Uchaguzi 2020 Mwita Waitara ahoji kwanini Naibu Spika Dr. Tulia hajaitwa kwenye kamati ya maadili?

Uchaguzi 2020 Mwita Waitara ahoji kwanini Naibu Spika Dr. Tulia hajaitwa kwenye kamati ya maadili?

nokwenumuya Kitu pekee tu ninachokijua ni kwamba wale Wabunge wote waliohamia CCM kutoka huko walikotoka iwe kwa utashi Wao wenyewe au Walihongwa au hata Walitishwa hakuna ambaye kuelekea Uchaguzi huu Mkuu ujao wa 2020 atapitishwa na CCM Kugombea. Safari yao ndiyo imeishia hapo na tena nawashauri waanze Kujiandaa mapema sana Kisaikolojia.
 
Asubiri UDC au sio???
 
Kheri ya Pasaka kwa Watanzania wenzangu.

Kama tunavyojua mwaka huu kuna harakati za Uchaguzi Mkuu na tayari wanasiasa wameanza kuzunguka hapa na pale katika kutafuta kuungwa mkono.

Na kila chama kina taratibu, miiko, makatazo na kanuni katika kuelekea katika uchaguzi huo.

Chama Cha Mapinduzi kilitoa katazo kwa makada wake kujizungusha majimboni kabla ya Wakati na mara kadhaa kupitia Katibu Mkuu na Makamu Mwenyekiti wamekuwa wakisisitiza hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wanaokiuka makatazo hayo.

Lakini kama kawaida sio watoto wote huwa na utii. Wengine hukiuka na kutumia njia za ujanja ujanja.

Moja ya watu waliokumbana na pitapita hiyo ni Mh. Mwita Mwikwabe Waitara, Mbunge wa Ukonga na Naibu Waziri wa TAMISEMI.

Baada ya kujitangaza hadharani kuwa atagombea Ubunge jimbo la Tarime Vijijini hapo January Mosi, 2020, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Ndugu Samwel Keboye alimkemea kwa kufanya hivyo kabla ya wakati na akasema kuwa ataitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Mkoa kujibu tuhuma za kuanza kampeni kabla ya wakati, na mwezi March aliitwa na kuhojiwa.

Sasa katika kundi la WhatsApp la CCM Tarime, Kuna mwanachama alitupia picha ikionyesha taasisi ya Tulia inayomilikiwa na Naibu Spika, Dr. Tulia Ackson ikionyesha matangazo ya mikopo ya Bajaj.

Ndipo Naibu Waziri, Mh. Waitara akahoji ni kwanini Dr. Tulia hajaitwa kamati ya Maadili ili kujibu tuhuma za kuanza kampeni kabla ya wakati? Na akaendelea kuuliza je na Dr. Tulia ataitwa kama na yeye alivyoitwa??

Nimeweka screen shot ya comment ya Naibu Waziri hapa.
View attachment 1418270
Wanatumia gharama kubwa Sana kununua kura wakipata kurudi Hadi wakati wa chaguzi
 
Haihitaji kuwasha tochi, koroboi, wala mshumaa ili kung'amua kuwa Dr. Betina ni mbunge ajae wa Mbeya mijini. Sugu should've started packing his mats.
Wachache hawatakuelewa

Sent from Tapatalk
 
Hata huko asahau labda awatoe ' Kafara ' wana Ukoo wake wote. Imeisha hiyo Mkuu!
Ila kwa yeye anavyowaambia watu wa Tarime hadi kafanikiwa kumrubuni Mwenyekiti wa CCM Tarime ni kwamba yeye ameagizwa na Rais Magufuli na kuwa atapewa Uwaziri Mkuu, hivyo wampiganie nae atawapigania.
 
Yeye mwita ni CCM makinikia, ni mtoto wa kambo, ni wakuja, hivyo basi atulize mshono asilete ujuaji. Matumizi yake yana expire hii 2020 baada ya hapo anatupwa chooni kama kondom iliyotumika kuibaka demokrasia. Awe mvumilivu mwisho unakalibia.

Mwita Waitara ni kama Mtoto mkubwa aliyezaliwa, akakulia Nyumbani akaenda kusoma Ng'ambo kisha akarejea Nyumbani kwa wasiomfahamu ndio watamshangaa kwa vile ndio wanamuona kwa muda huo na kushangaa kwao hakumfanyi kuwa Mgeni!
 
Na ndie Waziri Mkuu ajaye 2020 baada ya uchaguzi mkuu
 
Back
Top Bottom