"Mwili" wa Ivan uliingia Uganda kwa jina la Ally, Interpol wataka kaburi lifukuliwe

Ivan tena...mpaka anasahaulika yatasemwa mengi asee
 
Hatimaye Mahakama Kuu ya Uganda yatoa amri kaburi la Ivan Ssemwanga, yule mtalaka wa Zari, ambaye ni mke wa sasa Diakond Platinumz lifukuliwe, ili mamilioni ya pesa alizozikwa nazo zitolewe.

Mahakama imesema imechukua uamuzi huo ili kulinda heshima ya fedha ya nchi hiyo.

Mahakama imechukua uamuzi huo baada ya Mganda mmoja aitwaye Mgugu Abey, kuwashtaki Mahakamani kampuni iliyoraribu mazishi hayo ya A Plus Funeral Management na Benki Kuu ya Uganda,ambayo imeonekana ilizembea kwenye tukio hilo.

Hivyo, mahakama imeamuru kampuni ivunje kaburi kwa gharama zao,ili mlalamikaji achukue pesa hizo kwa niaba ya mataifa yenye fedha hizo, kwani zilikuwepo Rand za Afrika Kusini,Dola za Marekani pamoja na Shilingi za Uganda.

Kisha kampuni ya A Plus imeamriwa ilifukie kaburi hilo kwa gharama zake na kisha kumlipa ndugu Abey gharama zingine za usumbufu.Nakala ya huku inaletwa
Ama kweli mjini shule.
 
hii kesi tata sana, mshitakiwa akishindwa kutimiza inakuwaje?
 
haraka ya nini bob? hebu rekebisha title hiyo..
 
Hatimaye Mahakama Kuu ya Uganda yatoa amri kaburi la Ivan Ssemwanga, yule mtalaka wa Zari, ambaye ni mke wa sasa Diakond Platinumz lifukuliwe, ili mamilioni ya pesa alizozikwa nazo zitolewe.
Mtalaka wa Zari? Mke wa sasa wa Diamond? Mbona sielewi!...
 
una haraka yakuandikaa utadhani unakimbizwa kwani ungeandika bila kumuweka zari usingeeleweka
 
Ama kweli dunia ina mengi... Huku wat wanashinda njaa na kuhenya kisa chapaa na wengne wanazikwa nazo....
 
Hawawezi kuzikuta na wakibahatika kutoa vi nusu karatasi vyao watoe vishilling vyao na sio dolla zetu.

Watu wametoa povu eti ni kufuru kwani waliziiba? Wacha ya mungu yaende kwa mungu na za kaisai yaende kwa kaisai.

Kwanu situ, geneza na kaburi si vinatengenezwa kwa pesa mbona hizo haziwaumi?

Je wangeziweka ndani ya geneza wakakuta mtu alisaoza wanazitoa?

Wawe makini wataambulia buleee tusubiri.
 
Nilimwambia mtu mmoja hapa hizo fedha ztafukuliwa kwa amri ya mahakama. Ninachoshindwa kufahamu ni km hawa waliofikia uamuzi wa kumzika Ivan na fedha hawakujua kama hili jambo halikubaliki? Just a such a simple mind hawakujua?
 
Kwani HAWAKUUAGA MWILI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…