- Source #1
- View Source #1
kumekuwepo na chapisho ambalo linasamambazwa na moja ya ukurasa wa facebook likidai kuwa Inawezekana unatafuta dhahabu machimboni au madukani, lakini ukweli ni kwamba tayari unatembea ukiwa na dhahabu mwilini mwako!
Katika chapisho hilo wamedai kuwa Wanasayansi wamethibitisha kuwa ndani ya mwili wa binadamu kuna wastani wa miligramu 0.2 za dhahabu safi. Madini haya ya thamani yanapatikana ndani ya damu yetu yakifanya kazi zake za kibaolojia.
Sambamaba na hilo kumekuwepo na madai kuwa Hii ni dhihirisho tosha kuwa kila mmoja wetu ameumbwa akiwa na thamani kubwa tangu awali. Hivyo basi, thamani yako haitokani na kile unachomiliki kwa nje, bali kile kilichopo ndani yako!

- Tunachokijua
- Tafiti na makala za Sayansi zinabainisha kuwa mwili wa binadamu una madini ya dhahabu lakini ni kwa kiwango kidogo. Tovuti ya medicover genetics kupitia makala yao yenye kichwa "Your bllod is gold! Learn about componets of blood and symptoms and treatment of blood disorders" wanaeleza kuwa;
"Mwili wa mtu mzima una takribani lita 5 za damu ambazo zinajumuisha madini mbalimbali ikiwemo chuma, Kromiamu, Zinki na dhahabu kidogo kiasi cha Miligramu 0.2"
Jambo hili lilianza kujadiliwa kwenye kitabu cha The Elements cha John Emsley ambacho toleo la tatu lilichopashwa mwaka 1998 kinaleza kuwa kwa wastani mtu mwenye uzito wa kilogramu 70 anaweza kuwa na kiwango cha dhahabu chenye uzito wa Miligramu 0.2.
Licha ya kuwa dhahabu ipo kwa kiwango kidogo katika mwili wa binadamu laki ina uhumuhimu ikiwemo kuhusika katika baadhi ya michakato ikiwemo ya mawasiliano ya seli na afya ya viungo vya mwili. Hata hivyo kiasi cha dhahabu kinachopatika ni kidogo sana kiasi kwamba hakiwezi hata kuunda kitu kinachoonekana kwa macho.