Mwisho mbaya wa aliyekuwa Rais wa Sierra, Leone Valentine Esegragbo Melvine Strasser

Mwisho mbaya wa aliyekuwa Rais wa Sierra, Leone Valentine Esegragbo Melvine Strasser

*Enzi zake hakushikika kwa anasa za kila aina
*Aishiwa, sasa ni 'kula kulala’ kwa mama yake


SIKU tatu baada ya kutimiza umri wa miaka 25 ya kuzaliwa, Valentine Strasser aliweka rekodi ya kuwa Rais mwenye umri mdogo kabisa duniani.

wpid-captain-valentine-strasser-27-leader-of-the-provisional-ruling-council-b3r27y.jpg

Valentine Strasser

Aprili 29, 1992, Strasser akiwa kijana mwanajeshi mwenye cheo cha kapteni, aliwaongoza wenzake kuvamia Ikulu ya Sierra Leone ambako walimkuta Rais Joseph Saidu Momoh akiwa amejificha ndani ya kabati lililopo bafuni, wakamteka na kumlazimisha kuikimbia nchi yake, naye bila kubisha akachukua helikopta na kutorokea Conakry, Guinea.

Na baada ya Momoh kutorokea Conakry, Strasser alijitangaza kuwa Rais wa Sierra Leone. Aliwaongoza vijana wenzake sita waliofanikisha mapinduzi hayo na kuunda Serikali ya mpito waliyoipa jina la National Provisional Ruling Council (NPRC).

valentine-strasser.jpg

Valentine Strasser wakati wa utawala wake

Maisha yakabadilika. Alishakuwa mkuu wa nchi. Na tofauti na matarajio ya wengine, akajikuta akizama kwenye starehe na anasa, kamwe hakuwakumbuka tena raia wake wa Sierra Leone.

Hakuangalia tena miradi ya maendeleo, lakini aliwakwaza wengi zaidi kwa kushindwa kulipa malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma.

Akiwa madarakani alifuja almasi ya Sierra Leone. Rais kijana hakuambiwa kitu, ilikuwa yeye na starehe, starehe na yeye. Hata siku ya Wapendanao `Valentine’s Day’, yaani Februari 14 ya kila mwaka, yeye aliigeuza siku ya mapumziko ya kitaifa, kwa kuwa naye anaitwa Valentine.

Pamoja na mapumziko, siku hiyo ilikuwa na chereko za kila aina, huku ikulu ikiwa na sherehe za kukata na shoka. Alikuwa na mbwembwe nyingi mno, aliyepapatikia wanawake na wakati mwingine kuua hovyo wabaya wake.

Inaelezwa hata siku ya kuzaliwa kwa Mfalme wa muziki katika miondoko ya Reggae duniani, Bob Marley (Robert Nesta Marley), pia aliifanya siku ya mapumziko kitaifa, kutokana na kumhusudu nguli huyo wa muziki aliyeaga dunia Mei 11 mwaka 1981. Alizaliwa Februari 6, mwaka 1945.

Kwa ujumla alishaonekana kujisahau na kujiona pengine angeishika nafasi hiyo milele. Watu wake waliendelea kunung’unika, huku yeye akiponda raha ndani na nje ya bara la Afrika. Hata hivyo, ilipofika Januari 16, 1996, Strasser alipinduliwa madarakani na msaidizi wake, Brigedia Jenerali Julius Maada Bio.

Strasser akakimbilia London, Uingereza ambako aliamua kuingia darasani katika Chuo Kikuu cha Warwick, kilichopo mjini Coventry ambako alianza kusomea Sheria, akisema kiu yake ni kuwa wakili ili aweze kuwatetea Waafrika.

Hata hivyo, ndoto yake iliishia njiani, kwani baada ya mwaka mmoja wa masomo, Strasser alitetereka kiuchumi, alishindwa kulipa ada na kulazimika kuacha chuo. Inaelezwa alishindwa pia kulipa pango la nyumba katika eneo alilokuwa anaishia huko Islington huko Kaskazini mwa London, Uingereza.

