Mwizi maarufu wa Kawe/Mbezi Beach 'Minyembe' auawa na Wananchi

Mwizi maarufu wa Kawe/Mbezi Beach 'Minyembe' auawa na Wananchi

Pdidy

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2007
Posts
57,951
Reaction score
32,619
Kijana aliekuwa maarufu kupiga watu visu na mapanga na kuleta wezi wa Manzese na Magomeni kuwatesa wananchi wa Kawe na Mbezi ameuwawa usiku huu

Kijana Minyembe kijana mwembamba na mwemye mbio kuliko mwanariadha Bolt ameuawa usiku huu baada ya kumuibia dada mmoja njia ya mchangani chadema

Kama wasemavyo siku ya kifo n kifo tu Minyembe alikuwa na wenzie wawili. Ghafla walipokimbia yule binti akapiga kelele wananchi wakamfwata aliekimbilia mtoni Kawe

Alipoanza kukimbizwa kwenye maji akaomba asamehewe arudii tena ana mtoto, wakamshauri apande juu. Hapo ndipo wakamfunga kamba pembeni ya nyumba ya mjumbe. Wakanzaa mdundika mawe yasio na idadi kichwani

Kijana Minyembe ambae Kawe polisi pamekuwa kama shule yake akiingia na kutoka hivi sasa hatuko nae tena. Polisi wa Kawe mtusaidie kutoa hii maiti yake ulizeni kwa mjumbe

Nendeni bar ya Soweto mtaelekezwa alipo.

RIP Minyembe umewahi kunisachi kama mwanamke mara nne tena saa tano tu nashukuru hukuwahi kunidhuru ingawa nilijitahdi kukupa ushirikiano kila nikuonapo

Ulinifanya nikirudi saa sita niweke simu na pochi kwenye soksi huku nikikuwekea 2000-3000 kwa ajili ya kuweka amani nifike salama nyumbani

RIP
Dk Minyembe
 
Back
Top Bottom