Mwinyi Mkuu Katundu atekwa na wanaodaiwa kuwa wanausalama, hajulikani alipo. Huu ni mtihani wa kwanza kwa Diwani Athuman

Mwinyi Mkuu Katundu atekwa na wanaodaiwa kuwa wanausalama, hajulikani alipo. Huu ni mtihani wa kwanza kwa Diwani Athuman

Inshu hapo sio kuwa na passport, au huwa ana kwenda wapi, mnacho fail, ni kitu kidogo tu, njia za ukamataji, kwani ukiwatuma polisi wakaenda mchana tu, na kumkamata, na taratibu nyingine zikafuata, kuna tatizo? Kwani serikali zote huko nyuma hakukuwa na watu kama hawa?lakini approach haikuwa hii!! Ilani njia moja ya serikali zile zinazotisha wananchi!! Halafu unasikia viongozi wa dini wanatoa mapambio ya kusifia tu ili mambo yao yanyooke tu!! Bora yeriko nyerere anayeabudu mizimu ya mababu.
Tunacho fail? Kwamba na mimi nimo? Ahahah mkuu hapo unanionea... Lakini pia tukirudi kwenye mada, kuna vitu vingine hivi vyombo haviwezi kuingiliana kwa sababu za kiusalama zaidi..
 
Amechukuliwa usiku wa manane na watu waliojitambulisha kwamba ni askari ambao walikataa kutoa vitambulisho, sasa kwa nini wanafamilia walisubiri siku nne? Kwanini hawakuanza kufuatilia usiku huo huo? Siku hizi kuna simu za mkononi Je, walianza hizo pilika pilika na kuuliza?

Post ya Zito inaonyesha kwamba TISS wanahusika, Je, anao ushahidi?
Itakuwa ndio kwanza Leo una sikia hili saga...
 
Wait a minute, yaani machinga ana hati ya kusafiria ?? ( Passport)?? kuna harufu ya jambo hapa.
Hii post ya pili inayoshangaa machinga kuwa na pass
Kwani passport ni bei gani na wewe unamchukuliaje mtu anayemiliki pass
 
Mmachinga mmoja anayeonekana kwenye MKOKO hapo juu, amenyang'anywa vitambulisho vyake vyote ikiwamo HATI YAKE ya Kusafiria.
Machinga hana uwezo wa kunua? Hastahili kununua Mali anayo taka na kuimiliki? Je ndg zake hawa ruhusiwi kumsaidia? Kumnunulia ? Kumjengea? Ukiwa machinga hutakiwi kufanya maendeleo?
 
Mmachinga anamiliki hati ya kusafiria? Anafanya biashara za mpakani au!! Mfano Mtwara kwenda Msumbiji!!!

Wanafamilia walitakiwa kutuelezea kidogo kwa kina, nje ya hizo shughuli zake za umachinga, huyo Mwinyi anajishughjlisha na nini! Ni mwanasiasa, ni sheikh, ni mwanaharakati, nk. ili kuindoa sintofahamu.
 
Juzi wamechinjwa watu 20 kama kuku hatukuona MY TAKE kwenda zako
Sizani kama kuna watu 20 walio chinjwa... Zitto ana jarbu kusema kama ni mhalifu utaratbu ufatwe, na wengine wana sema itafikia hatua tutashindwa kutofautisha kati ya majambazi na maafisa wa usalama au poolisi
 
Wait a minute, yaani machinga ana hati ya kusafiria ?? ( Passport)?? kuna harufu ya jambo hapa.
Wewe una ndg wakulima na upo marekani, hawa ndg wana takiwa wawe na kitu gani ili waje kukuona huko ulipo, au kukusalimia,

Uzuri passport haikusemwa kama ni fake hivyo ana miliki kihalali, pia ni machinga au mfanyabiashara
 
Walipouawa watu 6 huko ntwara sijasikia mkikemea..
Serikali ina shughulikia hilo swala ndio maana kila RAIA ana amani, huku pia tukifatilia kupata taarifa ya yanayo jili... Tuna ndg wapo msumbiji mtwara nk...

Ila kuna ishu zingine hazitolewi taatifa yoyote ndio ukakasi wa RAIA una anza hapo na kuona kuna tatizo

Watanzania sio wajinga...
 
Wewe na ushamba wako unadhani kumiliki pass ya kusafiria ni anasa. na kama alienda hijja?

Kuuliza siyo ujinga! Unaweza tu ukanifahamisha bibie! Sasa unataka wote tuwe wa mjini kama wewe!! Mimi naongelea katika uhalisia! Mmachinga kumiliki hati ya kusafiria.
 
Kwa niaba ya familia ya Mwinyi Mkuu Mohammed Saidi Katundu, kwa masikitiko makubwa kabisa tunatangaza kupotelewa na Baba yetu Mzee Mwinyi Mkuu Mohammed Saidi Katundu katika tukio ambalo lilitokea mkoani Mtwara wilaya ya Tandahimba alfajiri ya tarehe 15 Novemba 2019.

Baba yetu alikuwa nyumbani na familia yake baada ya kurudi kutoka kwenye shughuli zake za kuuza bidhaa zake mtaani almaarufu kama machinga. Ghafla usiku wa saa nane alivamiwa na watu ambao walijitambulisha kama maafisa usalama. Lakini cha kushangaza, waligoma kutoa vitambulisho vyao na kwa kuwa walikuja na silaha za moto ilibidi mzee wetu akubali kuongozana nao. Walimchukua pamoja na kubeba vitambulisho vyake vyote ikiwemo hati yake ya Kusafiria (passport).

Hadi usiku wa siku hii ya leo (18 Novemba 2019) ni siku ya nne na hatufahamu mzee wetu yuko wapi.
Tumejitahidi kufanya juhudi za kumtafuta lakini juhudi zetu zote zimegonga mwamba huku Jeshi la polisi likikanusha kumshikilia au kuhusika na kumkamata Mzee wetu. Tunatoa wito kwa watanzania wote, mwenye kupata taarifa kuhusu mzee wetu, awasiliane na familia haraka iwezekanavyo.

Imetolewa na Mbarouk Khan (simu: ..0672289926, 0658112230,0716840684
76765459_2705396669481013_4293865057067991040_n.jpg
 
Back
Top Bottom