Mwitikio wa serikali na wananchi kusaidia wahanga wa milipuko ya Mbagala

Mwitikio wa serikali na wananchi kusaidia wahanga wa milipuko ya Mbagala

thread nzuri lakini 'IMEISHIA HEWANI'

LOL!
who will i blame jaman?
LOL!
 
thread nzuri lakini 'IMEISHIA HEWANI'

LOL!
who will i blame jaman?
LOL!

Fidel; Usikate tamaa, endelea kuichangamsha mkuu!

Hakikisha all the time iko kwenye top 20.
 
Dah inauma sana hakuna mwamko kabisa watu wapo kimyaaaa. Sasa sijui hii ni nn au ndo utanzania wenyewe ndivyo tulivyo?
 
TZS 50,000 From Superman

Ca I also request a Winner of 2009 JF Superlady and Celebrity to Contribute?

Msimamizi wa Uchaguzi ZeMarcopolo na Pia Mwanafalfasa, please come forth.

Please people, come up, let us show a way that JF is practical serious on sensitive issues as well.

Big Up Fidel for this idea!

Tupo pamoja mkuu. Ngoja tupate utaratibu wa kuchangia. Now this is what I call affirmative action siyo watu kuongea tu kila siku.
 
Mimi nadhani kabla ya kuchangia niambiwe na amewajibishwa?
 
Toka jana naomba mods wafanye utaratibu watu tutoe kidogo tulicho nacho kwa ajili ya wahanga hawa wa mabomu Mbagala lakini kama mnavyo ona mods wote wapo kimyaa mpaka muda huu. Wangetupa tu alternative ya kufanya michango si inawakilishwa kwenye ofisi ya Mkuu wa Mkoa pale chochote kile nauhakika wanapokea.
Jamani kama umeguswa tunaomba tuwe pamoja hata kwa swala/sala kuwafariji ndugu zetu si sote ni binadamu leo kwao kesho kwetu. Nawakilisha wakuu.
 
nina imani kubwa sana kila mmoja wetu hapa jf ameguswa sana na kilicho watokea ndugu,jamaa,rafiki,watanzania wenzetu kule mbagala baada ya maafa ya yale mabomu.
Hivyo basi kama umeguswa kwa namna yoyote ile tunaomba kama wana jf tutoe kile kidogo tulicho nacho ili kuwakumbuka na kuweza kuwasaidia wenzetu kule maana wote na uhakika ni watanzania wanao teseka kwa kulala nje ,kuwakiwa na jua mchana wengine huibiwa vitu na mali zao kwa nyakati tofauti.
Binafsi naomba wana jf wenzangu kama umeguswa tunaomba mchangie ili tuweze kuwasaidia wenzetu hawa. Naomba mods mtafute njia ili tuweze kuleta michango yetu au tutumie ile ile njia ya changia jf?
Mi mwanzilishi najitolea 20,000/= kwa ndugu zetu wahanga wa mabomu.
Karibuni nyote.

mkuu tuko tayari kuchangia madawati na meza za walimu kwa picha ya shule iliyo wahi kuonyeshwa hapa jamii forum tumejitahidi kupata ile picha kwenye thread lakini tumechemsha tafadhali kwa yeyote atayeweza kutuma hio picha tena hapa itatusaidia kufikisha msaada na tuta toa reference kuwa jf imekuwa source yakusaidia hao watotot wanafanyia mitihani mchangani.

mods tusaidie ile picha iliwahi kuonyeshwa mwezi uliopita hapa
 
Peter Masangwa na Salum Pazzy

SERIKALI imeahidi kuwalipa mafao kwa muda wa maisha yao yote, watu wote waliopata ulemavu wa aina mbalimbali kutokana na milipuko ya mabomu iliyotokea katika ghala la silaha la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Aprili 29, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Wiliam Lukuvi, alisema watu hao watalipwa fidia kulingana na madhara yaliyowapata.

Bw. Lukuvi alisisitiza kuwa Serikali ipo pamoja nao kwamba na itawasaidia kuendesha maisha yao ya kila siku.

Alifafanua kuwa mafao watakayokuwa wakilipwa watu hao , yatajulikana baada ya wataalamu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kutoa mchanganuo wa kile wanachostahili kuwa wanalipwa kulingana na aina ya ulemavu waliopata.

"Wizara ya Afya ndio inahusika na kufanya hesabu, nimewaagiza watuletee idadi kamili ya watu waliopata ulemavu wa kudumu pamoja na mapendekezo yao," alisema Bw. Lukuvi.

