jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
Tamko la Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Tabora
Ndg wanahabari,
Waheshimiwa ndugu waandishi tunashukuru sana kwa kujitokeza siku ya leo kuja kutusikiliza, tunaomba muendelee na moyo huo kutumikia jamii kwa kutoa habari za uhakika zenye tija na taifa letu.Mungu awabariki sana kwa hilo.
Tungependa kwanza kutumia fursa hii kuwapa pole wakazi wa Jiji la Dar es salaam, hasa maeneo ya Mbagala na Maeneo yote kwa Ujumla kwa tukio la jana la milipuko ya mabomu, na kuwapa pole majeruhi wote walioathirika na tukio hilo, na pia kuwapa pole familia zote waliofiwa na ndg zao kutokana na tukio hilo, mungu azilaze pema peponi roho zao, na tunawaombea majeruhi wapone haraka.
Tuliopo hapa mbele yenu ni Mwenyekiti UVCCM Mkoa, Mjumbe wa Baraza kuu Taifa na wenyeviti wa UVCCM wa wilaya zote za mkoa wa tabora, maana yake wilaya ya tabora mjini, Nzega, Sikonge, Igunga, Urambo,na Uyui. Pia tunaye katibu wa Uhamasishaji Uvccm wa Mkoa wa Tabora. Tumekuja hapa Dar-es-Salaam tangu juzi kwa ajili ya kufuatilia maandalizi ya fundraising kwa ajili ya miradi ya vijana wa mkoa wa Tabora, na tunaomba tuwahakikishie vijana wenzetu kwamba mipango inaendelea vizuri sana, na inshaalah mungu akijalia, maandalizi yatakuwa yamekamilika wakati tunarejea Tabora.
Aidha tumeamua kuongelea kauli ya Mfanyabiashara wa IPP, Ndugu Reginald Mengi aliitisha vyombo vyake vya habari na kuanza kutukana na kuhukumu watanzania wenzake, ni kauli ambazo hazivumiliki kwa mtu aliyestaarabika kutuhumu watu kwa maslahi binafsi na anyoyafahamu mwenyewe bila kufata misingi ya sheria.
Kauli hizo licha ya kuleta harufu ya ubaguzi wa rangi pia inakuza chuki ya raia dhidi ya wenzao kwa mtazamo kuwa umasikini wao unakuzwa na kundi la watu kwa manufaa yao. Aidha linatoa taswira kuwa serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa kiwango cha kuwaruhusu baadhi ya watu kuharibu nchi, jambo ambalo lina lengo la kuigombanisha serikali na wananchi wake.
Bila kujali utawala wa sheria na haki ya msingi ya binadamu, tunaamini kila mtanzania anayo haki sawa kabisa. Tunapenda kuishukuru na kuipongeza sana Serikali kupitia Waziri wa Utawala Bora na Waziri wa Habari kwa kukemea kitendo hicho na kuendelea kusisitiza Taifa lenye utawala wa Sheria.
Kilichotusukuma sisi leo kama Vijana wa CCM wa mkoa wa Tabora ni jinsi ambavyo Ndugu Mengi alimtaja mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM - Mhe Rostam Aziz, ambaye vilevile ni Mbunge wa Igunga. Wadhifa nyigine ambazo amewahi kushika ni pamoja na Mweka Hazina wa CCM Taifa, pia kwa sasa ni Mjumbe wa NEC kupitia mkoa wetu wa Tabora na Kamanda wa UVCCM wilaya ya Igunga, maana yake ni KADA kwelikweli wa CCM na nyumbani kwao ni Mkoa wa Tabora, tukaona hili haliwezi kupita bila sisi kama vijana kuja kutetea Chama chetu. Kazi kubwa ya Umoja wa Vijana ni kutetea uhai wa CCM na Viongozi wake pale tunapo amini kuwa wanasimamia maslahi ya Taifa.
Hivi karibuni kumetokea hali ya mabadiliko ktk mfumo/tabia yetu ya kutoa mawazo kama wananchi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Ikiwa ni haki ya mtu kutoa mawazo, ni haki iliyoainishwa katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, lakini haki hiyo inapotumiwa vibaya kwa maslahi binafsi, na kwa nia ya kuwachafua wengine haki hii hugeuka kuwa vurugu na vurugu hizi zinaweza kupelekea hata machafuko kwa kupandikiza chuki miongoni mwa jamii yetu.
