Greenwhich
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 1,337
- 968
- Thread starter
- #61
MASONJO SAMAHANI NIKUULIZE, ulisoma kozi gani pale UDSM?
na ulikuwa mwaka wa ngapi wakati Waitara akiwa Rais wa DARUSO?
Je, Unaweza kutueleza wana janvi ni deal gani alizokuwa akipiga akiwa kama Rais enzi hizo?
Kwa ufupi tu nikufahamishe, Mwita Waitara ni kiongozi shupavu asiyepelekeshwa hata kidogo na husimamia vema masrahi ya anaowaongoza.
Mimi kama Rais wangi enzi hizo, aliwahi kutuongoza kuikataa test ya Dr, aliyekuwa analazimisha tuifanye Jumapili badala ya katikati ya wiki, ambapo ndio siku muafaka ya kufanya Test. Kumbuka miongozo ya chuo hairuhusu kufanya test jumamosi wala jumapili.
Test haikufanyika na Dr. yule akakasirika na siku alipoileta katikati ya wiki akawa ameikaza balaa, lakini tukaipiga na akashindwa kutukamata. Manake test ya masaa mawili liliypangwa kufanyika J2 iligeuka kuwa ya Dr 60 ( saa 1) kwenye kipindi.
Sasa kaka, mtu kama huyo asiyepnda kupindishwa kwa sheria huoni kama ndiye anayefaa. Acha kumpakazia Mtu wa watu huyo.
Mwita Nakutakia kila la kheri kaka, na ungekuwa jimboni kwangu familia yangu yote ungechukua kura zao.
Mkuu wangu mamakunda nikuhakikishie tu hakuna wa kumzuia mwita Waitara kuchukua ubunge Ukonga.CCM imekufa kifo cha mende kwa kushindwa kutatua matatizo ya wananchi hasa ubovu wa barabara zote za Ukonga.
Unapoona michepuko ikimshambulia hapa ujue ameiweka CCM katika hali mbaya sana kisiasa..
Last edited by a moderator: