizuri lakini pia ni mibaya.

Nibu ni kwamba, huku Afrika mikopo ni mibaya kwa sababu pesa hukopwa na hutumiwa vibaya.

Kwa ujumla matokeo ya mikopo kwa ni afrika kidogo kutoka kuliko matarajio ya mikopo yenyewe.
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Mkopo sio Msaada, na Mkopo hutolewa kwa mwenye chanzo cha kulipa. Amesema, "Tutaendelea kukopa ili tutekeleze miradi mikubwa kwa haraka"

Amesema tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Mwezi Novemba inaonesha Deni ni himilivu kwa kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu

Vilevile, ameeleza kuwa sio jambo la kiungwana kusema Rais anakopa akisisitiza Marais hawakopi bali ni Serikali akisema "Hilo si jambo la Familia, ni la Nchi"
hivii mnada wa hili shamba utafanyika lini ? nataka niwastue jamaa zangu wajiandae kuja kulinunua shamba TZ. nadhani ndo itakuwa nafuu ya mwananchi atabadilisha maisha upyaaaa kuptia hawa jamaa!!
 
Salama wandugu
naona kwenye mkutano wao wa matumizi ya mkopo hakuna la maana linaloelezwa wanajipambanua tu kwamba wataendelea kukopa kwa kuwa wanasifa ya kukopa
Unaweza kuwa na sifa ya kukopa lakini ukawa wewe mdaiwa sugu ndio Jambo linalopigiwa kelele zaidi nilitegemea wataniambia lini na kiasi gani Deni lilipunguzwa kutoka kiasi gani mpaka kiasi gani Ndungai najua unatetea ugali wako ndio maana umekengeuka kutoa maelezo uliyotakiwa kueleza
 
A
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Mkopo sio Msaada, na Mkopo hutolewa kwa mwenye chanzo cha kulipa. Amesema, "Tutaendelea kukopa ili tutekeleze miradi mikubwa kwa haraka"

Amesema tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Mwezi Novemba inaonesha Deni ni himilivu kwa kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu

Vilevile, ameeleza kuwa sio jambo la kiungwana kusema Rais anakopa akisisitiza Marais hawakopi bali ni Serikali akisema "Hilo si jambo la Familia, ni la Nchi"
Atuambie tozo na hela za mikopo zinaenda wap maana deni la taifa linazid kuongezeka na hakuna unafuu wa maisha, namunukuu spika ipo siku nchi itapigwa mnada aliongea kiutu uzima na huo ndo ukwel
 
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Mkopo sio Msaada, na Mkopo hutolewa kwa mwenye chanzo cha kulipa. Amesema, "Tutaendelea kukopa ili tutekeleze miradi mikubwa kwa haraka"

Amesema tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Mwezi Novemba inaonesha Deni ni himilivu kwa kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu

Vilevile, ameeleza kuwa sio jambo la kiungwana kusema Rais anakopa akisisitiza Marais hawakopi bali ni Serikali akisema "Hilo si jambo la Familia, ni la Nchi"
Ndugai vipande vipande bado anaendelea kula nondo., ni kama vile amepanda mchongoma

Ivi ndugai anaweza kutoka mbele ya bunge akidai yeye ni spika? Kwa hali hii nikujiuzulu tu ndicho kilichobaki kwke
 
Hangaya anazima Moto wa umeme kwa maji😎😎😎😎
 
Kama Rais hakopi bali serikali, mbona akitoa pesa mnasema Samia katoa?

Wapuuzi.
 
Kama Rais hakopi ni Serikali, lugha hiyo hiyo itumike fedha zinapotolewa, yaani Serikali na siyo Rais anayetoa fedha kwa shughuli yoyote ya Kitaifa
Mkuu umeniwahi, na Mimi nilitaka kuchangia hivihivi.
 
Back
Top Bottom