Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Mwitikio wa Serikali na Wengine juu ya Mengi kutaja mafisadi!

Tamko la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Tabora

Ndg wanahabari,
Waheshimiwa ndugu waandishi tunashukuru sana kwa kujitokeza siku ya leo kuja kutusikiliza, tunaomba muendelee na moyo huo kutumikia jamii kwa kutoa habari za uhakika zenye tija na taifa letu.Mungu awabariki sana kwa hilo.

Tungependa kwanza kutumia fursa hii kuwapa pole wakazi wa Jiji la Dar es salaam, hasa maeneo ya Mbagala na Maeneo yote kwa Ujumla kwa tukio la jana la milipuko ya mabomu, na kuwapa pole majeruhi wote walioathirika na tukio hilo, na pia kuwapa pole familia zote waliofiwa na ndg zao kutokana na tukio hilo, mungu azilaze pema peponi roho zao, na tunawaombea majeruhi wapone haraka.

Tuliopo hapa mbele yenu ni Mwenyekiti UVCCM Mkoa, Mjumbe wa Baraza kuu Taifa na wenyeviti wa UVCCM wa wilaya zote za mkoa wa tabora, maana yake wilaya ya tabora mjini, Nzega, Sikonge, Igunga, Urambo,na Uyui. Pia tunaye katibu wa Uhamasishaji Uvccm wa Mkoa wa Tabora. Tumekuja hapa Dar-es-Salaam tangu juzi kwa ajili ya kufuatilia maandalizi ya fundraising kwa ajili ya miradi ya vijana wa mkoa wa Tabora, na tunaomba tuwahakikishie vijana wenzetu kwamba mipango inaendelea vizuri sana, na inshaalah mungu akijalia, maandalizi yatakuwa yamekamilika wakati tunarejea Tabora.

Aidha tumeamua kuongelea kauli ya Mfanyabiashara wa IPP, Ndugu Reginald Mengi aliitisha vyombo vyake vya habari na kuanza kutukana na kuhukumu watanzania wenzake, ni kauli ambazo hazivumiliki kwa mtu aliyestaarabika kutuhumu watu kwa maslahi binafsi na anyoyafahamu mwenyewe bila kufata misingi ya sheria.

Kauli hizo licha ya kuleta harufu ya ubaguzi wa rangi pia inakuza chuki ya raia dhidi ya wenzao kwa mtazamo kuwa umasikini wao unakuzwa na kundi la watu kwa manufaa yao. Aidha linatoa taswira kuwa serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa kiwango cha kuwaruhusu baadhi ya watu kuharibu nchi, jambo ambalo lina lengo la kuigombanisha serikali na wananchi wake.

Bila kujali utawala wa sheria na haki ya msingi ya binadamu, tunaamini kila mtanzania anayo haki sawa kabisa. Tunapenda kuishukuru na kuipongeza sana Serikali kupitia Waziri wa Utawala Bora na Waziri wa Habari kwa kukemea kitendo hicho na kuendelea kusisitiza Taifa lenye utawala wa Sheria.

Kilichotusukuma sisi leo kama Vijana wa CCM wa mkoa wa Tabora ni jinsi ambavyo Ndugu Mengi alimtaja mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM - Mhe Rostam Aziz, ambaye vilevile ni Mbunge wa Igunga. Wadhifa nyigine ambazo amewahi kushika ni pamoja na Mweka Hazina wa CCM Taifa, pia kwa sasa ni Mjumbe wa NEC kupitia mkoa wetu wa Tabora na Kamanda wa UVCCM wilaya ya Igunga, maana yake ni KADA kwelikweli wa CCM na nyumbani kwao ni Mkoa wa Tabora, tukaona hili haliwezi kupita bila sisi kama vijana kuja kutetea Chama chetu. Kazi kubwa ya Umoja wa Vijana ni kutetea uhai wa CCM na Viongozi wake pale tunapo amini kuwa wanasimamia maslahi ya Taifa.

Hivi karibuni kumetokea hali ya mabadiliko ktk mfumo/tabia yetu ya kutoa mawazo kama wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Ikiwa ni haki ya mtu kutoa mawazo, ni haki iliyoainishwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini haki hiyo inapotumiwa vibaya kwa maslahi binafsi, na kwa nia ya kuwachafua wengine haki hii hugeuka kuwa vurugu na vurugu hizi zinaweza kupelekea hata machafuko kwa kupandikiza chuki miongoni mwa jamii yetu.

