Mwisho mbaya wa aliyekuwa Rais wa Sierra, Leone Valentine Esegragbo Melvine Strasser

Mwisho mbaya wa aliyekuwa Rais wa Sierra, Leone Valentine Esegragbo Melvine Strasser

Nazielewa vema enzi za Rais Bwana huyu ambaye alipokuwa Rais hakuwa na utani na rushwa, hakuwa na tamaa za kujilimbikizia mali wala madaraka na zaidi sana alifungua milango ya demokrasia. Wa-Siera Leone wanajitia aibu wenyewe kumdhalilisha na kuidhalilisha Afrika nzima, tena wanajiletea maafa makubwa kwa kuwatafutia waroho sababu za kujilimbikizia mali na madaraka wanapokuwa madarakani ili "yasije yakawapata yanayompata mwenzao."
Hata Nyerere wetu (RIP) kama si busara za wabunge walioibana serikali kumboreshea mazingira ya kuishi angeishia kuwa masikini kabisa kule kwao Butiama. Maana Mzee yule hakuwa amejilimbilikizia mali yoyote wala kupitisha miswaada ya sheria za kumtengenezea maisha ya ujiko baada ya kustaafu.

Kwa hiyo wanawake wa sasa,moyo wa huruma hawana tena,eeh...

Ama Ellen Johnson Sirleaf ni rais wa nchi gani?
 
Je kwenye orodha ya kundi la pili yupo na M7 wa Uganda?
Mkuu pamoja na Africa kupita katika njia ngumu sana kuelekea demokrasia lakini pia katika njia hiyo tulipata viongozi kadhaa wazuri ambao hawakuingia madarakani kwa njia ya sanduku la kura. Ila kwa bahati mbaya sana viongozi hao hawakudumu madarakani pamoja na nia hao nzuri ya kuwafumikia wananchi wao. Waliondolewa na mabeberu ambao waliona mirija yao ndani ya bara la africa imezibwa. Viongozi hao ni kama Tom Sankara na huyu Valentine Stresser. Wengine waliingia madarakani wakiwa na nia njema ila wakaa madarakani kwa muda mrefu na kujisahau kabisa na kuanza kuwa miungu watu; hawa ni kama akina Col. Gaddafi, Master Sergeant Samwel Doe na sasa tunamuona huyu Yahya Jammeh. Mwisho wa hawa wa kundi la pili huwa mbaya sana. Bado tunasubiria mwisho wa Yahya Jammeh na akina Blaise Compaore.
 
Je kwenye orodha ya kundi la pili yupo na M7 wa Uganda?


Hakika mkuu Mseveni yupo kundi hilo la pili. Alipoingia madarakani mwaka 1986 kwa kumfukuza Okello, Mseveni alikuwa akiongea maneno ya kimapinduzi kwelikweli na alifanya kweli mwanzoni lakini sasa unaona naye amekuwa king'ang'anizi. Tusimsahau Gen. Kagame ambaye japo anaendelea kufanya vizuri lakini anakoelekea sioni mwisho mzuri kwake inabidi ajipange kupumzika kwa amani asije akapimzishwa.
 
Kwa hiyo wanawake wa sasa,moyo wa huruma hawana tena,eeh...

Ama Ellen Johnson Sirleaf ni rais wa nchi gani?

Huyu mama ni Rais wa Liberia. Nadhani unamkimbuka Master Seargent Samwel Doe na akina Charles Taylor.
 
Anaitwa Valentine Esegragbo Melvine Strasser alikuwa Rais wa Sierra Leone from 1992 to 1996 na alitwaa madaraka kwa mapinduzi ya Jeshi. Alitwaa madaraka akiwa na umri wa miaka 25 tu, hapo unamuona amepigika maisha magumu!

yaani huyu ndo ***** kweli..yaani badala ya kufungua akaunti awe na visa card alikuwa anashangaa tu..anapigika sasa..hahaaaaa pole we rais mstaafu
 
Mkuu sina hakika na hilo. Najua Okello huenda alitumiwa na akina Abdulrahman Mohamed Babu ambaye.alikuwa na mahusiano na Cuba. Ila hil la Okello kuwa polisi sina hakika sana na hata hiyo Wikipedia page inayohusu upolisi wa Okello haina mashiko sana. Wikipedia ina matatizo mengi. Iangalie upya utaona matatiz yake.


