Mwili wa James Temba, aliyepotea umeokotwa mto Msimbazi ukiwa hauna kichwa

Mwili wa James Temba, aliyepotea umeokotwa mto Msimbazi ukiwa hauna kichwa

Dogo ni huyo 🥲
20260503_154903.jpg
 
Mwili wa James Temba aliyepotea siku kadhaa umeokotwa katika mto Msimbazi Dar es Salaam ukiwa hauna kichwa.

James Temba ni ndugu wa Mwanamziki wa kundi la TMK Wanaume Family, Mhe. Temba. James Temba alichukuliwa na watu wasiojulikana Jijini Dar es salaam siku kadhaa zilizopita, na jana mwili wake umeonekana ukielea mto Msimbazi Tabata huku ukiwa hauna kichwa.

Kupitia mtandao wa Kijamii wa Instagram, msanii Mhe. Temba amethibitisha kifo hicho kwa kuandika ''
Rest in peace my uncle James Temba Umeondoka bado mdogo wamekufanyia kitendo cha kikatili cha kukatisha maisha yako na kukata kichwa chako na kuondoka nacho ila kwa kuwa Mungu yupo hakika atatenda miujiza 🙏


Wakuu! Huu ukatili umepitiliza,, nini kipo nyuma ya pazia?!
Temba alikuwa na title, au influence gani kwenye jamii?
Tuanzie hapo.
 
Aisee...

Misiba ipo, ipo ya ajali za barabarani... misiba ya ugonjwa...

Lakini kuna misiba mingine usiombe ikukute, ni maumivu zaidi ya maumivu.

Utalia kwasababu ya marehemu amefariki...

Lakini ukikumbuka sababu ya kifo cha marehemu utalia zaidi.

Hii misiba ya hivi mingi huacha makovu makubwa kwenye mind za ndugu waliopatwa na hiyo misiba.

Aisee usiombe ikukute.
 
kuna loop hole kubwa sana la mauaji kwa sasa watu wanavisasi sana vijana tue makini na dhuluma zetu mtu unamzika lets say 35 ml kwa kujiona mjanja tu watu watakufyeka kwakua upepo saiv n dola ndio inachomoa watu wahuni wanaishi nao umo umo, kingine tuache kula vya watu kwanzia pesa mpka wake za watu
 
Matukio kama haya yakizoeleka kwenye jamii inakuwa hakuna aliye salama tena.

Hata husda tu au ugomvi wa kawaida tu mtaani unaibukiwa,unakatwa kichwa!Inaisha hivyo!

BTW: Huyo jamaa alikuwa anajishughulisha na nini? Ni mkosoaji?
 
Back
Top Bottom