Mwinyi Mkuu Katundu atekwa na wanaodaiwa kuwa wanausalama, hajulikani alipo. Huu ni mtihani wa kwanza kwa Diwani Athuman

Wilaya ya Tandahimba ni kubwa kijijiji gani? Ili tuweze wasiliana na jamaa zetu huko kuwaulizia mambo yalikuwaje hasa
 
Nani alikudanganya kuwa zamani polisi uongozi wa wa mtaa unaambatana nao? Ulisoma wapi? Unaongolea Tanzania au nchi nyingine?
 
Mzee Katundu amepatikana, Amepatikana akiwa mzima wa Afya lakini akiwa na uchovu mwingi, Mazingira ya kuachiwa kwake hayana maelezo ya kuridhisha lakini amekiri kuachiwa na waliomteka.

Asante wana JF kwa kupaza sauti dhidi ya vitendo vya kikatili, kinyume cha sheria, vya uhuni vya kishenzi vya utekaji wa raia.

Sisi sote kwa umoja wetu tuendelee kupiga kelele ili matendo kama haya tuliyokuwa tukiyasikia yakitokea huko kwenye nchi nyingine kwenye tawala dhalimu yakianza kutokea katika nchi yetu.

Kila mmoja akatae Thuggish, unlawful, oppressive na inhumane treatment ya wananchi kinyume cha sheria. Wananchi sharti walindwe dhidi ya matendo ya kihuni ya aina hii

 
Nashangaa sana wanaouliza mmachinga kuwa na hatinya kusafiria.
Nawapeni tu taarifa huyu ni machinga maarufu wa kuuza marash ya kisunni kkoo huwa ana kibaiskeli chake. Aliwah kuishi arabuni.miaka.ya nyuma sana. Kkoo ana nyumba lkn pia mtwara ndiko inakokaa familia yake.

Btw kapatikana jana usiku akiwa kachoka sana na familia.yale.imesema itaongea leo
 
Mleta uzi pole yake lakini ni mbumbumbu. Mtu akijitambulisha ni askar Tayari ni askari? Kwa nini hamkujitolea wanafamilia watano kuongozana naye mkaone kituo anachopelekwa kisha mrudi nyumbani?
Imetajwa kuwa watekaji walikuwa na silaha za moto. Ungelikuwa wewe ungefwata mkia? Hayo mambo sikia yakitokea kwa wengine usiombe yakukute.
 

Hivi now days mtu akipotea tu anakuwa ametekwa
 
Atakuwa anafadhili ugaidi huyu
 
Mzee huyu ameachwa huru

Kupitia kwenye mjadala huu ni wazi watu wenye kanzu na ndevu wanatazamwa kwa chuki sana

Watu wamekwenda mbali kujenga kila aina ya dhana dhidi yake kwa kuwa mioyo imebugizwa chuki tuuuuu
 
Muogope Mungu, Si vizuri kumdhania mtu dhana mbaya bila ushahidi.
Usihukumu, usije ukahukumiwa, Kama huna ushahidi wa Jambo muachie Mungu ahukumu.
Hujafa hujaumbika!
We unaonaje, watu wamechinjwa Msumbiji na mpakani mwa Mtwara hamkupiga kelele, leo kachukuliwa mmoja tu kelele dunia nzima!! au waliochinjwa ni kuku? mmachinga gani anarudi usiku wa manane, ana hold passport, anaishi good life naona hata kwenye picha anaandaa msosi kwa gas coocker! ha ha ha ha ha haaa inataka moyo kuamini!
 
Tunasubiri atoroke kutoka huko alipo ili aje kufungua malalamiko yake ndipo tuweze kufuatilia.
Roma alishasema yaliyomsibu au Mo????? Tusubiri ipo siku wajukuu wetu wataandika wakati tumeshaoza makaburini. Mungu wao anawaona kama yupo. Huyo Mungu anayekaa kimya wakati watu wanateseka kwanini. Kutoka Misri Manna ilimwagwa jangwani kama ni kweli je sasa iweji dunia inalia au Mungu wamekuwa wengi na wanagawana majukumu?
 
Huyu ni zaidi ya Machinga. Kuna mahali amekosea!!!! Hati ya kusafiria!!!. Ukiangalia na mwonekano wake katika picha basi inatosha. Poleni ndugu zake.
 
Huyu ni zaidi ya Machinga. Kuna mahali amekosea!!!! Hati ya kusafiria!!!. Ukiangalia na mwonekano wake katika picha basi inatosha. Poleni ndugu zake.

Hati ya kusafiria kwani sh ngapi?
Ni sh 150000 tu
Yaani unahukumu uhalifu wa mtu kwa muonekano?,
Ina maana Waislamu wote wenye muonekano wa Ibada wote ni magaidi?
Acheni unyanyapaa kwa binadamu wenzenu, Ni ukatili huo
 

Upande wa pili ukija ku balance story tunaweza kushangaa
 
Upande wa pili ukija ku balance story tunaweza kushangaa

Matokeo ya utekaji yameshamiri nchini, na huu ni muendelezo tu wa utekaji kama alivyotekwa Roma, Mo, Ben. Saanane, Kanguye na Azory Gwanda.
Hakuna cha kubalance story hapo.
 
Matokeo ya utekaji yameshamiri nchini, na huu ni muendelezo tu wa utekaji kama alivyotekwa Roma, Mo, Ben. Saanane, Kanguye na Azory Gwanda.
Hakuna cha kubalance story hapo.

Kuna mwanasheria Arusha rafiki yangu na hakimu wa serikali walitekwa tukahangaika weeeeeee! Baada ya mda wakaonekana kituoni na tuhuma halali kabisa za kusikitisha!

Wakati mwingine vyombo vya I salama (kama basi ni wao) wanafanya kazi kwa utaratibu wao ili wasivuruge uchunguzi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…