Huenda umeshajibiwa huko kwa vile sikusoma post zote, ila Okelo alikuwa ni polisi.
 
Mkuu fuatilia utabaini. Okello alikuwa mpagazi

Vitabu vyote nilivyosoma kuhusu Okelo wakati wa mapinduzi vinaonyesha kuwa alikuwa polisi. Niliwahi kumsikiliza Bridegia Yusuf Himid wakati akiwa brigedi kamanda wa magharibi mwishoni mwa miaka ya sabini katika moja ya mihadhara yake katika shule za Tabora aliizungumzia kuwa walimtumia Okelo kastika mapinduzi kwa vile alikuwa ni polisi aliyekuwa anatisha watu sana. Wakati anaingia zanibar kutokea uganda kweli akiwa mpagazi, lakini hadi wakati wa mapinduzi yale alikuwa ni askari wa polisi. Neno askari lina maana pana sana, kiasi kuwa linachanganya professional soldiers na kuruta, kwa hiyo ingawa Okelo hakuwa professional police officer, lakini alikuwa ni polisi kulingana na rekodi za washirika wake.

---------

Nyongeza: Angalia pia hapa - http://en.wikipedia.org/wiki/John_Okello
 
vitabu vyote nilivyosoma kuhusu okelo wakati wa mapinduzi vinaonyesha kuwa alikuwa polisi. Niliwahi kumsikiliza bridegia yusuf himid wakati akiwa brigedi kamanda wa magharibi mwishoni mwa miaka ya sabini katika moja ya mihadhara yake katika shule za tabora aliizungumzia kuwa walimtumia okelo kastika mapinduzi kwa vile alikuwa ni polisi aliyekuwa anatisha watu sana. Wakati anaingia zanibar kutokea uganda kweli akiwa mpagazi, lakini hadi wakati wa mapinduzi yale alikuwa ni askari wa polisi. Neno askari lina maana pana sana, kiasi kuwa linachanganya professional soldiers na kuruta, kwa hiyo ingawa okelo hakuwa professional police officer, lakini alikuwa ni polisi kulingana na rekodi za washirika wake.

---------

nyongeza: Angalia pia hapa - http://en.wikipedia.org/wiki/john_okello

labda polisi jamii
 
Hakujiandaa kuwa rais, alibahatika kuwa msitari wa mbele kwenye maandamano na urais ukamwagukia.
 
Habari za mchana ndugu wanajamii,

Naomba kumjua huyu mtu anaeitwa Valentine Strasser aliepata kua rais wa nchi ya Sierra Leone akiwa na umri mdogo wa miaka 25.

Naomba kuwasilisha.
 
Ungejaribu hata kuingia kwenye google uone kama utapata habari zake. Kama kuna kitu specific hutapata au kuelewa ndy uombe msaada.
 
Nimegoogle ila nimepata kwa ufupi sana, ndiyo maana nikaonelea kua wadau wanaweza kua na michango zaidi na zaidi
 
Valentine Strasser alipata kuwa Rais wa Sierra Leone. Wakati akiingia madarakani aliweka rekodi ya kuwa kiongozi mwenye umri mdogo kuwahi kutokea. Hata sasa, hakuna taifa ambalo limewahi kupata Mkuu wa Nchi mwenye umri chini ya miaka 25 ili avunje rekodi ya Strasser.

Aprili 29, 1992, Strasser akiwa kijana mwanajeshi mwenye umri wa miaka 25, aliwaongoza wanajeshi wenzake kuvamia Ikulu ya Sierra Leone, wakamteka aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Joseph Saidu Momoh, wakamlazimisha kukimbia, naye akatorokea Conakry, Guinea.

