Mwita Waitara anusurika kipigo cha mbwa mwizi Mwanza

Mwita Waitara alikwenda kukagua ujenzi wa Zahanati ya maina na wananchi wakamlalamikia mkurugenzi wa Allience ambaye ni diwani mh Bwire.

Mwita Waitara alijaribu kumtetea Bwire kuhusu kuvamia kiwanja cha wazi ndipo wananchi wenye hasira wakaanza kumzomea, kumkejeli na kumtukana na wengine wakaanza kumsogelea ili wampe kichapo ndipo Naibu waziri akatoka mkuku huku akisindikizwa na mayowe ya huyo...... huyo...... huyoooooooo.

Chanz: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Video tafadhali
 
Salaam.

Taarifa nilizozipata kupitia chanzo changu kinasema Naibu Waziri wa Tamisemi Mh. Mwita Waitara amenusurika kupokea kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira.

Tunaendelea kufuatilia sababu ya Mh. Waziri kunusurika kipigo.
 
Hiyo ni rasharasha, masika inaenda kunyesha October.

Mwananchi mmoja amesikika akisema: "tunajua kilichomleta, ametumwa kuja kuvuruga na hatovuruga"

Watanzania wameshachoka kuchezewa akili na hawa watu.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ka video kangependeza
 

Hiyo ni rasha rasha tu. Wananchi wamewachoka hawa viongozi wanaojipendekeza pendekeza kwa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…