Mwili wangu huwa unanuka mpaka sina raha ya kuishi

Mwili wangu huwa unanuka mpaka sina raha ya kuishi

Mkuu ushauri mzuri sana lakini umechemka hiyo vaseline ikichanganyika na hilo fumba kali basi inazidi kuharibu hali ya hewa. Atafute bondy spray nyingi ambazo ni deodorant. Harufu kali mara nyingi hutokea kwapani lakini hiyo ya kwenye korodani za jamaa hapo ni usafi wa nguo za ndani na aepuke kuvaa nguo mbichi au kabla hajijifuta maji vizuri kwenye korodani na mikunjo ya mapajani na sehemu za siri. Jamaa asirudie kuvaa boxer au chupi siku mbili. Pia asivae chupi kabisa avae boxer za cotton zile zilizo panapana hazibani nyeti. Anyoshe na pasi hizo boxer kabla ya kuvaa ili kuuwa vijidudu vinavyochangia perispiration.
asante mkuu nimesema vaselline sababu me nikinyoa napaka na kuna kuwa kuzuri sana
 
Kunywa maji ya kutosha kuanzia lita tatu kwa siku. Ukishaoga jisuuze na apple cider vinegar na kabla haujavaa hakikisha umejifuta maji uwe mkavu kabisa.
 
Hiyo harufu inasabishwa na jasho wakati nacheza mpira shuleni tulikuwa na jamaa akishika mpira ukimfata anatishia kukupaka jasho lake na ukimaliza mazoezi utaoga hata siku tatu harufu yake unayo tu.Jaribu kumfata doct. wa ngozi anaweza kukusaidia
 
Habarini wanafamilia,

Utotoni mwangu nilikuwaga hata sinuki lakini nilivyojiunga na shule ya boarding nikaanza kunuka kuanzia form 2. Basi nimekuwa ninanuka mpaka leo nimeishakuwa mtu mzima na ninategemea kuoa. Kazini kwangu hata kabla sijapishana na mtu basi huyo mtu ataanza kuziba pua na kama yuko mbali basi akiniona tu utamwona anatema mate au kuvuta koromeo la koozi kuashiria kwamba anajiandaa kukabiriana na harufu yangu mbaya.

Nimejitahidi sana mpaka kufikia kuzoea ratiba ya kuoga mara 3 kwa siku lakini wapi, nikioga nina kuwa salama kwa masaa mawili ya mwanzo lakini baada ya hapo ninakuwa kero kwa watu. Harufu mbaya inayowatesa wenzangu mimi siisikii lakini wao inawashinda. Nimekuwa nikiharibu siku za watu kila mara.

Sehemu ambayo nimekuja kugundua kwamba inato harufu hii ni kwenye mapumbu (Samahani kwa kutumia lugha kali lakini sina namna ya kuweka tafsida ya hili neno bila kuharibu maana). Nimekuwa nikiosha sana pumbu zangu usiku, mchana na asubuhi lakini haija saidia. Hakuna mtu duniani anayejitahidi kuoga kama mimi. Kuna ndugu zangu wengine anaweza asioge hata wiki lakini mimi nikioga muda huu baada ya masaa 3 ninanuka balaa. Mimi ni mtu mwembamba tu na wala umbo langu sio kubwa na wala sina mafuta mafuta lakini, hii harufu inaninyima raha ya kuwepo duniani.

Mimi ni mpole ukiniona lakini kiuhalisia mimi nilikuwaga mtundu sana na huu upole wangu wa sasa ni siri yangu, upole wangu ni kwa sababu ninanuka kwa hiyo sina amani ya kujitutumua mbele ya jamii inayo nizunguka. Inanibidi niwe mpooooole na tulivu hata muda mwingine nimekuwa mtu wa ndio mzee, sawa mkuu, ilimradi tu kuharakisha mtu asisimame na mimi kwa muda mrefu akaisikia harufu yangu kali akawa ananikimbia kwenye korido. Marafiki zangu wa kweli ambao tumeishi nao muda mrefu mpaka nimefanya pua zao kuzoea harufu yangu na wala hawaoni kama ninanuka, ukiwauliza watakwambia jinsi mimi nilivyo mtundu, mcheshi na mpenda sifa tena machepele kweli kweli dakika mbili mbele, lakini ni kwa hawa tu ambao kwao mimi sinuki bali ni shujaa na roll model wao pia.