Ndg wanahabari, baada ya utangulizi hapo juu, sisi kama viongozi wa UVCCM wa wilaya zote na mkoa wa Tabora na kwa niaba ya UVCCM (M) Tabora, tunaomba kusema yafuatayo:
1. Tunalaani kauli kuwa Mh Rostam Aziz, kama kiongozi wetu na kamanda wa Umoja wa Vijana wilaya ya Igunga kudhalilishwa hadharani na mtu bila kuleta ushahidi wowote, tunamtaka Mzee Reginald Mengi atuombe radhi wana CCM wa mkoa wa tabora kwa kumtuhumu kiongozi wetu ambaye wananchi wake wana imani naye sanjali na wana Tabora, na amechaguliwa kidemokrasia na wananchi wengi tu. Tukiacha kauli yake bila kukemea maana yake tumekubaliana, jambo ambalo siyo kweli na kazi zake katika mkoa wa Tabora na wilaya ya igunga ni ushahidi tosha.
2. Tunalaani matamshi ya Ndugu Reginald Mengi dhidi ya Raia wenzake, na tunahoji nafasi ya ndugu Mengi kwenye jamii mpaka achukuwe nafasi ya kutuhumu, kuchunguza na kuhukumu. Raia yoyote wa Tanzania mwenye nia njema anaruhusiwa kisheria kupeleka ushahidi au kushitaki na kufungua kesi dhidi ya yeyote anayehujumu Taifa, kama kweli anayosema kwanini asiende mahakamani kuwafungulia kesi watu hawa na kuishtaki kwa maslahi ya Nchi. Tunaomba serikali kama ambavyo Mhe Mkuchika amesema, kuchunguza kauli za Ndugu Mengi na kumchukulia hatua kali zakisheria ili watu waheshimu utawala wa sheria nchini.
3. Tunahoji nafasi yake ni nini kwenye CCM? Na kwanini anatumia majukwaa ya CCM kutukana viongozi kama anavyojisikia,na kutamka kuwa wateule wa Rais ni wezi. Ndugu Mengi anayo historia ya kulumbana tena kwa kashfa na Mawaziri wengi nchini, tunamtaka aache mara moja na kama anataka siasa aingie kwenye ulingo wa siasa na tutakuna nae kwenye majukwaa ya kisiasa
4. Tunaiomba serikali iangalie upya sheria na matumizi haya mabaya ya vyombo vya habari ambayo yanaweza kuleta mtikisiko mkubwa kwenye nchi, mgawanyiko na serikali iweze kupiga marufuku tabia hii ya Bwana Mengi kutumia umaskini wa watanzania kupandikizia chuki watu wengine.
5. Tumefuatilia kwa karibu mwenendo na Ziara za Ndugu Mengi akiwa na Msafara wa Wabunge huku akitoa Misaada Mbali mbali, na tumepata taarifa kwamba anakuja katika wilaya ya Mkoa wa Tabora, Uvccm Mkoa wa Tabora inatoa Angalizo ikiwa kama misaada yake inaendana na tabia ya kutukana na kuwaundia majina mabaya viongozi wetu wa Chama, tunamuonya kama vijana wa Tabora na kamwe hatutavumilia jambo hili. Wananchi wa Tabora wana matatizo mengi, lakini vilevile wanaheshimu utu na kamwe hatuwezi kukubali matatizo yetu yatumike kudhalilishwa utu wetu na wa viongozi wetu tuliowachagua kidemokrasia.
6. UVCCM tunamuunga mkono MNEC wa Mkoa wa Tabora Mh Rostam Aziz(Mb) na kuwaambia Watanzania kuwa Mkoa wa Tabora tuna imani naye na hatuna shaka juu ya Uzalendo wake kwa Taifa hili tunafahamu anafanya biashara zake halali na hajawahi kushtakiwa na serikali kuwa amekwepa kodi zozote anazotakiwa kulipa na kwa hili uzalendo wake hauna shaka , na kumtaka asivunjike moyo, hizi ni kelele za watu wenye nia mbaya na tunamuahidi tutakuwa naye bega kwa bega katika kipindi hiki na hatutaruhusu kauli chafu dhidi ya kiongozi wetu. Tunathamini sana mchango wake wa muda mrefu kwa Chama Cha Mapinduzi na maendeleo anayohangaika nao kwa wananchi wa jimbo la igunga na mkoa wa tabora kwa ujumla.
