Mwisho mbaya wa aliyekuwa Rais wa Sierra, Leone Valentine Esegragbo Melvine Strasser

Kile apandacho mtu, ndicho atakachovuna........pia malipo huwa ni hapa hapa duniani.
 
Kutoka Urais Hadi Ombaomba Mtaani

DUNIANI tunajifunza na kuona vitu vingi tofauti vya kushangaza, kuogofya na kufurahisha. Wengi hawamjui Valentine Strasser ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi ya Sierra Leone kati ya Aprili 29, 1992 hadi Januari 16 , 1996 akiwa ndiye amiri jeshi mkuu na kiongozi wa ngazi ya juu kwenye taifa hilo lililopo kaskazini-magharibi mwa bara la Afrika.Wakati akiingia madarakani aliweka rekodi ya kuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi, yaani akiwa na chini ya miaka 25.Kapteni Valentine Strasser kiongozi wa mapinduzi ya Rais Saidu Momoh.

Aprili 29, 1992, Strasser akiwa kijana mwanajeshi mwenye cheo cha kapteni, akiwa na umri wa miaka 25, aliwaongoza wanajeshi wenzake kuvamia Ikulu ya Sierra Leone, walimkuta rais amejificha ndani ya kabati lililopo kwenye chumba cha kuogea, kisha wakamteka Rais Joseph Saidu Momoh na wakamlazimisha kukimbia, naye akatorokea Conakry, Guinea.

Valentine Strasser baada ya mapinduzi kufanikiwa.

Strasser alichukua madaraka ya nchi hiyo siku tatu tangu ashehereke sikukuu yake ya kuzaliwa.

Baada ya Momoh kutorokea Conakry, Strasser alijitangaza kuwa Rais wa Sierra Leone. Aliwaongoza vijana wenzake sita waliofanikisha mapinduzi hayo na kuunda serikali ya mpito waliyoipa jina la National Provisional Ruling Council (NPRC).

Maisha yakabadilika, alishakuwa mkuu wa nchi, kwa hiyo hakutaka kuishi kwenye nyoyo za Wasierra Leone.

Hakulipa malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma. Alifuja almasi ya Sierra Leone, kwa vile jina lake ni Valentine, basi sikukuu ya Valentine’s Day akaifanya kuwa sherehe ya kitaifa yenye mapumziko huku sherehe kubwa ikiandaliwa ikulu ya nchi hiyo.

Strasser alikuwa na mbwembwe nyingi, mwaka 1993 katika mkutano wa wakuu wa serikali katika nchi za Jumuiya ya Madola, uliofanyika Limassol, Cyprus, alitinga kwa mbwembwe akiwa amevaa suruali ya jeans na fulana yenye maandishi Sunny Days in Cyprus (Siku za Jua Kali Cyprus).

Alikuwa mtu wa starehe, vurugu nyingi kwa wanawake, aliua watu wasio na hatia. Strasser alisahau kuwa ipo siku uongozi hautakuwa kwenye mikono yake, na ambacho kinaweza kumfaa ni kuishi ndani ya mioyo ya watu ili wamtetee na kumpigania baadaye. Januari 16, 1996, Strasser alipinduliwa na msaidizi wake, Brigedia Jenerali Julius Maada Bio.

Strasser akakimbilia Uingereza, akajiunga na Chuo Kikuu cha Warwick, kilichopo mjini Coventry, akaanza masomo ya sheria, akasema anataka awe wakili ili awatetee Waafrika.

Mwaka mmoja wa masomo, Strasser aliishiwa fedha, akaacha chuo.

Maisha Uingereza yakawa magumu, akakimbilia Gambia nako kukawa pagumu, mwisho akarudi Sierra Leone, mjini Grafton, mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Freetown.

Kazi ya kwanza ambayo Strasser aliifanya, ikawa kuanzisha kichuo kidogo cha kufundisha kompyuta na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama). Maisha ya chuo yakamshinda.

Baada ya kila kitu kwenda kombo, Strasser alirudi nyumbani kwa mama yake mzazi na kuishi kwenye banda la uani.
Hata sasa, akiwa na umri wa miaka 49, anakunywa pombe za kienyeji mtaani.
Picha ya Valentine Strasser alivyo sasa.

Hana hadhi yoyote kama kiongozi mkuu wa nchi mstaafu. Strasser anaishi kama mtu wa kawaida tu mtaani. Mlevi na hakuna anayemjali.
Hana mtu wa kumtetea wala kumpigania kwa sababu hakuishi kwenye nyoyo za watu. Strasser ndiye mkuu wa nchi wa zamani, anayeishi kimaskini kuliko wakuu wote wa nchi duniani.

