Mwita Waitara afikishwa mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM mkoa wa Mara

Mwita Waitara afikishwa mbele ya Kamati ya Maadili ya CCM mkoa wa Mara

Walidhani Magu anawapenda kumbe aliwapenda kisa wako CHADEMA, sasa thamani yao haipo na wengi wao watatoswa kwenye upitishaji majina ya wagombea wa CCM
 
Mwita Waitara akiendelea na tabia yake, kamati ya nidhamu CCM Taifa inaweza mpa onyo kali sana.
 
Yuda eacarioti akifukuzwa atajiua, maescarioti kujiua ni kawaida
 
Hapa ndipo chama letu linapocheza kwa akili.

Huyu jamaa ameshajaa mazima na mwenyekiti hana lawama. Atamwambia wewe bwana ulikosea step.

Jambo linaishia hapo,ataambiwa asubiri kwenye teuzi nyingine,huko nako itapita.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafadhali wamkanye kuhusu kuunga mkono hadharani ukiukwaji wa sheria. Ukeketaji ni kosa la jinai, aache kuwahimiza wananchi waendelee na ukeketaji.
 
Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za serikali za mitaa (TAMISEMI) Mhe.Mwita Waitara amefika mbele ya kamati ya Maadili ya chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa Mara kuitikia wito wa Mwenyekiti wa Chama hicho mkoa wa Mara Samweli Kiboye kujibu tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Zikiwemo za kuanza kampeni za Ubunge nje ya taratibu za Chama na kumdhihaki Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mara mbele ya Vyombo vya habari.
Mtaka yote kwa pupa hukosa yote!
 
wakuu andiko hili nimelitoa kweny page ya Thadei Ole Mushi.

RASMI VITA YA WAHAMIAJI NDANI YA CCM NA WAFIA CHAMA IMEANZA

Na Thadei Ole Mushi.

Leo Tarehe 25/7/2020 Mwita Waitara kaitwa kwenye KAMATI ya MAADILI ya Mkoa huko Mara kwa kosa la kuanza kampeni kabla ya muda. Vita niliyoitabiri itakuwa imeaanza rasmi Kati ya Wana CCM asilia na Wahamiaji, Kati ya wanaccm waliotafuta kura 8,882,935 sawa na asilimia 58 za Rais Magufuli kuingia Ikulu na waliotafuta Kura za Lowassa. Hii ndio Vita kubwa kuliko zote kwa CCM kuelekea 2020.

Je chama kitawapa Wahamiaji nafasi na kuacha watoto wake waliopigana usiku na mchana na matusi yote walihotukanwa? Nakumbuka 2015 ulikuwa ukivaa sare ya CCM unatukanwa unazomewa unadhalilishwa vya kutosha lakini Kuna watu walijitoa Sana, wakakubali kutukanwa, kuzomewa, wakakubali kudhalilishwa ili Mgombea wetu aingie Ikulu.
Nitoe Wito kwa Wana CCM wote waliopigana usiku na mchana 2015 kuungana katika Vita hii. Dr Bashiru aliwaita wahamiaji kuwa Ni vifaru Sasa tuwaonyeshe kwa vitendo kuwa tuna utimamu wa akili kuliko wahamiaji. Tukatae dharau, tukatae kutukanwa, tukatae udhakikishaji huu.
Watakula walikopeleka Mboga 2015.
Nimekaa pembeni hapa nawachora tu wahamiaji hahahah mtajuta.....
 
Back
Top Bottom