Wadau naombeni msaada sana katika hili ili niweze na mimi kujihisi ni mtu wa kawaida kwa kuondokana na hili tatizo nguli katika maisha yangu.

Natanguliza shukrani zangu kwenu.
Pole sana mkuu.
Nina dawa ambayo utapona na gharama yake ni 50,000/ tu ambazo utazilipa baada ya kupona.
Njoo PM nikuelekeze dawa ambayo utaifanyia nyumbani kwako.
Kama huwezi kunitumia pesa baada ya kupona usiijaribu.
Nimeamua kuwekeza kwenye uchawi na uganga.
Siri ya ugonjwa huo ni kwambw hata kama ndo uwe umetoka bafuni kuoga ila baada ya dk chache lazima unuke na hata ukitumia marashi gani ila lazima unuke. Tena ukitumia marashi ndo utaharibu kabisa
Trust me utapona na utaleta ushuhuda hapa. Njoo pm
 
Pole sana......

Jaribu kutatua tatizo....

Zaidi zaidi jikubali mkuu ata usione soo mambo ya kawaida........!
 
Am sorry but nimeshindwa kujizuia[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pole sana mkuu, kama upo mikoa ya Pwani, jaribisha kuoga baharini kwa dakika 15 mpaka 20, mara mbili kwa siku, asubuhi na jioni mfululizo kwa muda wa wiki moja.
 
Pole sana kinjana. Kila eneo la mwili lina bakteria ambao ni rafiki tunaishi nao. Kwapani, kinywani tumboni kwenye makalio na ht sehemu ulizotaja. Hawa bakteria wanapokuwa wengi wanapotoa uchafu wao ndio unaotoa hiyo harufu. Kutokana na mfumo wako wa maisha inaonesha eneo hilo bakteria wamekuwa wengi kuliko inavyotakikana. Ningekushauri uache kunywa pombe za kienyeji (samahani) halafu kila uogapo osha nyeti kwa limao usisugue! Halafu jipime km una URTI. Usiingiw gharama za vipodozi kabla ya kujua ttz. Maji unakunywa kiasi gani kwa siku?
 
Pole sana kama umeshajaribu hospital ikashindikana, mwone shekh sharifu majini yupo mabibo atakuombea utabaki na amani Poleee
 
Pole sana mkuu.
Nina dawa ambayo utapona na gharama yake ni 50,000/ tu ambazo utazilipa baada ya kupona.
Njoo PM nikuelekeze dawa ambayo utaifanyia nyumbani kwako.
Kama huwezi kunitumia pesa baada ya kupona usiijaribu.
Nimeamua kuwekeza kwenye uchawi na uganga.
Siri ya ugonjwa huo ni kwambw hata kama ndo uwe umetoka bafuni kuoga ila baada ya dk chache lazima unuke na hata ukitumia marashi gani ila lazima unuke. Tena ukitumia marashi ndo utaharibu kabisa
Trust me utapona na utaleta ushuhuda hapa. Njoo pm
Mkuu wewe ni mshirikina
 
Nenda hospitalii ,nahisi una tezi (gland) ambayo Ina kuletea tatizo hilo na dawa ni kuliondoa kwa upasuaji mdogo
 
Mkuu wewe ni mshirikina
Mkuu kama una hilo tatizo sema nukusaidie utapona ndani ya week Tatu. Namshangaa anayetafuta ushauri kaebda mazima. Ni dawa za uhakika. Mimi sio mshirikina mkuu. Ila ukijichanganya siyo mbaya pia
 
Back
Top Bottom