Ukiwa kiongozi na kugeuka kituko kama Strasser inawezekana kabisa.
Ishi vibaya na watu wasikupende, akija mtawala ambaye hatakutambua kama mkuu uliyepita, unaweza kuishi maisha ya hovyo kama ombaomba mtaani au kuwa mnywa gongo uliyeshindikana.

Vyema sasa viongozi wote duniani watambue kwamba uongozi ni dhamana, wafanye kazi kwa kujituma na wataishi mioyoni mwa wananchi waliowaongoza milele.

Kuna viongozi wengi waliofanya mema na bado wanaenziwa mpaka sasa kama Julius Nyerere na Nelson Mandela, wako wengi hawa ni baadhi tu ya viongozi walioweka mbele maslahi ya wananchi wao na watakumbukwa milele.

TMPDOODLE1486489537064.jpg
TMPDOODLE1486489556660.jpg
TMPDOODLE1486489574424.jpg
 
Mjue KAMANDA Valentine Strasser
16508570_1352762134784689_5366851275669159603_n.jpg
16473858_1352762318118004_2519237605425363064_n.jpg

Kutoka Urais hadi Ombaomba Mtaani.

DUNIANI tunajifunza na kuona vitu vingi tofauti vya kushangaza, kuogofya na kufurahisha. Wengi hawamjui Valentine Strasser ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi ya Sierra Leone kati ya Aprili 29, 1992 hadi Januari 16 , 1996 akiwa ndiye amiri jeshi mkuu na kiongozi wa ngazi ya juu kwenye taifa hilo lililopo kaskazini-magharibi mwa bara la Afrika.Wakati akiingia madarakani aliweka rekodi ya kuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi, yaani akiwa na chini ya miaka 25.Kapteni Valentine Strasser kiongozi wa mapinduzi ya Rais Saidu Momoh.

16472988_1352762321451337_4678951951790676414_n.jpg

Aprili 29, 1992, Strasser akiwa kijana mwanajeshi mwenye cheo cha kapteni, akiwa na umri wa miaka 25, aliwaongoza wanajeshi wenzake kuvamia Ikulu ya Sierra Leone, walimkuta rais amejificha ndani ya kabati lililopo kwenye chumba cha kuogea, kisha wakamteka Rais Joseph Saidu Momoh na wakamlazimisha kukimbia, naye akatorokea Conakry, Guinea.
Valentine Strasser baada ya mapinduzi kufanikiwa.
Strasser alichukua madaraka ya nchi hiyo siku tatu tangu ashehereke sikukuu yake ya kuzaliwa.
Baada ya Momoh kutorokea Conakry, Strasser alijitangaza kuwa Rais wa Sierra Leone. Aliwaongoza vijana wenzake sita waliofanikisha mapinduzi hayo na kuunda serikali ya mpito waliyoipa jina la National Provisional Ruling Council (NPRC).

Maisha yakabadilika, alishakuwa mkuu wa nchi, kwa hiyo hakutaka kuishi kwenye nyoyo za Wasierra Leone.
Hakulipa malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma.
Alifuja almasi ya Sierra Leone, kwa vile jina lake ni Valentine, basi sikukuu ya Valentine’s Day akaifanya kuwa sherehe ya kitaifa yenye mapumziko huku sherehe kubwa ikiandaliwa ikulu ya nchi hiyo.

Strasser alikuwa na mbwembwe nyingi, mwaka 1993 katika mkutano wa wakuu wa serikali katika nchi za Jumuiya ya Madola, uliofanyika Limassol, Cyprus, alitinga kwa mbwembwe akiwa amevaa suruali ya jeans na fulana yenye maandishi Sunny Days in Cyprus (Siku za Jua Kali Cyprus).
Alikuwa mtu wa starehe, vurugu nyingi kwa wanawake, aliua watu wasio na hatia.
Strasser alisahau kuwa ipo siku uongozi hautakuwa kwenye mikono yake, na ambacho kinaweza kumfaa ni kuishi ndani ya mioyo ya watu ili wamtetee na kumpigania baadaye. Januari 16, 1996, Strasser alipinduliwa na msaidizi wake, Brigedia Jenerali Julius Maada Bio.
Strasser akakimbilia Uingereza, akajiunga na Chuo Kikuu cha Warwick, kilichopo mjini Coventry, akaanza masomo ya sheria, akasema anataka awe wakili ili awatetee Waafrika.
Mwaka mmoja wa masomo, Strasser aliishiwa fedha, akaacha chuo.
Maisha Uingereza yakawa magumu, akakimbilia Gambia nako kukawa pagumu, mwisho akarudi Sierra Leone, mjini Grafton, mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Freetown. Kazi ya kwanza ambayo Strasser aliifanya, ikawa kuanzisha kichuo kidogo cha kufundisha kompyuta na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama). Maisha ya chuo yakamshinda.
Baada ya kila kitu kwenda kombo, Strasser alirudi nyumbani kwa mama yake mzazi na kuishi kwenye banda la uani. Hata sasa, akiwa na umri wa miaka 49, anakunywa pombe za kienyeji mtaani.
16427784_1352762098118026_5484645359166690860_n.jpg
16508064_1352762341451335_89008465670560256_n.jpg