Maisha yakawa magumu zaidi, akajikuta akilazimika kuikimbia Ulaya na kurejea Afrika mwaka 1999, akiweka makazi katika mji wa Banjul, Gambia ambako hata hivyo mambo yalimbana mno, akashindwa kulipia hata vibali vya kuishi nchini humo. Wakati fulani inadaiwa alilazimika kuishi mtaani na kuombaomba, lakini aliposhitukiwa, alitimuliwa ikielezwa pengine alikuwa anapanga kushirikiana na askari wa nchi hiyo kufanya mapinduzi.

Serikali ya Gambia iliamua kumsafirisha kurudi Uingereza mwaka 2000, lakini alikataliwa kuingia nchini humo, hivyo kulazimika kurejea Sierra Leone, hadi mjini Grafton, Mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Freetown.

Akiwa huko, kwa kuwa hakuwa na fedha wala biashara ya kuisimamia, aliamua kuanzisha chuo kidogo cha kufundishia kompyuta na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama). Hata hivyo, kutokana na mazingira ya chuo hicho, nacho kikamshinda. Kwa muda mrefu buibui na tandabui ndivyo vilivyoshamiri.

valentine-strasser.jpg

Valentine Strasser akiwa na wanafunzi wake wa computer

Na kutokana na kila kitu kwenda kombo, inaelezwa Strasser mwenye umri wa miaka 50 sasa, aliamua kurudi nyumbani kwa mama yake mzazi aitwaye Beatrice anakolelewa tena, kwa chakula na malazi.

strasser.jpg

Hapa ndipo anapoishi Valentine Strasser kwa sasa

wpid-img-20150706-wa0014.jpg

Valentine Strasser alivyo kwa sasa, akiwa nyumbani kwa mama yake


Maisha yake kwa sasa ni pombe, yeye na pombe. Halewi pombe za gharama, bali za kienyeji ikiwa ni pamoja na pombe ya mnazi. Baa anazokunywa hazina chembe ya hadhi ya mtu aliyewahi kushika madaraka makubwa katika nchi.

Ni mtu wa kawaida mno kijijini kwao, anachukuliwa kama mlevi tu. Hakuna anayeshituka kumuona, zaidi ya kumkwepa pengine kwa kuhofia kuombwa fedha.

Pulse-Valentine-Strasser-.jpg

Valentine Strasser akiwa kwenye kilabu cha mataputapu

sub-buzz-14717-1475183239-3.jpg



wpid-fb_img_1436141577834.jpg

Amelia Rogers mke aliyemkimbia Valentine Strasser baada ya maisha kuwa magumu

Maisha ya Strasser ni magumu mno, na inaelezwa alikimbiwa pia na mkewe Amelia. Kwa sasa Strasser hana marafiki wa uhakika, zaidi ya wamiliki wa baa. Anapuuzwa na kila mtu wakisema kwa kuwa hakuwajali wakati akiwa Rais, basi hastahili heshima yoyote kwa sasa.

Pengine huyo ndiye mkuu wa nchi wa zamani anayeishi maisha duni zaidi kuliko wote duniani. Kipato kikubwa cha Strasser katika miaka ya hivi karibuni ni fedha kiasi cha dola za Kimarekani 2,000 (Sh milioni 4.2) alicholipwa kama kiinua mgongo chake jeshini.

Alipoulizwa hivi karibuni kama ana mpango wa kurudi katika siasa, alikana akisema hana muda huo.

Anatamani kurudi jeshini? “Hapana, sihitaji tena kusikia habari hizo”. Ni kauli ya Strasser akiwa katika baa ya John’s akiwa na rafiki yake na msiri wake mkubwa aitwaye Daniel.

Strasser hataki kukumbuka mengi ya nchi yake, lakini anasema hatasahau mafanikio ya timu ya soka ya taifa ya Sierra Leone katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) enzi za utawala wake. Angalau ilifika raundi ya kwanza mwaka 1994 na 1996.

Kwa hisani ya HabariLeo la leo Jumapili
 

Attachments

  • Valentine-Strasser.jpg
    Valentine-Strasser.jpg
    41.9 KB · Views: 106
Haya ndiyo yatakayomkuta Bashite. Kwa kung'ang'aniaa Ukuu wa Mkoa mpaka leo badala ya kujiuzuru, ameudhihirishia ulimwengu kuwa ni kijana mpumbavu sana. Ngoja atimuliwe ajiunge kunywa mataputapu mitaani.
 