Ndg wanahabari, baada ya utangulizi hapo juu, sisi kama viongozi wa UVCCM wa wilaya zote na mkoa wa Tabora na kwa niaba ya UVCCM (M) Tabora, tunaomba kusema yafuatayo:

1. Tunalaani kauli kuwa Mh Rostam Aziz, kama kiongozi wetu na kamanda wa Umoja wa Vijana wilaya ya Igunga kudhalilishwa hadharani na mtu bila kuleta ushahidi wowote, tunamtaka Mzee Reginald Mengi atuombe radhi wana CCM wa mkoa wa tabora kwa kumtuhumu kiongozi wetu ambaye wananchi wake wana imani naye sanjali na wana Tabora, na amechaguliwa kidemokrasia na wananchi wengi tu. Tukiacha kauli yake bila kukemea maana yake tumekubaliana, jambo ambalo siyo kweli na kazi zake katika mkoa wa Tabora na wilaya ya igunga ni ushahidi tosha.

2. Tunalaani matamshi ya Ndugu Reginald Mengi dhidi ya Raia wenzake, na tunahoji nafasi ya ndugu Mengi kwenye jamii mpaka achukuwe nafasi ya kutuhumu, kuchunguza na kuhukumu. Raia yoyote wa Tanzania mwenye nia njema anaruhusiwa kisheria kupeleka ushahidi au kushitaki na kufungua kesi dhidi ya yeyote anayehujumu Taifa, kama kweli anayosema kwanini asiende mahakamani kuwafungulia kesi watu hawa na kuishtaki kwa maslahi ya Nchi. Tunaomba serikali kama ambavyo Mhe Mkuchika amesema, kuchunguza kauli za Ndugu Mengi na kumchukulia hatua kali zakisheria ili watu waheshimu utawala wa sheria nchini.

3. Tunahoji nafasi yake ni nini kwenye CCM? Na kwanini anatumia majukwaa ya CCM kutukana viongozi kama anavyojisikia,na kutamka kuwa wateule wa Rais ni wezi. Ndugu Mengi anayo historia ya kulumbana tena kwa kashfa na Mawaziri wengi nchini, tunamtaka aache mara moja na kama anataka siasa aingie kwenye ulingo wa siasa na tutakuna nae kwenye majukwaa ya kisiasa

4. Tunaiomba serikali iangalie upya sheria na matumizi haya mabaya ya vyombo vya habari ambayo yanaweza kuleta mtikisiko mkubwa kwenye nchi, mgawanyiko na serikali iweze kupiga marufuku tabia hii ya Bwana Mengi kutumia umaskini wa watanzania kupandikizia chuki watu wengine.

5. Tumefuatilia kwa karibu mwenendo na Ziara za Ndugu Mengi akiwa na Msafara wa Wabunge huku akitoa Misaada Mbali mbali, na tumepata taarifa kwamba anakuja katika wilaya ya Mkoa wa Tabora, Uvccm Mkoa wa Tabora inatoa Angalizo ikiwa kama misaada yake inaendana na tabia ya kutukana na kuwaundia majina mabaya viongozi wetu wa Chama, tunamuonya kama vijana wa Tabora na kamwe hatutavumilia jambo hili. Wananchi wa Tabora wana matatizo mengi, lakini vilevile wanaheshimu utu na kamwe hatuwezi kukubali matatizo yetu yatumike kudhalilishwa utu wetu na wa viongozi wetu tuliowachagua kidemokrasia.

6. UVCCM tunamuunga mkono MNEC wa Mkoa wa Tabora Mh Rostam Aziz(Mb) na kuwaambia Watanzania kuwa Mkoa wa Tabora tuna imani naye na hatuna shaka juu ya Uzalendo wake kwa Taifa hili tunafahamu anafanya biashara zake halali na hajawahi kushtakiwa na serikali kuwa amekwepa kodi zozote anazotakiwa kulipa na kwa hili uzalendo wake hauna shaka , na kumtaka asivunjike moyo, hizi ni kelele za watu wenye nia mbaya na tunamuahidi tutakuwa naye bega kwa bega katika kipindi hiki na hatutaruhusu kauli chafu dhidi ya kiongozi wetu. Tunathamini sana mchango wake wa muda mrefu kwa Chama Cha Mapinduzi na maendeleo anayohangaika nao kwa wananchi wa jimbo la igunga na mkoa wa tabora kwa ujumla.

7. Uvccm Mkoa wa Tabora, tunatoa angalizo kwa watanzania wenzetu kuwa Tusiruhusu UKABURU kutuingia kwa mtu kuja na hoja ya UBAGUZI ili kuwajengea chuki Watanzania . Tabia hii Baba wa Taifa aliwahi kuikemea na kuifananisha na ukaburu tusiruhusu makaburu kuibuka katika nchi yetu.