Picha ya Valentine Strasser alivyo sasa.
Hana hadhi yoyote kama kiongozi mkuu wa nchi mstaafu. Strasser anaishi kama mtu wa kawaida tu mtaani. Mlevi na hakuna anayemjali.

Hana mtu wa kumtetea wala kumpigania kwa sababu hakuishi kwenye nyoyo za watu. Strasser ndiye mkuu wa nchi wa zamani, anayeishi kimaskini kuliko wakuu wote wa nchi duniani.
Ukiwa kiongozi na kugeuka kituko kama Strasser inawezekana kabisa.
Ishi vibaya na watu wasikupende, akija mtawala ambaye hatakutambua kama mkuu uliyepita, unaweza kuishi maisha ya hovyo kama ombaomba mtaani au kuwa mnywa gongo uliyeshindikana.

Vyema sasa viongozi wote duniani watambue kwamba uongozi ni dhamana, wafanye kazi kwa kujituma na wataishi mioyoni mwa wananchi waliowaongoza milele. Kuna viongozi wengi waliofanya mema na bado wanaenziwa mpaka sasa kama Julius Nyerere na Nelson Mandela, wako wengi hawa ni baadhi tu ya viongozi walioweka mbele maslahi ya wananchi wao na watakumbukwa milele.

Source; Hamis Hamad Hamis facebook page.
Hamis Hamad Hamis | Facebook
 
Mkuu asante kwa kututoa tongo tongo. Kwakweli kwa kupitia hyo jamaa tuna mengi ya kujifunza kama binadamu.
 
Labda pengine yeye anaridhika na hayo maisha maybe maisha mazur anaona kayala vyakutosha since 25 years to now
 
Huo ndio uanaume!! Sio eti mtu anafukuzwa tu kazi anaamua kujiua!!! Kana kwamba ndio mwisho wa maisha!! Huyu jamaa hata kia fya yuko vizuri kwani kwa maisha hayo magonjwa kama BP, na wenzake wale kama kiharusi wasingemuacha kamwe!! HONGERA KAMANDA
 
Kutoka Urais hadi Ombaomba wa Mtaani.

Duniani tunajifunza na kuona vitu vingi tofauti vya kushangaza, kuogofya na kufurahisha,
Wengi wetu hatumjui Valentine Strasser ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi ya Sierra Leone kati ya Aprili 29, 1992 hadi Januari 16 , 1996 akiwa ndiye amiri jeshi mkuu na kiongozi wa ngazi ya juu kwenye taifa hilo lililopo kaskazini-magharibi mwa bara la Afrika.

Wakati akiingia madarakani aliweka rekodi ya kuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi, yaani akiwa na chini ya miaka 25.Kapteni Valentine Strasser kiongozi wa mapinduzi ya Rais Saidu Momoh.

ILIKUWAJE KUWAJE MAPAKA AKAWA RAIS MDOGO ZAIDI DUNIANI KWA WAKATI HUO?

Aprili 29, 1992, Strasser akiwa mwanajeshi kijana mwenye cheo cha kapteni, akiwa na umri wa miaka 25 tu, aliwaongoza wanajeshi wenzake kuvamia Ikulu ya Sierra Leone, walimkuta raisJoseph Saidu Momoh amejificha ndani ya kabati lililopo kwenye chumba cha kuogea, kisha wakamteka na wakamlazimisha kukimbia, naye akatorokea jijini Conakry nchini Guinea.
Baada ya mapinduzi kufanikiwa rais
Strasser alichukua madaraka ya nchi hiyo siku tatu tangu ashehereke sikukuu yake ya kuzaliwa na baada ya kuthibitika kwamba aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Momoh kutorokea Conakry, mwanajeshi Strasser alijitangaza kuwa rais wa Sierra Leone. Aliwaongoza vijana wenzake sita waliofanikisha mapinduzi hayo na kuunda serikali ya mpito waliyoipa jina la National Provisional Ruling Council (NPRC).

