Mwisho mbaya wa aliyekuwa Rais wa Sierra, Leone Valentine Esegragbo Melvine Strasser

Mwisho mbaya wa aliyekuwa Rais wa Sierra, Leone Valentine Esegragbo Melvine Strasser

Ajitambulishe kwa jamaa wa guiness book of records anaweza kupata mihela ya kukaa viti virefu.
 
wpid-captain-valentine-strasser-27-leader-of-the-provisional-ruling-council-b3r27y.jpg
55f4410668784d749b977cb3c639b6b7.jpg

juu akiwa kijana na picha ya chini hali aliyonayo sasa
 
*MJUE RAISI WA ZAMANI WA SIERRA LEON*.- *Valentine Strasser*



Kutoka Urais Hadi Ombaomba Mtaani
*DUNIANI* tunajifunza na kuona vitu vingi tofauti vya kushangaza, kuogofya na kufurahisha. Wengi hawamjui *Valentine Strasser* ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi ya *Sierra Leone* kati ya Aprili 29, 1992 hadi Januari 16 , 1996 akiwa ndiye amiri jeshi mkuu na kiongozi wa ngazi ya juu kwenye taifa hilo lililopo kaskazini-magharibi mwa bara la Afrika.Wakati akiingia madarakani aliweka rekodi ya kuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi, yaani akiwa na chini ya miaka 25.

Aprili 29, 1992, Strasser akiwa kijana mwanajeshi mwenye cheo cha kapteni, akiwa na umri wa miaka 25, aliwaongoza wanajeshi wenzake kuvamia Ikulu ya Sierra Leone, walimkuta rais amejificha ndani ya kabati lililopo kwenye chumba cha kuogea, kisha wakamteka *Rais Joseph Saidu Momoh* na wakamlazimisha kukimbia, naye akatorokea *Conakry, Guinea*.


Strasser alichukua madaraka ya nchi hiyo siku tatu tangu ashehereke sikukuu yake ya kuzaliwa.
Baada ya Momoh kutorokea Conakry, Strasser alijitangaza kuwa Rais wa Sierra Leone. Aliwaongoza vijana wenzake sita waliofanikisha mapinduzi hayo na kuunda serikali ya mpito waliyoipa jina la *National Provisional Ruling Council* *(NPRC).*

Maisha yakabadilika, alishakuwa mkuu wa nchi, kwa hiyo hakutaka kuishi kwenye nyoyo za Wasierra Leone.
Hakulipa malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma.
Alifuja almasi ya Sierra Leone, kwa vile jina lake ni Valentine, basi sikukuu ya Valentine’s Day akaifanya kuwa sherehe ya kitaifa yenye mapumziko huku sherehe kubwa ikiandaliwa ikulu ya nchi hiyo.

Strasser alikuwa na mbwembwe nyingi, mwaka 1993 katika mkutano wa wakuu wa serikali katika nchi za Jumuiya ya Madola, uliofanyika *Limassol, Cyprus*, alitinga kwa mbwembwe akiwa amevaa suruali ya jeans na fulana yenye maandishi Sunny Days in Cyprus (Siku za Jua Kali Cyprus).
Alikuwa mtu wa starehe, vurugu nyingi kwa wanawake, aliua watu wasio na hatia.

Strasser alisahau kuwa ipo siku uongozi hautakuwa kwenye mikono yake, na ambacho kinaweza kumfaa ni kuishi ndani ya mioyo ya watu ili wamtetee na kumpigania baadaye. Januari 16, 1996, Strasser alipinduliwa na msaidizi wake, *Brigedia Jenerali Julius Maada Bio.*
Strasser akakimbilia Uingereza, akajiunga na Chuo Kikuu cha Warwick, kilichopo mjini Coventry, akaanza masomo ya sheria, akasema anataka awe wakili ili awatetee Waafrika.
Mwaka mmoja wa masomo, Strasser aliishiwa fedha, akaacha chuo.

Maisha Uingereza yakawa magumu, akakimbilia Gambia nako kukawa pagumu, mwisho akarudi Sierra Leone, mjini Grafton, mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Freetown.
Kazi ya kwanza ambayo Strasser aliifanya, ikawa kuanzisha kichuo kidogo cha kufundisha kompyuta na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama). Maisha ya chuo yakamshinda.
Baada ya kila kitu kwenda kombo, Strasser alirudi nyumbani kwa mama yake mzazi na kuishi kwenye banda la uani.

Hata sasa, akiwa na umri wa miaka 49, anakunywa pombe za kienyeji mtaani.

Hana hadhi yoyote kama kiongozi mkuu wa nchi mstaafu. Strasser anaishi kama mtu wa kawaida tu mtaani. Mlevi na hakuna anayemjali.
Hana mtu wa kumtetea wala kumpigania kwa sababu hakuishi kwenye nyoyo za watu. Strasser ndiye mkuu wa nchi wa zamani, anayeishi kimaskini kuliko wakuu wote wa nchi duniani.
Ukiwa kiongozi na kugeuka kituko kama Strasser inawezekana kabisa.