8. Uvccm mkoa wa Tabora, tunakemea na tunashauri Chama Cha Mapinduzi kuchukua hatua kurudisha nidhamu ndani ya chama na Serikali kwani CCM ndiyo chama tegemeo. Kwani hivi sasa kuna kashfa, malumbano ambayo hayasaidii nchi na kutoruhusu mijadala ambayo itatuyumbisha kama taifa, tabia ya aina hii si jambo zuri bali ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu.

9. Mwisho tunapenda kuwahakikishia wanahabari na watanzania kwa ujumla Uvccm mkoa wa tabora tunamuunga mkono MNEC wetu na hatuko tayari kuona anadhalilishwa bila kuwa ushahidi wa jambo lolote na imani serikali haitaruhusu tabia ya watu kujitafutia umaarufu kwa Gharama za kuchafua wengine.

10. Uvccm Mkoa tunatoa angalizo kwa Wabunge wa Majimbo yote ya mkoa wa Tabora ,na wa viti maalum kuwa wakasimamie utekelezaji wa Ilani ya CCM kama walivyoahidi kwa wapiga kura, pia tunatoa wito kwa wabunge wa Mkoa wetu wanaoambatana na Misafara ya Bwana Mengi wajiepushe na misafara inayokashifu na kuita majina mabaya viongozi wetu na wao kuwa sehemu ya jambo hilo wakishangilia. Kwa kuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP ana Tabia ya kutumia majukwaa ya CCM na kukashifu watendaji wakuu wa serikali na wakati huo huo kumsifia Rais kwani huwezi kumsifia Rais wakati unakashifu na kuwaita watendaji wake wa chama na Serikali kuwa ni Mafisadi na hawamsaidii Rais kimantiki ni kwamba anakosoa uteuzi wa Rais na kuonyesha kuwa unamapungufu. Vijana hatutakuwa tayari kubeba wabunge 2010 wanaoshiriki katika ziara ambazo zinakichafua chama na serekali kupitia kivuli cha kusaidia wanyonge.

11. Tunasisitiza tunalaani kauli ya Mengi na tunaomba serekali itekeleze alichosema Mh Mkuchika.

AHSANTENI SANA, MUNGU AWABARIKI

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

Naona 400 milions zinafanya kazi yake,ukiwa na pesa burdani kweli,ukiwa na pesa kama Somaiya,aah,hakuna shida....Watanzania wajue ccm imenunuliwa,na kama na wao wamo ndani ya kapu haya,tufanyeje sasa,maana JK mwenyewe kimyaa!
Yani ni shida kujuwa yuko upande gani,naona shida iko kwenye hao watano waliobaki ambao Mengi hajawataja,ila kutajwa kwa kina Subash Patel ni sawa na kutajwa kwa JK mwenyewe hilo liko wazi,na kwahiyo JK amewekwa kwenye mtego ambao hawezi kujinasua kwani maji moto ni unga tu unahitajika ugali uliwe.
R.E Mengi si mjinga kama wapambe wa mafisadi wanavyofikiri.
Shukran kwa R.E Mengi kwa kujitolea kwa ajili ya Taifa letu na kuazisha chachu kwa watanzania,chachu ya ukombozi,time is running out,na kutokana na pressure iliyopo, explosion lazima itokee ili taifa letu listawi.
 
Jana wazee wa Yanga walitoa kauli kuhusu mfadhili wao kutobughudhiwa hata kidogo. Juzi mapato ya mechi ya Yanga Vs Simba yalikuwa kidogo sana mpaka wadau wote ikiwemo Serikali imestushwa na udogo wa mapato ukilinganisha na idadi ya watuwaliongia uwanjani. Kwakuwa Yanga ni taasisi ya michezo na imekuwa ikitegemea viingilio vya mlangni kuendesha timu yao tokea ianzishwe hadi juzi juzi tu ndipo timu hiyo imekuwa ni taasisi ya mtu binafsi.

Ni kwanin wazee hawa hawajatoa tamko kuhusu uchache wa mapato ya mechi timu yao inazocheza? Je kwa kushindwa kutolea tamko masuala ya michezo ambyo ndio core function ya taasisi yao na badala take wakakamua kujiingiza katika mjadakla ya ufisadi ambapo mtuhumiwa sio siri anatumia fedha nyingi kwa timu hiyo. Je wazee hawa hawajageuzwa sehemu ya ufisadi hapa nchini?