Baada ya Momoh kutorokea Conakry, Strasser alijitangaza kuwa Rais wa Sierra Leone. Maisha yakabadilika, alishakuwa Mkuu wa Nchi, kwa hiyo hakutaka kuishi kwenye nyoyo za Wasierra Leone.
Hakulipa malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma. Alifuja almasi ya Sierra Leone, kwa vile jina lake ni Valentine, basi sikukuu ya Valentine’s Day akaifanya kuwa sherehe ya kitaifa yenye mapumziko.
Strasser alikuwa na mbwembwe nyingi, mwaka 1993 katika mkutano wa Wakuu wa Serikali katika nchi za Jumuiya ya Madola, uliofanyika Limassol, Cyprus, alitinga kwa mbwembwe akiwa amevaa suruali ya jeans na fulana yenye maandishi Sunny Days in Cyprus (Siku za Jua Kali Cyprus).

Alikuwa mtu wa starehe, vurugu nyingi kwa wanawake, aliua watu wasio na hatia. Strasser alisahau kuwa ipo siku uongozi hautakuwa kwenye mikono yake, na ambacho kinaweza kumfaa ni kuishi ndani ya mioyo ya watu ili wamtetee na kumpigania baadaye.
Januari 16, 1996, Strasser alipinduliwa na msaidizi wake, Brigedia Jenerali Julius Maada Bio. Strasser akakimbilia Uingereza, akajiunga na Chuo Kikuu cha Warwick, kilichopo mjini Coventry, akaanza masomo ya sheria, akasema anataka awe wakili ili awatetee Waafrika.

Mwaka mmoja wa masomo, Strasser aliishiwa fedha, akaacha chuo. Maisha Uingereza yakawa magumu, akakimbilia Gambia nako kukawa pagumu, mwisho akarudi Sierra Leone, mjini Grafton, Mashariki ya Mji Mkuu wa nchi hiyo, Freetown.
Kazi ya kwanza ambayo Strasser aliifanya ikawa kuanzisha kichuo kidogo cha kufundisha kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama). Maisha ya chuo yakamshinda.

Baada ya kila kitu kwenda kombo, Strasser alirudi nyumbani kwa mama yake mzazi na kuishi kwenye banda la uani. Hata sasa, akiwa na umri wa miaka 49, anakunywa pombe za kienyeji mtaani. Hana hadhi yoyote kama kiongozi mkuu wa nchi mstaafu.
Strasser anaishi kama mtu tu mtaani. Mlevi na hakuna anayemjali. Hana mtu wa kumtetea wala kumpigania kwa sababu hakuishi kwenye nyoyo za watu. Strasser ndiye Mkuu wa Nchi wa zamani, anayeishi kimaskini kuliko wote duniani.

Ukiwa kiongozi na kugeuka kituko kama Strasser inawezekana kabisa. Ishi vibaya na watu wasikupende, akija mtawala ambaye hatakutambua kama mkuu uliyepita, unaweza kuishi maisha ya hovyo kama ombaomba mtaani au mnywa gongo uliyeshindikana.
Jifunze sasa kwamba ukiishi vizuri kama kiongozi, hata baada ya kutoka au kutolewa, jamii itakuenzi, itakupenda, kukupigania na kukutetea ukiwa nje ya ulingo na hutaishi vibaya. Ukiishi vibaya, utakuwa na mwisho mbaya kama Strasser.
 
Habari za mchana ndugu wanajamii,

Naomba kumjua huyu mtu anaeitwa Valentine Strasser aliepata kua rais wa nchi ya Sierra Leone akiwa na umri mdogo wa miaka 25.

Naomba kuwasilisha.
Niliwahi kusoma kuhusu huyu jamaa. Alipata madaraka siyo kwa mapinduzi ya kupanga. Wakati huo Sierra Leone wanajeshi wa vyeo vya chini walikuwa na hali mbaya kiuchumi hadi walikuwa wanakosa sare. Hivyo wakaandama kwenda ikulu kupeleka malalamiko yao kwa rais. Baada ya rais kuona kundi la wanajeshi linaingia ikulu akadhani wamekuja kumpindua na akakimbia. Hivyo dogo alikuwa kinara wa maandamano akaokota dodo kwenye mnazi. Ila kwa sasa anagonga mnazi kama teja vile.
 
Back
Top Bottom