FUNZO KWA VIJANA WENYE DHAMANA.- Tunapo Aminiwa na Kupewa Madaraka Tusilewe Sifa Tusisahau Tulipotoka na Tusione Tumefika... Uongozi Ni Dhamana na Madaraka Ni Amana kutoka Kwa Mungu,Unaweza Kupewa Madaraka na Umri Mdogo na Mwenendo wako Ukakupelekea Kuhitimisha Safari Yako Ya Uongozi Ukiwa na Umri Mdogo zaidi.

*TUSIJISAHAU*

1475407481775.jpg


1475407508574.jpg


1475407532154.jpg


Kwa sasa akiwa saiti
 
Kutoka Urais Hadi Ombaomba Mtaani
TOPICS:AFRIKA.

DUNIANI tunajifunza na kuona vitu vingi tofauti vya kushangaza, kuogofya na kufurahisha. Wengi hawamjui Valentine Strasser ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi ya Sierra Leone kati ya Aprili 29, 1992 hadi Januari 16 , 1996 akiwa ndiye amiri jeshi mkuu na kiongozi wa ngazi ya juu kwenye taifa hilo lililopo kaskazini-magharibi mwa bara la Afrika.Wakati akiingia madarakani aliweka rekodi ya kuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi, yaani akiwa na chini ya miaka 25.

valentine-1Kapteni Valentine Strasser kiongozi wa mapinduzi ya Rais Saidu Momoh.

Aprili 29, 1992, Strasser akiwa kijana mwanajeshi mwenye cheo cha kapteni, akiwa na umri wa miaka 25, aliwaongoza wanajeshi wenzake kuvamia Ikulu ya Sierra Leone, walimkuta rais amejificha ndani ya kabati lililopo kwenye chumba cha kuogea, kisha wakamteka Rais Joseph Saidu Momoh na wakamlazimisha kukimbia, naye akatorokea Conakry, Guinea.

valentine-3Valentine Strasser baada ya mapinduzi kufanikiwa.

Strasser alichukua madaraka ya nchi hiyo siku tatu tangu ashehereke sikukuu yake ya kuzaliwa.

Baada ya Momoh kutorokea Conakry, Strasser alijitangaza kuwa Rais wa Sierra Leone. Aliwaongoza vijana wenzake sita waliofanikisha mapinduzi hayo na kuunda serikali ya mpito waliyoipa jina la National Provisional Ruling Council (NPRC).

Maisha yakabadilika, alishakuwa mkuu wa nchi, kwa hiyo hakutaka kuishi kwenye nyoyo za Wasierra Leone.

Hakulipa malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma.

Alifuja almasi ya Sierra Leone, kwa vile jina lake ni Valentine, basi sikukuu ya Valentine’s Day akaifanya kuwa sherehe ya kitaifa yenye mapumziko huku sherehe kubwa ikiandaliwa ikulu ya nchi hiyo.

Strasser alikuwa na mbwembwe nyingi, mwaka 1993 katika mkutano wa wakuu wa serikali katika nchi za Jumuiya ya Madola, uliofanyika Limassol, Cyprus, alitinga kwa mbwembwe akiwa amevaa suruali ya jeans na fulana yenye maandishi Sunny Days in Cyprus (Siku za Jua Kali Cyprus).

Alikuwa mtu wa starehe, vurugu nyingi kwa wanawake, aliua watu wasio na hatia.

Strasser alisahau kuwa ipo siku uongozi hautakuwa kwenye mikono yake, na ambacho kinaweza kumfaa ni kuishi ndani ya mioyo ya watu ili wamtetee na kumpigania baadaye. Januari 16, 1996, Strasser alipinduliwa na msaidizi wake, Brigedia Jenerali Julius Maada Bio.

Strasser akakimbilia Uingereza, akajiunga na Chuo Kikuu cha Warwick, kilichopo mjini Coventry, akaanza masomo ya sheria, akasema anataka awe wakili ili awatetee Waafrika.

Mwaka mmoja wa masomo, Strasser aliishiwa fedha, akaacha chuo.

Maisha Uingereza yakawa magumu, akakimbilia Gambia nako kukawa pagumu, mwisho akarudi Sierra Leone, mjini Grafton, mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Freetown.

Kazi ya kwanza ambayo Strasser aliifanya, ikawa kuanzisha kichuo kidogo cha kufundisha kompyuta na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama). Maisha ya chuo yakamshinda.

Baada ya kila kitu kwenda kombo, Strasser alirudi nyumbani kwa mama yake mzazi na kuishi kwenye banda la uani.

Hata sasa, akiwa na umri wa miaka 49, anakunywa pombe za kienyeji mtaani.

valentine-2Picha ya Valentine Strasser alivyo sasa.

Hana hadhi yoyote kama kiongozi mkuu wa nchi mstaafu. Strasser anaishi kama mtu wa kawaida tu mtaani. Mlevi na hakuna anayemjali.

Hana mtu wa kumtetea wala kumpigania kwa sababu hakuishi kwenye nyoyo za watu. Strasser ndiye mkuu wa nchi wa zamani, anayeishi kimaskini kuliko wakuu wote wa nchi duniani.