Kwa kuwa kuna wakati wazee hawa hawa walikuwa wakingaa kwenye vyombo vya habari wakimsifia Mengi kwa ufadhili wake japo mdogo, na sasa wanafadhiliwa na mtuhumiwa wetu wa ufisadi, hawafanani na mke anayechangua mume kutokana na uwezo wke kifedha (natanguliza samahani kwa kutumia mfano ambao is a bit gender sensitive)
 
Pole sana mpambanaji,tatizo umaskini unaouona Tabora hauko huko tu ni sehemu nyingi.Kinachosumbua kwa watanzania wengi ni fikra tegemezi hawawezi kusimamia hoja zao wenyewe.Ni bahati mbaya Rais wa kwanza alikuwa msomi na akili nyingi na alioongoza kwa mda mrefu.Hivyo fikra za watanzania wengi ukishakuwa kiongozi wao fikra zao zinawatuma kuwa una uwezo wa kufikiri kuliko wao na kuangukia kila wakati kusubiri maagizo ya watawala wao.
Juhudi ya kuanzisha wazo na walisimamie wenyewe hawana,Mwalimu aliwadekeza kufikiri kwa niaba yao.Nashukuru sana Mwanakijiji anahangaika kuwatoa kutoka huko kwamba mungu aliwapa mwalimu tu na hatoi mara mbili.Nakumbuka hotuba ya kihistoria aliyotoa Mbeya siku ya mei mosi watawala wetu hawataki kuirudia.Na wamehakikisha electronic media hairudii hotuba ile wakihofia wananchi wasielewe namna ya kutafuta viongozi bora.

Mpoki,

Nakuelewa na asante sana kwa Pole. Ila hizi habari na picha huwa nikianza kuzisikia na kuona huwa namkumbuka marehemu baba. Mzee aliishia darasa la nne ila alikuwa na akili sana kuzidi hao vijana wa CCM na tena ukichanganya wotee!!
Siku moja alituchukua hadi sehemu ambapo ilikuwa imebaki sakafu na wanakijiji wanatumia kukaushia unga. Akatuuliza mlishawahi kufika, mnajua hapa palikuwa nini? Tukasema hatujui. Akasema hapa Wakatoliki walikuwa wameanza kujenga mission yao na haya ni mabaki ya majengo yao. Hili lilikuwa eneo zuri sana na walilipenda. Ila tatizo moja likazuka, mnaona lil jengo? (Umbali kama wa nusu km), tukasema ndiyo (ulikuwa msikiti), ilizuka vita moja kubwa sana. Moja ya watu wapinzani wa jamaa kujenga pale alikuwa Sheik mkuu wa kijiji (wa wakati ule). Wazungu mwisho wakachoka na wakaondoka. Mzee alisema kuwa kama pale pangejengwa basi kijiji chetu leo hii tungelikuwa na ndugu na jamaa wengi ndani na nje ya nchi na huku wengine wakiwa na vyeo vikubwa sana. Hadi leo nikikumbuka huwa siamini kuwa ni maneno yanayotoka kwa mzee aliyeishia darasa la 4.
Sipo hapa kukashifu dini ya Kiislam na sababu kubwa ni kuwa nusu ya familia yangu, marafiki na jamaa ni waislam. Ila ukweli ni kuwa Wanyamwezi tunapenda sana kuwa na wake wengi na dini ya Kikristo ilikuwa inazuia. Hivyo wengi walikuwa wanaingia kwenye Uislam kama fasion maana inabidi uwe na dini na kigezo kikubwa unaweza kuwa na wanawake hadi wanne ingawa ukiangalia ni kuwa wengi walikuwa hawawapendi wote sawasawa kama dini inavyotaka. Pia ukiwa na wake wengi unakuwa na watoto wengi na hivyo unakuwa na Manpower almost ya bure (utumwa wa aina fulani) huku wewe baba ukiwa unatanua tu au kujifanya umekuwa mmfanya biashara na wanao/wake zako ndiyo wana produce.

Nafahamu kuwa hata mikoa mingine kuna umasikini. Ulaya/USA pia wako. Ila tatizo la Tabora kubwa kabisa ni umasikini wa mawazo. Unakuta mtu ana akili zake timamu, ardhi ya kutupa Sikonge, ana afya tele lakini analalamika kuwa hana pesa na summer nzima amekaa tu anasubiri msimu wa mvua ndiyo aanze kazi. Hajishughulishi kwenye kilimo cha nyanya, miwa, vitunguu, kabegi, michicha nk au kwenda kwenye ufugaji wa samaki, nyuki nk. Amekaa tuu!!! Akikuona anasema umpe visenti kidogo maana kakwama. Jioni ikifika, wao ni kwenye ulevi wa tende.....🙂 Ehhh bwana wee, Tabora kuna Bangi, gongo na Wanzuki kwa wingi sana.