7. Uvccm Mkoa wa Tabora, tunatoa angalizo kwa watanzania wenzetu kuwa Tusiruhusu UKABURU kutuingia kwa mtu kuja na hoja ya UBAGUZI ili kuwajengea chuki Watanzania . Tabia hii Baba wa Taifa aliwahi kuikemea na kuifananisha na ukaburu tusiruhusu makaburu kuibuka katika nchi yetu.
8. Uvccm mkoa wa Tabora, tunakemea na tunashauri Chama Cha Mapinduzi kuchukua hatua kurudisha nidhamu ndani ya chama na Serikali kwani CCM ndiyo chama tegemeo. Kwani hivi sasa kuna kashfa, malumbano ambayo hayasaidii nchi na kutoruhusu mijadala ambayo itatuyumbisha kama taifa, tabia ya aina hii si jambo zuri bali ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu.
9. Mwisho tunapenda kuwahakikishia wanahabari na watanzania kwa ujumla Uvccm mkoa wa tabora tunamuunga mkono MNEC wetu na hatuko tayari kuona anadhalilishwa bila kuwa ushahidi wa jambo lolote na imani serikali haitaruhusu tabia ya watu kujitafutia umaarufu kwa Gharama za kuchafua wengine.
10. Uvccm Mkoa tunatoa angalizo kwa Wabunge wa Majimbo yote ya mkoa wa Tabora ,na wa viti maalum kuwa wakasimamie utekelezaji wa Ilani ya CCM kama walivyoahidi kwa wapiga kura, pia tunatoa wito kwa wabunge wa Mkoa wetu wanaoambatana na Misafara ya Bwana Mengi wajiepushe na misafara inayokashifu na kuita majina mabaya viongozi wetu na wao kuwa sehemu ya jambo hilo wakishangilia. Kwa kuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP ana Tabia ya kutumia majukwaa ya CCM na kukashifu watendaji wakuu wa serikali na wakati huo huo kumsifia Rais kwani huwezi kumsifia Rais wakati unakashifu na kuwaita watendaji wake wa chama na Serikali kuwa ni Mafisadi na hawamsaidii Rais kimantiki ni kwamba anakosoa uteuzi wa Rais na kuonyesha kuwa unamapungufu. Vijana hatutakuwa tayari kubeba wabunge 2010 wanaoshiriki katika ziara ambazo zinakichafua chama na serekali kupitia kivuli cha kusaidia wanyonge.
11. Tunasisitiza tunalaani kauli ya Mengi na tunaomba serekali itekeleze alichosema Mh Mkuchika.
AHSANTENI SANA, MUNGU AWABARIKI
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Naona 400 milions zinafanya kazi yake,ukiwa na pesa burdani kweli,ukiwa na pesa kama Somaiya,aah,hakuna shida....Watanzania wajue ccm imenunuliwa,na kama na wao wamo ndani ya kapu haya,tufanyeje sasa,maana JK mwenyewe kimyaa!
Yani ni shida kujuwa yuko upande gani,naona shida iko kwenye hao watano waliobaki ambao Mengi hajawataja,ila kutajwa kwa kina Subash Patel ni sawa na kutajwa kwa JK mwenyewe hilo liko wazi,na kwahiyo JK amewekwa kwenye mtego ambao hawezi kujinasua kwani maji moto ni unga tu unahitajika ugali uliwe.
R.E Mengi si mjinga kama wapambe wa mafisadi wanavyofikiri.
Shukran kwa R.E Mengi kwa kujitolea kwa ajili ya Taifa letu na kuazisha chachu kwa watanzania,chachu ya ukombozi,time is running out,na kutokana na pressure iliyopo, explosion lazima itokee ili taifa letu listawi.