Mwigulu: Watumishi wala rushwa TRA watimuliwe na wafikishwe Mahakamani

Hivi vitu haviwezi kufichika daima. Mahali penye uhalifu huwa hapakosi mkosi. Wakusanya kodi wanaongezeka sana kutokana na idadi ya watu kuongezeka, kwa ajili hiyo wataanza kupigana vita wenyewe kwa wenyewe na hata kuuana. Kwa uhalifu huu hawawezi kubaki salama kwa muda mrefu. Yapo baadhi ya mambo lazima yatalipuka hivi karibuni.
 
Hao maboss wa TRA wanatamba Sana mtaani ndiyo maana na Sisi hatulipi Kodi, haiwezekani baadhi ya wafanyakazi waishi maisha ya wizi huku wafanyabiashara tukitaabika na biashara zetu...
Hakuna Fala anaweza kukubali kulipa Kodi kwenye mazingira hayaa

Kama vyombo vya dola vitafanya kazi yake sawasawa, kwenye kukusanya kodi kuna watuhumiwa wengi sana. Muda utakuja kuyaweka yote hadharani
 
Wanaiba sana tu,hasa mipakani wanahujumu
Mfanyakazi wa chini hawezi kuiba kama boss wake haibi

Takukuru ifutwe! Hakuna kazi wanayofanya nchini! Wanakula mishahara ya bure tu!
 
Naunga mkono hoja
 
Naona na Kamishna amekuja na moto Mpya 🔥🔥

View: https://twitter.com/Jambotv_/status/1813882790573732078?t=xL3zw6bHL4RosrKQ_mkC9w&s=19
 
Asante kwa mchango/shuuda nzuri dada ake.

Mimi jamaa yangu collin kapata ajira kwenye hiyo taasisi mwaka juzi tu ila kwa mambo aliyoyaona humo, akaniambia hili uweze kufanya biashara kwa mafanikio nchii hii hakikisha una ndugu wawili watatu ambao ni wafanyakazi wa TRA kwa ajiri ya kupindisha mambo huko kwenye system hili biashara yako iende, kama huna ni heri usifungue kabisa biashara.. na akatoa mfano wa baadhi ya jamii ambazo zinafanya vizuri Kibiashara kuwa ni lazima wawe na mwanafamilia hata mmoja huko.

Anasema sera na mifumo yetu ya kodi hasa ya makadirio ni ya kipuuzi mno na kila mtu anayefanya kazi kwenye hiyo taasisi anajua, ila imeachwa kwa makusudi tu...!! 🥲🥲
 
Sahihi kabisa kaka, Everyone know about this shit, and no one says shit about shit!

Tunaishi humo!
 
Je mawaziri wala rushwa ina kuwaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…