Natoa ombi kwa mtu yeyote atakesoma hapa na siku moja awe Rais au PM. Ili sisi Wanyamwezi tuendelee, basi ni viboko lazima vitembee. Ndiyo kitu pekee ndugu zangu huamka. Vinginevyo basi labda kama alivyoandika Masanilo kuwa "Unafyeka kizazi kizima na kuanza upya...." Uzuri mmoja wa hawa Wanyamwezi ni woga sana. Ukiwatetemesha kidogo, watafanya kila kitu unachotaka. Viboko kwanza na shule ndiyo ifuate baadaye. Hawa wataendelea kuwachagua Vibaka hata kama vibaka watakuja na kubeba watoto wao. So longer wakati wa uchaguzi wamepewa vi-Tshirt.

Mafisadi wa Tabora wanalisikiliza sana huu wimbo na huwa wanautumia. Mwanzo ulikuwa utumike kuwashambulia wakoloni, ila sasa wanautumia wao kutunyanyasa sisi, huku wakizuia watu wengine wasiusikilize (mfano ni maneno ya Mwanakijiji uliyosema). Hebu angalia chini kuanzia dakika ya ya Kwanza (1:00). Yes, we don't want no Rostam philoso

[ame="http://www.youtube.com/watch?v=KyLLlgdY2aQ"]YouTube - bob marley-one drop[/ame]

They made their world so hard (so hard):
Every day we got to keep on fighting (fighting);
They made their world so hard (so hard):
Every day the people are dyin (dying), yeah!

And then you give us the teachings of his majesty,
For we no want no devil philosophy; (Rostam Aziz, Manji, Lowasa etc)
A you fe give us the teachings of his majesty,
A we no want no devil philosophy

NB: Mtoto mmoja wa Sheick mkuu wa kijiji nilimkuta akiwa ofisa wa elimu wa Mkoa. Nilishangaa sana na nafikiri aligundua. Akasema kisa cha yeye kusoma ni kuwa alisaidiwa na Mwalimu Kauga (Wale wazee Old School na walimu kwelikweli). Mwalimu Kauga alipoona jina la kijana akajua huyu hataletwa shuleni. Akaandika barua ya tishia nyau, na akawaomba Polisi waigonge muhuli. Jioni kijiji kizima kilipata habari kuwa Sheick kapata barua ya Polisi. Basi Sheick hakuwa hata na akili ya kufukiria zaidi ila kumpeleka kijana middle school (Mbirani, Sikonge) ambako alienda hadi akamaliza form 6 miaka hiyooooo huko Tanga. And his father was proud of him. Nilifika kwake na kukuta misahafu ya dini na mezani gazeti la New Africa na nikashinda siku nzima nasoma mpango wa Wanigeria kumteka nyara Diko na mpango ukakwama Hethrow Airport.
Kweli, kile kizazi kilikuwa kingine. Sasa hivi ni Watoto ambao baba zao walikuwa ugali wa Yanga na ma-bulga sijui??
 
Last edited:
Hawa wamesahau kwamba bila Mengi kuonyesha picha za mauaji ya Rwanda mwaka 1995 waingeshinda NCCR Mageuzi. Watumikia tumbo hawa. Ni uzalendo gani wanaouzungumzia ni ule wa kusimamia na kuendesha rushwa katuika chaguzi mbali mbali hapa nchini?

wakawadanganye wakulima wa Tumbaku waliozoea kuwaibia makato yao!!!!!!!!!!!!
 
Then mntakiwa kuwa gavana aitwaye Mnali, aliyewachapa viboko waalimu. This time vibokois demand driven.Whoops!!!!
 
Hatushangai sana maana ni juzi tu wamefadhiliwa na mmoja wa mafisadi, ukila nyama ya mtu utaendelea tu!
 
