wakuu andiko hili nimelitoa kweny page ya Thadei Ole Mushi.
RASMI VITA YA WAHAMIAJI NDANI YA CCM NA WAFIA CHAMA IMEANZA
Na Thadei Ole Mushi.
Leo Tarehe 25/7/2020 Mwita Waitara kaitwa kwenye KAMATI ya MAADILI ya Mkoa huko Mara kwa kosa la kuanza kampeni kabla ya muda. Vita niliyoitabiri itakuwa imeaanza rasmi Kati ya Wana CCM asilia na Wahamiaji, Kati ya wanaccm waliotafuta kura 8,882,935 sawa na asilimia 58 za Rais Magufuli kuingia Ikulu na waliotafuta Kura za Lowassa. Hii ndio Vita kubwa kuliko zote kwa CCM kuelekea 2020.
Je chama kitawapa Wahamiaji nafasi na kuacha watoto wake waliopigana usiku na mchana na matusi yote walihotukanwa? Nakumbuka 2015 ulikuwa ukivaa sare ya CCM unatukanwa unazomewa unadhalilishwa vya kutosha lakini Kuna watu walijitoa Sana, wakakubali kutukanwa, kuzomewa, wakakubali kudhalilishwa ili Mgombea wetu aingie Ikulu.
Nitoe Wito kwa Wana CCM wote waliopigana usiku na mchana 2015 kuungana katika Vita hii. Dr Bashiru aliwaita wahamiaji kuwa Ni vifaru Sasa tuwaonyeshe kwa vitendo kuwa tuna utimamu wa akili kuliko wahamiaji. Tukatae dharau, tukatae kutukanwa, tukatae udhakikishaji huu.
Watakula walikopeleka Mboga 2015.
Nimekaa pembeni hapa nawachora tu wahamiaji hahahah mtajuta.....