Alisisitiza kuwa taarifa hiyo itaambatana na ile tathmini ya maafa itakayotolewa Juni 13, mwaka huu.

Bw. Lukuvi alisisitiza kuwa yupo makini kwa kuwa anaguswa na maafa yaliyowapata wakazi wa Mbagala.

Kuhusu vurugu zilizotokea wakati wa ugawaji misaada kwa waathirika wa mabomu, Bw. Lukuvi alisema kazi ya kusimamia ugawaji wa misaada hiyo ameachiwa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Bw. Said Mkumbo.

Source:Waliopata ulemavu Mbagala kulipwa mafao milele
 
Wakuu sioni response yeyote ile.
Naomba mods mfunge thread
 
KWELI BANA!hii mimi sielewi tafsiri yake nin?
 
Mamod wame jibu kuhusu process za kuchangia mkuu?

Mkuu wapo kimyaaaa kama vile hawajaona hii thread.
Ndo maana nawaomba wafunge basi mjadala na vile vile naona watu hawajaguswa na wahanga wa mabomu.
 
Mkuu wapo kimyaaaa kama vile hawajaona hii thread.
Ndo maana nawaomba wafunge basi mjadala na vile vile naona watu hawajaguswa na wahanga wa mabomu.

Nadhani watu wame guswa mkuu sema kama hakuna taarifa kamili ya jinsi ya kuchangia na mambo kama hayo lazima watu wataona thread ni uzushi tu.
 
Nadhani watu wame guswa mkuu sema kama hakuna taarifa kamili ya jinsi ya kuchangia na mambo kama hayo lazima watu wataona thread ni uzushi tu.

Ndo maana nikaomba msaada kwa mods kama vp tunaweza tumbukiza kwenye ile Changia JF ingekuwa rahisi sana.
 
ha!ha!ha! ujapata jibu ni kwa nn mods wapo kimya? jaribu kutafakari zaidi utapata jibu.Ukishindwa kupata jibu ni PM nikupe JIBU.
 
ha!ha!ha! ujapata jibu ni kwa nn mods wapo kimya? jaribu kutafakari zaidi utapata jibu.Ukishindwa kupata jibu ni PM nikupe JIBU.

hehehe haya bana napata ufahamu kidogo kidogo.
 
mkuu tuko tayari kuchangia madawati na meza za walimu kwa picha ya shule iliyo wahi kuonyeshwa hapa jamii forum tumejitahidi kupata ile picha kwenye thread lakini tumechemsha tafadhali kwa yeyote atayeweza kutuma hio picha tena hapa itatusaidia kufikisha msaada na tuta toa reference kuwa jf imekuwa source yakusaidia hao watotot wanafanyia mitihani mchangani.

mods tusaidie ile picha iliwahi kuonyeshwa mwezi uliopita hapa

ofisini kwetu tunatoa sehemu ya faida kwa ajili ya kusaidia nilitoa idea ya mbagala lakini wakasema ni vizuri tukawapa picha unajua tena bosi akiwa mweupe/mzungu inakuwa hivyo/facts sasa kama ile picha ningeipata tungetoa mchango mkubwa ambao ungesaidia wale wanafunzi sikumbuki aliyebandika ile picha ni nani
 
Nimekumbuka ile shule ya miti sio? Au mbweni lile la secondary ya Tanga ?
 
nimekumbuka ile shule ya miti sio? Au mbweni lile la secondary ya tanga ?

hapana fidel80 ilikuwa picha ya mbagala inayoonyesha wanafunzi wamekaa chini ya mti wanafanya mitihani na hawajavaa viatu, iliniuma sana jua lao mvua yao wakati wizara zetu zina magari ya kifahari wakiuza/wasiponunua 1 linatosha kuwapa watoto wale uhauweni leo jioni tunaingia kwenye kikao cha kuamua misaada hio iende wapi
 
@ Nguli, hiyo thread ilianzishwa na Game Theory inaitwa 'Picha itakayomsuta JK na wabunge wake mamilionea'...nimeshindwa kuweka link ila ipo jukwaa la siasa..Kuna picha inawaonyesha wanafunzi wamekaa chini na sare zao za shule ( yaani ndo darasani kwao hapo kwenye mchanga).

@ Fidel - Imani ya watu kuchangia wana mbagala ipo ila jinsi ya kufaniksha hili zoezi ni gumu maana watu tupo sehemu mbalimbali na pia hupati uhakika kama walengwa watafikiwa na msaada wetu. Nikijua utaratibu, nitakujulisha na mie..

Siku njema!!
 
Back
Top Bottom