Mpoki,

Nakuelewa na asante sana kwa Pole. Ila hizi habari na picha huwa nikianza kuzisikia na kuona huwa namkumbuka marehemu baba. Mzee aliishia darasa la nne ila alikuwa na akili sana kuzidi hao vijana wa CCM na tena ukichanganya wotee!!
Siku moja alituchukua hadi sehemu ambapo ilikuwa imebaki sakafu na wanakijiji wanatumia kukaushia unga. Akatuuliza mlishawahi kufika, mnajua hapa palikuwa nini? Tukasema hatujui. Akasema hapa Wakatoliki walikuwa wameanza kujenga mission yao na haya ni mabaki ya majengo yao. Hili lilikuwa eneo zuri sana na walilipenda. Ila tatizo moja likazuka, mnaona lil jengo? (Umbali kama wa nusu km), tukasema ndiyo (ulikuwa msikiti), ilizuka vita moja kubwa sana. Moja ya watu wapinzani wa jamaa kujenga pale alikuwa Sheik mkuu wa kijiji (wa wakati ule). Wazungu mwisho wakachoka na wakaondoka. Mzee alisema kuwa kama pale pangejengwa basi kijiji chetu leo hii tungelikuwa na ndugu na jamaa wengi ndani na nje ya nchi na huku wengine wakiwa na vyeo vikubwa sana. Hadi leo nikikumbuka huwa siamini kuwa ni maneno yanayotoka kwa mzee aliyeishia darasa la 4.
Sipo hapa kukashifu dini ya Kiislam na sababu kubwa ni kuwa nusu ya familia yangu, marafiki na jamaa ni waislam. Ila ukweli ni kuwa Wanyamwezi tunapenda sana kuwa na wake wengi na dini ya Kikristo ilikuwa inazuia. Hivyo wengi walikuwa wanaingia kwenye Uislam kama fasion maana inabidi uwe na dini na kigezo kikubwa unaweza kuwa na wanawake hadi wanne ingawa ukiangalia ni kuwa wengi walikuwa hawawapendi wote sawasawa kama dini inavyotaka. Pia ukiwa na wake wengi unakuwa na watoto wengi na hivyo unakuwa na Manpower almost ya bure (utumwa wa aina fulani) huku wewe baba ukiwa unatanua tu au kujifanya umekuwa mmfanya biashara na wanao/wake zako ndiyo wana produce.

Nafahamu kuwa hata mikoa mingine kuna umasikini. Ulaya/USA pia wako. Ila tatizo la Tabora kubwa kabisa ni umasikini wa mawazo. Unakuta mtu ana akili zake timamu, ardhi ya kutupa Sikonge, ana afya tele lakini analalamika kuwa hana pesa na summer nzima amekaa tu anasubiri msimu wa mvua ndiyo aanze kazi. Hajishughulishi kwenye kilimo cha nyanya, miwa, vitunguu, kabegi, michicha nk au kwenda kwenye ufugaji wa samaki, nyuki nk. Amekaa tuu!!! Akikuona anasema umpe visenti kidogo maana kakwama. Jioni ikifika, wao ni kwenye ulevi wa tende.....🙂 Ehhh bwana wee, Tabora kuna Bangi, gongo na Wanzuki kwa wingi sana.

Natoa ombi kwa mtu yeyote atakesoma hapa na siku moja awe Rais au PM. Ili sisi Wanyamwezi tuendelee, basi ni viboko lazima vitembee. Ndiyo kitu pekee ndugu zangu huamka. Vinginevyo basi labda kama alivyoandika Masanilo kuwa "Unafyeka kizazi kizima na kuanza upya...." Uzuri mmoja wa hawa Wanyamwezi ni woga sana. Ukiwatetemesha kidogo, watafanya kila kitu unachotaka. Viboko kwanza na shule ndiyo ifuate baadaye. Hawa wataendelea kuwachagua Vibaka hata kama vibaka watakuja na kubeba watoto wao. So longer wakati wa uchaguzi wamepewa vi-Tshirt.

Mafisadi wa Tabora wanalisikiliza sana huu wimbo na huwa wanautumia. Mwanzo ulikuwa utumike kuwashambulia wakoloni, ila sasa wanautumia wao kutunyanyasa sisi, huku wakizuia watu wengine wasiusikilize (mfano ni maneno ya Mwanakijiji uliyosema). Hebu angalia chini kuanzia dakika ya ya Kwanza (1:00). Yes, we don't want no Rostam philoso

YouTube - bob marley-one drop

They made their world so hard (so hard):
Every day we got to keep on fighting (fighting);
They made their world so hard (so hard):
Every day the people are dyin (dying), yeah!