Kama aliuwa alozania wabaya wake sasa anatafuta nini uraiani. Sheria ichukue mkondo wake.
 
Haya ndiyo yatakayomkuta Bashite. Kwa kung'ang'aniaa Ukuu wa Mkoa mpaka leo badala ya kujiuzuru, ameudhihirishia ulimwengu kuwa ni kijana mpumbavu sana. Ngoja atimuliwe ajiunge kunywa mataputapu mitaani.

Hmm! Huyu Bashite ni kiongozi wa nchi gani?...
 
Mafao pekee aliyostahili kiongozi huyu ni kupelekwa ICC na kufungwa maisha. Nashangaa sijui kwanini wamemuacha kunywa mataputapu uraiani!...
Apelekwe ICC kwa sababu anakunywa mataputapu...
ICC hawapokeagi kesi za kijinga namna hio..
Kesi gani hata mahaka za huko kwao ukifungua kesi kwa mtu aliejichokea kama huyu.. watasonya na kuitupilia mbali.

Hapo halipo hata hafai kwenda jela.. maisha yake ni jela tosha
 
Ana bahati kuwa hai, wengine wakirudi wanauliwa, ila duh! Kachoka sana, hadi kukimbiwa na wauza pombe!
 
Apelekwe ICC kwa sababu anakunywa mataputapu...
ICC hawapokeagi kesi za kijinga namna hio..
Kesi gani hata mahaka za huko kwao ukifungua kesi kwa mtu aliejichokea kama huyu.. watasonya na kuitupilia mbali.

Hapo halipo hata hafai kwenda jela.. maisha yake ni jela tosha

ICC kwa kunywa mataputapu?!
Nilimaanisha apelekwe ICC kwa kuwa alifanya mauaji enzi za utawala wake na kuitia nchi katika hasara kubwa.
Hata hivyo, umemalizia vizuri, kwamba "maisha yake ni jela tosha"...
 
KUTOKA KUWA RAIS MPAKA KUWA MLALA HOI MTAANI.
____________________________________________
Kutana na Kapteni Valentine Strasser,Alikuwa Rais wa Nchi na Sasa Ni Ombaomba Mkubwa...!!! Duniani tunajifunza na kuona vitu vingi tofauti vya kushangaza, kuogofya na kufurahisha,
Wengi wetu hatumjui Valentine Strasser ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi ya Sierra Leone kati ya Aprili 29, 1992 hadi Januari 16 , 1996 akiwa ndiye amiri jeshi mkuu na kiongozi wa ngazi ya juu kwenye taifa hilo lililopo kaskazini-magharibi mwa bara la Afrika.

Wakati akiingia madarakani aliweka rekodi ya kuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi, yaani akiwa na chini ya miaka 25.Kapteni Valentine Strasser kiongozi wa mapinduzi ya Rais Saidu Momoh.

ILIKUWAJE KUWAJE MAPAKA AKAWA RAIS MDOGO ZAIDI DUNIANI KWA WAKATI HUO?

Aprili 29, 1992, Strasser akiwa mwanajeshi kijana mwenye cheo cha kapteni, akiwa na umri wa miaka 25 tu, aliwaongoza wanajeshi wenzake kuvamia Ikulu ya Sierra Leone, walimkuta raisJoseph Saidu Momoh amejificha ndani ya kabati lililopo kwenye chumba cha kuogea, kisha wakamteka na wakamlazimisha kukimbia, naye akatorokea jijini Conakry nchini Guinea.

Baada ya mapinduzi kufanikiwa rais
Strasser alichukua madaraka ya nchi hiyo siku tatu tangu ashehereke sikukuu yake ya kuzaliwa na baada ya kuthibitika kwamba aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Momoh kutorokea Conakry, mwanajeshi Strasser alijitangaza kuwa rais wa Sierra Leone. Aliwaongoza vijana wenzake sita waliofanikisha mapinduzi hayo na kuunda serikali ya mpito waliyoipa jina la National Provisional Ruling Council (NPRC).