KAMA KAWAIDA MADARAKA YANALEVYA

Baada ya kuwa rais kamili,maisha yakabadilika kwakuwa tu ashakuwa mkuu wa nchi, kwa hiyo hakutaka kuishi kwenye nyoyo za wananchi wake Sierra Leone,Hakukumbuka tena kulipa malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma,alifuja almasi ya Sierra Leone na rasilimali zingine na kupelekea kuchukiwa na wananchi na wanajeshi wenzake kwa mda mfupi,

Maajabu mengine ya bwana huyu

kwa vile jina lake ni Valentine, basi sikukuu ya Valentine’s Day ambayo dunia yote huazimisha kila ifikapo tarehe 14 ya mwezi 2,akaifanya kuwa sherehe hiyo kuwa miongoni mwa sherehe za kitaifa yenye mapumziko huku sherehe kubwa ikiandaliwa ikulu ya nchi hiyo na kula bata sana.

Bwana huyu alikuwa bingwa wa mbwembwe na starehe

Rais Strasser alikuwa mtu wa mbwembwe nyingi na kupenda sifa na kusifiwa,kwa mfano mwaka 1993 katika mkutano wa wakuu wa serikali katika nchi za Jumuiya ya Madola, uliofanyika Limassol nchini Cyprus, alitinga kwa mbwembwe akiwa amevaa suruali ya jeans na fulana yenye maandishi Sunny Days in Cyprus (Siku za Jua Kali Cyprus) ,kitu kilichokuwa kama dharau kwa waCyprus,alikuwa mtu wa starehe sana,mbabe, vurugu nyingi,na mpenda wanawake (womenizer),pia kipindi cha utawala wake aliua watu wasio na hatia,na hasa wapinzani wake.

Rais Strasser alisahau na kujisahau kuwa ipo siku uongozi hautakuwa kwenye mikono yake, na ambacho kinaweza kumfaa ni kuishi ndani ya mioyo ya watu ili wamtetee na kumpigania baadaye.

Waswahili wanasema ukiuwa kwa upanga nawe utakufa kwa upanga na malipo ni hapahapa duniani,ilikuwa ni january 16, 1996, rais Strasser naye alipinduliwa na msaidizi wake, Brigedia Jenerali Julius Maada Bio,

Baada ya kupinduliwa,ilibidi bwana Strasser akimbilie nchini Uingereza, ambapo akiwa huko akajiunga na Chuo Kikuu cha Warwick, kilichopo mjini Coventry, akaanza kusomea masomo ya sheria,huku akijinasibu kutaka kuwa wakili na kuja kuwatetea waafrika alioshindwa kuwatetea akiwa madarakani kama rais,

Baada ya mwaka mmoja wa masomo, Strasser aliishiwa fedha na kumbidi kuacha chuo,na kuingia mtaani nchini uingereza,
Maisha ya Uingereza yakawa magumu kwake na kuamua kukimbilia nchini Gambia,ambapo inadaiwa nako kukawa pagumu, mwishowe akaamua kurudi nchini mwake alipozaliwa yaani Sierra Leone mjini Grafton, mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo Freetown.

Kazi ya kwanza ambayo Strasser aliifanya ni kuanzisha chuo kidogo cha kufundisha kompyuta na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama),ambapo napo laana ya na dhambi ya kuwanyanyasa raia wakati akiwa rais ikazidi kumwandama na hatimaye maisha ya kuendesha chuo chake yakamshinda pia na baada ya kila kitu kwenda kombo, Strasser alirudi nyumbani kwa mama yake mzazi na kuishi kwenye banda la uani,ambapo mpaka sasa, akiwa na umri wa miaka 49 bado anaishi hapo bila kazi na kunywa pombe za kienyeji mtaani huku akiishi kwa kuombaomba bila kujali kama alishawahi kuwa rais wa taifa kubwa na tajiri kama Sierra Leone.

Naamini kila mmoja wetu aliesoma andiko hili atapata cha kujifunza.
source :C&P 4m JF
 
Maisha Sijui yakoje.ila jamaa kazeeka kwa mawazo miaka 42 tu keshafubaah.
 
Back
Top Bottom