Ukiwa kiongozi na kugeuka kituko kama Strasser inawezekana kabisa.

Ishi vibaya na watu wasikupende, akija mtawala ambaye hatakutambua kama mkuu uliyepita, unaweza kuishi maisha ya hovyo kama ombaomba mtaani au kuwa mnywa gongo uliyeshindikana.

Vyema sasa viongozi wote duniani watambue kwamba uongozi ni dhamana, wafanye kazi kwa kujituma na wataishi mioyoni mwa wananchi waliowaongoza milele. Kuna viongozi wengi waliofanya mema na bado wanaenziwa mpaka sasa kama Julius Nyerere na Nelson Mandela, wako wengi hawa ni baadhi tu ya viongozi walioweka mbele maslahi ya wananchi wao na watakumbukwa milele.
1475445649130.jpg
1475445668393.jpg
 
Duh!!
Hatari sana!!
Vipi ndugu na jamaa za aliowaua bila hatia!? Wamemwacha aonje joto ya jiwe au wanamyatia walipize?
 
Kweli hana madhara tena duuuuuh ukiwa maskini kichwani hata ukipewa benki ya dunia hutoboi
 
Ebu ngoja akiamka atakuja ausome hii simulizi ya ukweli toka kwa kiongozi alie wahi kushika nafasi ya juu kabisa ya uongozi wa nchi.
Ila sina hakika kama atabadilika..[emoji69]
 
Hata hapa Tanzania kuna kiongozi mmoja "aliibaka" katiba mpya iliyokuwa inapendwa na waTanzania

Naskia huyo mzee Sasa yuko hoi kitandani.. roho inamtoka.. halafu inarudi... Kweli malipo ni hapa hapa duniani.
 
Ivi huyu mtu tumuweke kwenye kundi La Wasio na bahati au Kundi la Wazembe??
 
An Open Letter to President Ernest Koroma Please Rescue Capt. Valentine Strasser

Valentine Strasser....Was Not A Bad Guy

Posted by Donald Georgestone California

Dear Mr President

The deteriorating condition of a former Head of State of Sierra Leone
and a former military Officer , Capt . Valentine Strassar, who
went to the battle field to save the peaceful people of the
Republic of Sierra Leone is on the Internet, and it is seen all
over the world .

Mr President , the whole world is waiting and watching , to see
if your Government has respect for a former Head of State of the
country you are now governing , and a former Miltary Officer who
was shot on the line of duty .

Capt. Valentine Strasser was Head of State of Sierra Leone from
April 29 , 1992 through January 16 , 1996 . Prior to that period , he
was shot on the battle field by the ( RUF ) Revolutionary United
Front led by Foday Sankoh . That in itself , is heroism and
patriotism . Let us be true to ourselves .. How many Sierra
Leoneans today , are prepared to risk their lives for Sierra Leone ?
I bet my life , it is less than twenty percent .

Mr President, Capt. Valentine Strasser sacrificed his life by serving
in the army , He introduced the cleaning exercise in Freetown and
other parts of the country. If he had not taken over the governmemt
in 1992 , the country would have fallen into complete anarchy , because
when the soldiers came to the State House to report about the poor
conditions of the fighting force, the then President Momoh flee the country
and took refuge in Guinea . Moreover, Capt. Strasser had not been
found guilty of any crime , so these are some of the many reasons
why the Govenment should come to his rescue.

Mr President , it is un Sierra Leonean to see a former Head of State ,
and a former Military Officer perishing in another third world country ,
and we fail to come to his rescue. There are times, when citizens
of a country are judged , by the way the government of that country
treats its citizens who had made great contributions towards the
development of that country .

Mr President, if your government fails to rescue Capt. Valentine Strasser ,
then we are sending the wrong message to our men and women
in uniform .We are telling them , that we do not care about them , whether
they are shot or not , and once they leave the force they are on their own .
That is not good , it would affect the morals of our men and women in
uniform .So Mr. President , I am appealing to you Sir , to look into
Capt. Strasser’s case , and see what type of help could be rendered .
That way , we will be sending a positive message to our men and women
in uniform , that we appreciate their services and heroism . That would also
boost their morals .
Lastly Mr President , I know you are a Christian , and you have good
intentions for the people of Sierra Leone . We in the Diasporas are
praying for you , that God grant you the strength , wisdom and courage
to lead that nation on the right path , so that she can take her place
amongs the progressive nations of the world

Donald Georgestone
 
me naona afadhali yupo hai inawezekana mikono yake haikuwa na damu za watu.. tuwakumbuke pia watu kama samwel doe,charles taylor,foddei sanko, na wanamapinduzi wengi wa west africa,wako wapi..... wengi wameuwawa kinyama sana na wengine wako jela... bora mr. valentine yupo hai anagonga zake banana na viroba kwa raha zake,nafikiri na heshima ya upresident bado inamnukia watu hawawezi kumdharau kupita kiasi.. kwangu mie huyo ni rais mstaafu tu. wote tunafahamu ilivyokuwa kuwa kazi ngumu kuingia ikulu ukawa rais kwa njia yoyote ile,sio shughuli ya kitoto..
 
Back
Top Bottom