And then you give us the teachings of his majesty,
For we no want no devil philosophy; (Rostam Aziz, Manji, Lowasa etc)
A you fe give us the teachings of his majesty,
A we no want no devil philosophy
Pongezi bwana sikonge kwa kuonyesha ukweli kwamba jhata viboko ni demand driven ili Tabora iweze kuendelea. Kosa la Jk ilikuwa ni kumitimua kwa pupa pengine angemleta huko Tabora ilia wachalaze vibioko haswa hao vibaraka kutoka UvCCM
 
Nanyi msituletee za kuleta hapa Mengi amemtukana nani. Ameleza kile anachofahamu ambacho kinawakera wananchi wengi. Nyie mmekosa la kufanya basi nendeni kazibueni mifereji na vyoo mpate shughuli sio kukurupuka na kujidai sisi tunalaani kitendo bla bla pelekeni kule upuuzi wenu.
 
Ni njaa tu wao wanaona vijisenti wanavyopewa na fisadi Manji vina umuhimu mkubwa kuliko maslahi ya nchi yetu ambayo yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na ufisadi wa Manji.
 
Sikujua kwamba mtu aweza fisadi hadi bongo za watu!

Kumbe wale wazee wetu walio kuwa wanapewa shanga na wakoloni na kuuza nchi walikuwa sawa tu, Kwani sioni tofauti yao na hawa wa karne ya 21.
 
2009-04-30 14:37:56
Na Restuta James

Askofu wa Kanisa la Pentecostal Evangelistic lenye Makao Makuu mkoani Mbeya, Zebadiah Mwakatage, amemshambulia Waziri wa Nchi, Ofsi ya Rais (Utawala Bora), Sophia Simba, kuwa kauli yake ya kutetea mafisadi ni udhalilishaji serikali.

Alisema hali hiyo itafanya Watanzania kuamini kuwa waziri huyo na seikali yake wameajiriwa kuwa mawakili wa mafisadi.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Askofu Mwakatage, alisema anashangaza na kukatisha tamaa kwa tamko la serikali kupitia Waziri Simba, kutetea mafisadi na huku akijua umaskini unaokabiliwa Watanzania umetokana na kuchotwa kwa mabilioni ya fedha.

Alisema hata baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanaosema Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, anajipendekeza kwa Rais Jakaya Kikwete ni heri kuliko kujipendekeza kwa mafisadi kama alivyofanya Simba.

``Hivi Waziri Simba ameajiriwa uwakili na mafisadi kuyatetea, maana wao wana fedha tena wana midomo yao ambayo wao ndio wangelalamika, kwanini aibuke na kuwatetea eti ni wafanyabishara safi, hapa kuna mashaka,`` inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Alisema kutokana na maandiko matakatifu, Mengi asione ajabu kuchukiwa na mafisadi na baadhi ya viongozi wa serikali bila shaka wana maslahi wanayopata kutoka kwa mafisadi.

Askofu Mwakatage alisema kwa kuzingatia kuwa msema kweli ni mpenzi wa Mungu, Watanzania wataendelea kuwaombea waadilifu, wanaouchukia ufisadi kama Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroud Slaa, Dk Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Same, Anne Kilango, Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka.

``Nchi yetu tajiri kwa kila kitu, imebatizwa jila la dharau na aibu la umaskini, Mungu tuokoe. Wachonganishe ndimi zao mafisadi na waongo wote wasielewane,`` alisema Askofu Mwakaatage.

Juzi, Simba alijitokeza hadharani na kutetea wanaotuhumiwa kuwa mafisadi mapapa watano waliotajwa na Mengi na kwamba, kitendo cha kuwataja ni sawa na lugha ya kijiweni.

Simba alisema mapapa hao waliotajwa na Mengi ni watu safi na waadilifu kwa sababu, hawajahukumiwa na mahakama.

Alisema Mengi ameingilia kazi za serikali na kumtaka aiache ifanye kazi.
  • SOURCE: Nipashe
Hapo patamu. Sasa vita dhidi ya ufisadi inapamba moto walio upande wa ufisadi tutawajuwa na wa upande wa wananchi tutawajuwa
 
Alicho fanya mtumishi si kumshambulia bali kamweleza ukweli tupu. Alipo nifurahisha ni ombi lake kwa maulana awachanganye mafisadi waparulane!

Mungu hujibu maombi ya watu, na iwe hivo mtumishi.
 
- Nimewauliza wakulu huko ndani ya CCM, kwamba hii kauli ya UV-CCM maana yake ni nini kisiasa, the dataz ni kwamba:-

Kuna kijana anayeitwa Bashe, ndiye aliyeko nyuma ya hili tamko kwa 100%, nia na madhumuni yake ni kupata support ya Rostam ili amuondoe ubunge Seleli nothing more au less!

- Kila kiongozi anatafuta opportunity, hakuna anayejali wananchi wala taifa, huzuni sana kwa taifa hili!