KAMA KAWAIDA MADARAKA YANALEVYA

Baada ya kuwa rais kamili,maisha yakabadilika kwakuwa tu ashakuwa mkuu wa nchi, kwa hiyo hakutaka kuishi kwenye nyoyo za wananchi wake Sierra Leone,Hakukumbuka tena kulipa malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma,alifuja almasi ya Sierra Leone na rasilimali zingine na kupelekea kuchukiwa na wananchi na wanajeshi wenzake kwa mda mfupi,

Maajabu mengine ya bwana huyu

kwa vile jina lake ni Valentine, basi sikukuu ya Valentine’s Day ambayo dunia yote huazimisha kila ifikapo tarehe 14 ya mwezi 2,akaifanya kuwa sherehe hiyo kuwa miongoni mwa sherehe za kitaifa yenye mapumziko huku sherehe kubwa ikiandaliwa ikulu ya nchi hiyo na kula bata sana.

Bwana huyu alikuwa bingwa wa mbwembwe na starehe

Rais Strasser alikuwa mtu wa mbwembwe nyingi na kupenda sifa na kusifiwa,kwa mfano mwaka 1993 katika mkutano wa wakuu wa serikali katika nchi za Jumuiya ya Madola, uliofanyika Limassol nchini Cyprus, alitinga kwa mbwembwe akiwa amevaa suruali ya jeans na fulana yenye maandishi Sunny Days in Cyprus (Siku za Jua Kali Cyprus) ,kitu kilichokuwa kama dharau kwa waCyprus,alikuwa mtu wa starehe sana,mbabe, vurugu nyingi,na mpenda wanawake (womenizer),pia kipindi cha utawala wake aliua watu wasio na hatia,na hasa wapinzani wake.

Rais Strasser alisahau na kujisahau kuwa ipo siku uongozi hautakuwa kwenye mikono yake, na ambacho kinaweza kumfaa ni kuishi ndani ya mioyo ya watu ili wamtetee na kumpigania baadaye.

Waswahili wanasema ukiuwa kwa upanga nawe utakufa kwa upanga na malipo ni hapahapa duniani,ilikuwa ni january 16, 1996, rais Strasser naye alipinduliwa na msaidizi wake, Brigedia Jenerali Julius Maada Bio

Baada ya kupinduliwa,ilibidi bwana Strasser akimbilie nchini Uingereza, ambapo akiwa huko akajiunga na Chuo Kikuu cha Warwick, kilichopo mjini Coventry, akaanza kusomea masomo ya sheria,huku akijinasibu kutaka kuwa wakili na kuja kuwatetea waafrika alioshindwa kuwatetea akiwa madarakani kama rais,

Baada ya mwaka mmoja wa masomo, Strasser aliishiwa fedha na kumbidi kuacha chuo,na kuingia mtaani nchini uingereza

Maisha ya Uingereza yakawa magumu kwake na kuamua kukimbilia nchini Gambia,ambapo inadaiwa nako kukawa pagumu, mwishowe akaamua kurudi nchini mwake alipozaliwa yaani Sierra Leone mjini Grafton, mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo Freetown.

Kazi ya kwanza ambayo Strasser aliifanya ni kuanzisha chuo kidogo cha kufundisha kompyuta na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama),ambapo napo laana ya na dhambi ya kuwanyanyasa raia wakati akiwa rais ikazidi kumwandama na hatimaye maisha ya kuendesha chuo chake yakamshinda pia na baada ya kila kitu kwenda kombo, Strasser alirudi nyumbani kwa mama y
41eedc42a9b1cdad482f69acddf831b1.jpg
ake mzazi na kuishi kwenye banda la uani,ambapo mpaka sasa, akiwa na umri wa miaka 49 bado anaishi hapo bila kazi na kunywa pombe za kienyeji mtaani huku akiishi kwa kuombaomba bila kujali kama alishawahi kuwa rais wa taifa kubwa na tajiri kama Sierra Leone.
 
Kawaida Maisha Tu Ghadafi Kutoka Rais Anayeogopwa Na Wananchi Ila Muda Ulipofika Aliwakimbia Wananchi Wake Kwa Kuwaogopa
 
Back
Top Bottom