Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Kwa niaba ya familia ya Mwinyi Mkuu Mohammed Saidi Katundu, kwa masikitiko makubwa kabisa tunatangaza kupotelewa na Baba yetu Mzee Mwinyi Mkuu Mohammed Saidi Katundu katika tukio ambalo lilitokea mkoani Mtwara wilaya ya Tandahimba alfajiri ya tarehe 15 Novemba 2019.
Baba yetu alikuwa nyumbani na familia yake baada ya kurudi kutoka kwenye shughuli zake za kuuza bidhaa zake mtaani almaarufu kama machinga. Ghafla usiku wa saa nane alivamiwa na watu ambao walijitambulisha kama maafisa usalama. Lakini cha kushangaza, waligoma kutoa vitambulisho vyao na kwa kuwa walikuja na silaha za moto ilibidi mzee wetu akubali kuongozana nao. Walimchukua pamoja na kubeba vitambulisho vyake vyote ikiwemo hati yake ya Kusafiria (passport). Hadi usiku wa siku hii ya leo (18 Novemba 2019) ni siku ya nne na hatufahamu mzee wetu yuko wapi.
Tumejitahidi kufanya juhudi za kumtafuta lakini juhudi zetu zote zimegonga mwamba huku Jeshi la polisi likikanusha kumshikilia au kuhusika na kumkamata Mzee wetu. Tunatoa wito kwa Watanzania wote, mwenye kupata taarifa kuhusu mzee wetu, awasiliane na familia haraka iwezekanavyo.
Imetolewa na Mbarouk Khan (simu: ..0672289926, 0658112230, 0716840684
Chanzo: Ukurasa wa Facebook wa Zitto Kabwe
My Take:
Tulitegemea baada ya mabadiriko TISS mambo ya utekaji na upoteaji hovyohovyo wa raia yangekomeshwa.
Lakini cha kusikitisha kumbe mambo yanaendelea business as usual!
Kama ni vyombo vya serikali vinahusika basi ukamataji wa raia una taratibu zake za kisheria lakini hii ya kuvamia watu na kuwapoteza haijakaa sawa.
Serikali itoe maelezo, huyu mwananchi yuko wapi na amechukuliwa na nani?
Haya mambo ni lazima tuendelee kukemea, huyu mtu ana familia yake inayomtegemea kama ana kosa basi afikishwe mahakamani siyo kupotezwa!.