Mwigulu: Wananchi wanaenda kupata fedha nyingi, watazoea makato

Mwigulu: Wananchi wanaenda kupata fedha nyingi, watazoea makato

Huyu jamaa kweli ni mchumi ?

Wananchi hata kila mtu akiwa bilionea kama kuna option A na B na B ni gharama ndogo unadhani atatumia option A ?

Kama kutuma pesa nakatwa Buku Tatu, mtu anayenidai unadhani atasema tuma tu ili nikatwe sababu ninazo nyingi au atasema tukutane mtaa wa pili unipe pesa au mtume Bwana mdogo alete mia tano anunue pipi ?

Huyu Jamaa asipoangalia Historia itamkumbuka kama jamaa aliyeuwa maendeleo / kasi ya teknolojia kwa kupunguza kasi ya Safari ya kuelekea Cashless Society...., Tanzania ilikuwa ni nchi kati ya nchi zinazoongoza kwa Financial Inclusive sababu ya hizi Mpesa et al jambo ambalo mabenki yalishindwa (sasa je tunarudishana kule tulipotoka)?

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema wananchi wasiwaze kuhusu gharama za miamala ya simu kwa kuwa mzunguko wa fedha utaongezeka

Akiongea katika kipindi cha Aridhio, TBC amesema gharama za miamala hazina maana kwa kuwa watakuwa wanapata fedha zaidi katika kipindi hichi

Amesema serikali imejipanga kulipa madeni ili wananchi wawe na fedha
Hivi mwigulu alishawahi wapi kushughulika na uchiumi nje ya siasa.
 
Mkuu kwani si mlikuwa mnasema mama anafungua nchi na kurudisha hela mtaani ili muwe mnaziokota?

Sasa kwanini unapinga mawazo ya mwigulu?
Mbona unanukuu mambo ambayo hayahusiani Mama alisema anafungua Nchi ili Wawekezaji waje kutoa Ajira ni jambo jema sana

Sisi 'bifu' yetu iko kwa Mwigulu na Zungu kuhusu hii tozo ilyogomewa na Wananchi
 
Kodi zinaumiza lakini kwa nchi zetu hizi za dunia ya tatu ni kwamba hatuna ujanja, vinginevyo ni sisi wenyewe ambao tusipoona kinachofanyika cha kimaendeleo tunakuwa wa kwanza kuikejeli serikali tukisema hakuna cha maana inachofanya.

Bila ya ukusanyaji makini wa kodi mawaziri wetu wa fedha na mipango wataendelea kwenda ulaya na marekani wakiongea lugha ya ombaomba vikaoni. Sasa hivi Ulaya imekumbwa na mafuriko yaliyochukua uhai wa watu zaidi ya 100, waache kufikiria namna ya kushughulika na hiyo shida wamfikiria waziri wetu wa fedha anayokwenda kupeleka njaa ya watu wake!!.

Kodi kukusanywa ni kuongeza nidhamu zetu za matumizi, inatuongezeka ule utambuzi wa kutumia kila senti kwa uangalifu mkubwa. Hakuna njia ya mkato itakayotutoa hapa tulipo na kutusogeza mbele kimaendeleo.
 
Mbona unanukuu mambo ambayo hayahusiani Mama alisema anafungua Nchi ili Wawekezaji waje kutoa Ajira ni jambo jema sana

Sisi 'bifu' yetu iko kwa Mwigulu na Zungu kuhusu hii tozo ilyogomewa na Wananchi
Sasa kufungua nchi si ndio huko?

Bifu liko kwa Mwigulu na Zungu ila unamtenga mama?
 
Kodi zinaumiza lakini kwa nchi zetu hizi za dunia ya tatu ni kwamba hatuna ujanja, vinginevyo ni sisi wenyewe ambao tusipoona kinachofanyika cha kimaendeleo tunakuwa wa kwanza kuikejeli serikali tukisema hakuna cha maana inachofanya...
Ongeza kodi kwenye luxuries sio kwenye necessities..., unaongeza kodi kwenye miamala yaani ni kama wewe nakwambia kila ukinunua kutoka mfuko wa shati nakukata senti kadhaa ukitumia mfuko wa nyuma haukatwi unadhani utaendelea kuweka pesa mfuko wa shati ?
 
Miaka yote kodi imeongezwa kwenye hizo luxuries. Kumbuka hizo luxuries zina watu wengi tu wanaoishi kwa kuzitegemea, na kwao kilio ni kama hiki cha kwako.

Ni kukubaliana na uhalisia wa dunia ya sasa, wigo wa pesa za nje zenye kuwezesha bajeti zetu kuweza kuendeshwa, unakwenda ukipungua.
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema wananchi wasiwaze kuhusu gharama za miamala ya simu kwa kuwa mzunguko wa fedha utaongezeka

Akiongea katika kipindi cha Aridhio, TBC amesema gharama za miamala hazina maana kwa kuwa watakuwa wanapata fedha zaidi katika kipindi hichi

Amesema serikali imejipanga kulipa madeni ili wananchi wawe na fedha
Uchumi wa kati halafu unamkamua mwananchi
 
Ila watanzania pia tujaribu kushauri ..je ingefanyika kitu gani ili serikali ipate fedha za kugharimia vitu kama barabara za lami vijijini..shuke zilizobireka vijijin..na kutoa ahira za walimu na watu wa afya..Naomba tutoe mawazo
Kwani hapo kabla awamu zilizopita pesa walikuwa wanapata kutoka wapi?
 
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba amesema wananchi wasiwaze kuhusu gharama za miamala ya simu kwa kuwa mzunguko wa fedha utaongezeka

Akiongea katika kipindi cha Aridhio, TBC amesema gharama za miamala hazina maana kwa kuwa watakuwa wanapata fedha zaidi katika kipindi hichi

Amesema serikali imejipanga kulipa madeni ili wananchi wawe na fedha
Sick mind......as usual.....wajanja wameshachukua hatua long time...atabaki na mafala tu.
 
Miaka yote kodi imeongezwa kwenye hizo luxuries. Kumbuka hizo luxuries zina watu wengi tu wanaoishi kwa kuzitegemea, na kwao kilio ni kama hiki cha kwako.

Ni kukubaliana na uhalisia wa dunia ya sasa, wigo wa pesa za nje zenye kuwezesha bajeti zetu kuweza kuendeshwa, unakwenda ukipungua.
Duh naona hauelewi

Hivi kuongeza kodi kwenye mbegu na mbolea kuna tija ? , Kama issue ni pesa tu kwanini tusiongeze huko pia ? Ila utaona kwamba huu ni mtiririko chain fulani ambayo ni kama mto badala ya kulishia mifugo yako kwenye chanzo cha mto ni bora ukalishia mwishoni mwa mto ili hayo maji yawe yamefanya mengine kabla wewe haujayapata...

Vinginevyo ni kuchafua maji ambayo yatakuwa hayana maana tena.
 
Back
Top Bottom