Mwigulu: Watumishi wala rushwa TRA watimuliwe na wafikishwe Mahakamani

Toka mfanyakazi mmoja wa TRA aniambie yeye hatakuja kufungua biashara hii nchi nilinyanyua mikono, I was so done na kuhamasisha uzalendo uchwara.

TRA wenyewe wanajua wanachowafanyia wafanyabiashara wa hii nchi? Wanazijua Vizuri sheria za kinyanyasaji walizoziweka, wanajua na viwango vya kodi kuwa havilipiki na vinashawishi ukwepaji.

Wewe unaowatetea TRA ni nani?
 
Hakuna watu wanaoongoza Kula Rushwa Kama viongozi (CCM )
Kukwepa kodi Kama matapeli kwa mgongo wa uchungaji, aliyeleta haya mambo ya wachungaji kutolipa kodi ndo aliharibu nchi ,


Britanicca
 
Upo sawa mkuu ila si nyakati zote.

Unajua ni mara chache sana kula pesa ya hoja zisizojibika, huwa wanakula pesa za hoja zinazojibika.

Mfano:
Labda umekutwa kuna utofauti wa M200 kati ya mashine na taarifa za bank, hii hoja inajibika ila inabidi uwe na nyaraka za M200 kuijibu, ukiwa nazo huna sababu ya kutoa rushwa unaweza ijibu tu na usitoe mia.

Tatizo linaanza huna nyaraka za kufikia M200.
Pendekezo la kodi ni 18% x 200,000,000/= na 30% x 200,000,000/= plus interest. Inakuja kodi kama M98 hivi.

Sasa wewe unajua kabisa kuwa M200 si zote ni mauzo, nyingine ni michango ya msiba ilipitishwa kwenye akaunt yako, ila una sample za M50 zisizo na shaka kuwa ni pesa ya msiba na M150 inayobaki huna.

Afisa anapaswa kupiga kodi ya 150 ila anaweza futa hiyo hoja na kuchukua fedha kisha akatumia sample za M50 tu kumjibu bosi wake kuwa ongezeko ni fedha za msiba na akakuelekeza jinsi ya kujibu kwa kutumia sample tu. Hapo boss hatajua unless aamue kufanya hiyo kazi mwenyewe jambo ambalo si rahisi.
 
Naomba na yeye akumbushwe kulipia kodi ya mabango yake aliyojaza kwenye majabari nchi nzima mwaka 2015.
 
😄 hiyo haliwezekani

Landa atoke kiongozi chuma kweri kweri....

Alafu mbona simple sana,unaanza kuhakiki mali za wafanyakazi wa TRA tu 😄

Ova
 
Jambo hilo ni rahisi kweli kuelewa, lakini inashangaza viongozi wasomi ma Dr and PhD holders eti hawaelewi jambo rahisi kama hilo. Nchi kweli inaongozwa kisanii na wasanii.
Hawa ni wanaufaika wakubwa wa mfumo wa rushwa familia zao zinaogelea utajiri wa kupindukia, fuatilia watoto wao wanasoma wapi lakini watakwambia Rais ameboresha elimu
 
ANABWABWAJA TU CCM WOTE NI MAJIZI
 
Wanasiasa ni viumbe wa ajabu sana, Mwigulu anapata wapi moral authority ya kukemea rushwa wakati yeye anajulikana ni mwizi namba 2 nchi hizi?
 
Mwigulu mwenyewe ni mla rushwa.mabasi yake 120 ya masafa marefu alitoa wapi Hela zote ya kuyanunua Kwa mkupuo?
 
Yani nchi ilianza kwa kualibika toka kwa huyu jamaa
Hapa nchi imepigwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…