TANZIA Mwimbaji maarufu kundi la Zabron Singers, Marco Joseph afariki dunia

TANZIA Mwimbaji maarufu kundi la Zabron Singers, Marco Joseph afariki dunia

Poleni sana kikundi cha Zablon Singers, familia, marafiki na wapenzi wa nyimbo za gospel.

Kikundi cha Zablon Singers ni kwaya pekee iliyoweza kuvuka views 50,000,000 kutazamwa wimbo wake wenye title ya "Tumeuona Mkono wa Bwana" katika account yake ya YouTube

View attachment 3076182

MKONO WA BWANA by Zabron Singers (SMS SKIZA 8561961 TO 811)

59M views​


Kimataifa kwaya hii imeweza kuhudumu katika shughuli kubwa ikiwemo katika uapisho wa rais wa Jamhuri ya Kenya


View: https://m.youtube.com/watch?v=ByHAn9HIkfo

Kama hujaimbiwa hii nyimbo harusiyako ujue una gundu
 
Mwimbaji wa kundi la Zabron Singers, Marco Joseph amefariki dunia kwa ugonjwa wa Moyo jana usiku akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Shemeji wa marehemu, Tecla Lucas ameiambia Mwananchi leo Agosti 22, 2024 kuwa mwili wa marehemu bado upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali hiyo, wakisubiri ratiba za mazishi kupangwa.

"Amefariki kwa ugonjwa wa moyo akiwa Hospitali ya Muhimbili jana usiku msiba utakuwa Mikocheni kwa mama yake mdogo, mwili kwa sasa bado upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti,"amesema Tecla
Rip mwimbaji..🙏
 
Mwili wake umekufa, ila roho pamoja na sauti yake, wimbo na ujumbe wake utaishi milele na milele! Kuna watu wamekufa ila kama hawajafa na wengine wakifa ndio wamekufa.
 
Back
Top Bottom