Mwigulu: Watumishi wala rushwa TRA watimuliwe na wafikishwe Mahakamani

Mwigulu: Watumishi wala rushwa TRA watimuliwe na wafikishwe Mahakamani

View attachment 3041028
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb), amemwagiza Kamishna Mkuu Mpya wa TRA, Yusuph Juma Mwenda, kuwachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu ikiwemo kuwafukuza kazi baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo wanaokiuka maadili ya kazi zao ikiwemo kudai na kupokea rushwa, kwa kuwa vitendo hivyo vinaitia doa Mamlaka na kuikosesha Serikali mapato.

Mhe. Dkt. Nchemba, amesema hayo wakati akihitimisha Kikao cha Tathmini ya Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).

Aidha, Dkt Nchemba, amemwagiza Kamishna huyo kuwachukulia hatua kali wafanyabiashara wasiowasilisha ritani za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), kwa kuwa Fedha hizo zinatakiwa kuwasilishwa serikalini kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwani wafanyabiashara ni Mawakala wa Serikali wa kukusanya kodi hiyo na hazitakiwa kufanywa kama ni sehemu ya mapato yao.

Aidha, Dkt. Nchemba amewataka watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, kuongeza ubunifu, umahiri na kuhakikisha wanatenda haki wakati wa kukusanya mapato ya Serikali ili kutimiza matarajio ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kuwaletea watanzania maendeleo ya uhakika.

Pia Dkt. Nchemba ametumia fursa hiyo pia kuwapongeza TRA kwa utendaji kazi mahiri kwa mwaka wa fedha ulioisha wa 2023/24, ambapo walikusanya kiasi cha shilingi trilioni 27.64, ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.67 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 28.30, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 14.50, ikilinganishwa na makusanyo ya shilingi trilioni 24.14 katika mwaka wa Fedha uliopita 2022/23.

Katika Halfa hiyo Mhe. Dkt. Nchemba aliambatana na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha.
Hadithi za majukwaani
Hao wafanyakazi wote hao wako kwenye mtandao wa wakubwa utaanzia wapi kuwachukulia hatua
 
Wizi hautaisha kwa bla bla inatakiwa vitendo na vitendo maana yake lazima baadhi waungame na kusema tulikuwa waizi na tumetubu na sasa tunapambana na majizi

La sivyo mdomo mkavu hautoshi inaonekana na wewe umo kwa kupiga hizi hela

Mkiugua cancer ndio mnaanza kumuomba Mungu na hela mnaziacha

Punguzeni mishahara yenu na muwaongeze mishahara Waalimu na manesi
Rushwa haitaisha na wizi bila kutubu nyie kwanza
 
View attachment 3041028
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb), amemwagiza Kamishna Mkuu Mpya wa TRA, Yusuph Juma Mwenda, kuwachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu ikiwemo kuwafukuza kazi baadhi ya watumishi wa Mamlaka hiyo wanaokiuka maadili ya kazi zao ikiwemo kudai na kupokea rushwa, kwa kuwa vitendo hivyo vinaitia doa Mamlaka na kuikosesha Serikali mapato.

Mhe. Dkt. Nchemba, amesema hayo wakati akihitimisha Kikao cha Tathmini ya Utendaji Kazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, kilichofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano Arusha (AICC).

Aidha, Dkt Nchemba, amemwagiza Kamishna huyo kuwachukulia hatua kali wafanyabiashara wasiowasilisha ritani za Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT), kwa kuwa Fedha hizo zinatakiwa kuwasilishwa serikalini kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kwani wafanyabiashara ni Mawakala wa Serikali wa kukusanya kodi hiyo na hazitakiwa kufanywa kama ni sehemu ya mapato yao.

Aidha, Dkt. Nchemba amewataka watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, kuongeza ubunifu, umahiri na kuhakikisha wanatenda haki wakati wa kukusanya mapato ya Serikali ili kutimiza matarajio ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kuwaletea watanzania maendeleo ya uhakika.

Pia Dkt. Nchemba ametumia fursa hiyo pia kuwapongeza TRA kwa utendaji kazi mahiri kwa mwaka wa fedha ulioisha wa 2023/24, ambapo walikusanya kiasi cha shilingi trilioni 27.64, ambayo ni sawa na ufanisi wa asilimia 97.67 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 28.30, ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 14.50, ikilinganishwa na makusanyo ya shilingi trilioni 24.14 katika mwaka wa Fedha uliopita 2022/23.

Katika Halfa hiyo Mhe. Dkt. Nchemba aliambatana na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Hamad Hassan Chande (Mb), Kamishna Msaidizi wa Idara ya Sera Wizara ya Fedha, Bw. William Mhoja, na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha.
"Ikiwa ni kweli hili likifanyika kwa miezi mitatu (03) tu kikamilifu nchi yetu itakuwa mahali pa salama pa kuishi" vinginevyo tamko litakuwa sawa na tabia ya Ng'ombe ya kutia ulimi wake puani na kuurudisha kinywani.
 
Yaani umeniwahi, ingekuwa China huyu siku nyingi washamnyonga. Only in Tanzania fisadi anapewa wizara ya fedha aile vizuri. Leo hii afanyiwe ukaguzi na watu toka nje ya Tz. Watu watabaki midomo wazi, kwa ukwasi alionao.
Asante unajicho pevu dada!
Huyu ni aina ya viongozi wenye uchu wa madaraka sana. Na ni mwizi mkubwa sana ni vile mfumo unawakingia kifua. Hakutakiwa kuwa uraiani
 
Serikali hii hakuna mwenye uhalali wa kukemea rushwa au ufisadi.

Watu wanafahamu kwa kina namna watawala na baadhi ya wabunge walivyokula rushwa kubwa kupindukia ili kuwezesha uporwaji wa rasilimali za nchi.

Watu wanafahamu namna watawala wanavyokula rushwa kubwa kubwa za ndani ya nchi. Halafu eti hao hao wala rushwa na mafisadi wakubwa wa kuuza rasilimali za nchi, eti wanakemea rushwa!! Huu ni unafiki mkubwa, na hata hao wala rushwa wa TRA sidhani kama watayazingatia hayo matamko. Mwizi wa ng'ombe anatoa tamko dhidi ya mwizi wa kifaranga, huyo mwizi wa kifaranga, atazingatia? Mwizi wa kifaranga anapambana ili na yeye afike kwenye nafasi ya kuiba angalao mbuzi na baadaye ng'ombe.

CCM kwa sasa, ni vema wangeingiza kwente katiba ya chama kuwa watawala kuiba, kula rushwa au kufanya ufisadi kwa kupora rasilimali za nchi ni halali. Japo wameliweka hili la kuhalalisha ufisadi wa watawaka kwa kuzunguka sana. Hawajatamka moja kwa moha, bali wanasema kuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Mkuu na Spika, hawatashtakiwa kwa kosa lolote wawapo madarakani au baada ya kutoka madarakani. Hivyo wamehalalisha hao watu kufanya uovu wote bila ya kuwa na hofu yoyote.

Nchi inatawaliwa na watu wenye ticket ya kuwafanyia uhalifu wowote wananchi bila ta kuhoniwa na yeyote.
 
Hao maboss wa TRA wanatamba Sana mtaani ndiyo maana na Sisi hatulipi Kodi, haiwezekani baadhi ya wafanyakazi waishi maisha ya wizi huku wafanyabiashara tukitaabika na biashara zetu...
Hakuna Fala anaweza kukubali kulipa Kodi kwenye mazingira hayaa
Ulipe Kodi ya Nini? Ili wakaishi maisha ya anasa na Malaya wao? Shwaini!
 
Back
Top Bottom