Mungu Aibariki Tanzania!

FMES
 
Kuna kijana anayeitwa Bashe, ndiye aliyeko nyuma ya hili tamko kwa 100%, nia na madhumuni yake ni kupata support ya Rostam ili amuondoe ubunge Seleli nothing more au less!

Kamanda ndo vijana wenu hao mnawaandaa kuchukua uongozi wa juu wa chama na serikali...wamekaa kama mafisi kuvizia mizoga bila hata kufikiri.....wanatumika kwa njaa zao wala maslahi ya taifa hayapo! Rostam ni balaaa
 
- Finally Chadema! Kumbe wapo? Saaafi sana maana Mengi anahitaji msaada na bado sio too late, ingawa wamechele lakini wakati ni muafaka bado sasa tuweasikie kila wakati!

FMES!
 
Duh, kwenye msafara wa mamba hata makenge yamo. Haya ndi makenge yenyewe toka Tabora. Makenge ya namna hii yanastahili kuchapwa bakora.
 
- Nimewauliza wakulu huko ndani ya CCM, kwamba hii kauli ya UV-CCM maana yake ni nini kisiasa, the dataz ni kwamba:-

Kuna kijana anayeitwa Bashe, ndiye aliyeko nyuma ya hili tamko kwa 100%, nia na madhumuni yake ni kupata support ya Rostam ili amuondoe ubunge Seleli nothing more au less!

- Kila kiongozi anatafuta opportunity, hakuna anayejali wananchi wala taifa, huzuni sana kwa taifa hili!

Mungu Aibariki Tanzania!

FMES

Mungu hawezi kusaidia watu wa.ji.nga kiasi hiki. HAWEZI. Actions now, no more and the END should justify the MEANS we will use.
 
Jana wazee wa Yanga walitoa kauli kuhusu mfadhili wao kutobughudhiwa hata kidogo. Juzi mapato ya mechi ya Yanga Vs Simba yalikuwa kidogo sana mpaka wadau wote ikiwemo Serikali imestushwa na udogo wa mapato ukilinganisha na idadi ya watuwaliongia uwanjani. Kwakuwa Yanga ni taasisi ya michezo na imekuwa ikitegemea viingilio vya mlangni kuendesha timu yao tokea ianzishwe hadi juzi juzi tu ndipo timu hiyo imekuwa ni taasisi ya mtu binafsi.

Ni kwanin wazee hawa hawajatoa tamko kuhusu uchache wa mapato ya mechi timu yao inazocheza? Je kwa kushindwa kutolea tamko masuala ya michezo ambyo ndio core function ya taasisi yao na badala take wakakamua kujiingiza katika mjadakla ya ufisadi ambapo mtuhumiwa sio siri anatumia fedha nyingi kwa timu hiyo. Je wazee hawa hawajageuzwa sehemu ya ufisadi hapa nchini?

Kwa kuwa kuna wakati wazee hawa hawa walikuwa wakingaa kwenye vyombo vya habari wakimsifia Mengi kwa ufadhili wake japo mdogo, na sasa wanafadhiliwa na mtuhumiwa wetu wa ufisadi, hawafanani na mke anayechangua mume kutokana na uwezo wke kifedha (natanguliza samahani kwa kutumia mfano ambao is a bit gender sensitive)

Much respect man. Ingawa mimi ni shabiki wa Yanga siwezi kumfagilia mtu aliyefisadi pesa zetu za Mashirika ya Hifadhi. Kila mwezi tunaktwa kwenye salary halafu yeye na wezi wenzake wanaziiba Kiulaini. Hao wazee wetu wa Klabu ni njaa tu inawasumbua, na uelewa wao pia ni mdogo masikini. waliwahi kumnyenyekea Mengi wakati wa mgogoro wao hapo nyuma.
 
miaka ya nyuma mengi alikwenda yanga na mawazo ya kujitegemea akawaambia yanga iwe kampuni kama vile MANUTD, arsenal, liverpool na nyinginezo. yanga wakamfukuza wakamwambia hawataki iwe kampuni, leo hii yanga ni omba omba kwa manji.

mengi alikuwa na mawazo ya timu kuwa kampuni miaka 20 iliyopita kabla ya watu binafsi kuanza kumiliki timu...
je yanga ingekuwa kampuni miaka ile leo ingekuwa wapi???
je hii tabia ya wana yanga kuwa omba omba na kukataa kujitegemea ina tufundisha nini sisi wa TZ wote?
je hii ni tabia ya wana siasa wetu kuomba omba?
 
Back
Top Bottom