Ndugu zangu, kama nilivyosema Watanzania tuna tabia ya kusameheana.
Mr Suggestion, labda hukuwa unafuatilia utawala wa daruso wakati huo au ulikuwa ndio kwanza unaingia, waulize wenzio waliokuwa wakongwe kwako watakwambia, mie sizungumzie Magesa ambaye nae aliishia kuwa fisadi tu, nazungumzia Mwita Mwikwabe Waitara, aliyeingia madarakani kwa kusaidiwa na mpiganaji wa wakati huo Tweve.
Naamini waliokuwa UDSM wakati huo japo wanaweza kumsamehe ni mashahidi hapa, utawala wa mwita ulidissappoint sana watu maana watu walijua wameingiza wapiganaji kumbe wameingiza mafisadi na wezi, jamaa walikuwa busy kupiga deal na kula pesa tu, kila kitu kwao ilikuwa biashara.
Msifieni kwenye mengine ila mkitaka kumsifia kuhusu urais UDSM mtaharibu maana wengi wanaufahamu utawala wake pale.