Mwl. Mwakasege: Nilienda Mbinguni nikaongea na Yesu na Musa

Mwl. Mwakasege: Nilienda Mbinguni nikaongea na Yesu na Musa

Katika mtu ninayemuheshimu humunJF ni pamoja na wewe ila hiki ulichoandika, inawezekana uliandika ukiwa umelewa maana hata wewe ukitulia na kusoma, sidhani kama utakielewa.
Huwezi kuelewa kwa sababu akili yako umeifunga. Panua akili yako mkuu. Utaelewa tu
 
Wadau kwema?

Nipo hapa nafuatilia Semina ya Neno la Mungu - Dodoma mubashara kabisa kupitia Upendo TV (Huduma ya Mana)

Mwalimu Mwakasege naye anasema eti eti alienda Mbinguni akakutana na Musa, na pia akakutana na Yesu na akapiga nao story. Na kasema eti Yesu kamwambia yuko njiani anarudi.

Dah! Hii kitu imekaaje wadau?

Alianza Nabii Mkuu Geordavie then Zumaridi na sasa Mwl. Mwakasege.

Mbinguni hiyo vipi wadau, mbona sielewi mapichapicha haya!!!

Mbinguni dah! Aloo mbinguni!!!

(Mmh!..hahahaha ...mhhh!...hahaha) Twibhwa nabazenganwa! Ehenao yaya gete....bagoshaaaaa!!!! Alichene!
!View attachment 2593179
Afadhali hata huyo.Zumaridi alidai alitongozwa na mtume petro akakataa.
 
Enzi zile za kale Mungu hakuwahi kumkaribisha binadamu wa nyama na damu Mbinguni ,aliongea na Abramu huku duniani,aliongea na kipenzi chale Musa huku duniani,aliongea na manabii wengi huku duniani.hata wakati wa Yesu Kristi hakuwahi kwenda Mbinguni kabla kufufuka kwake .Yohane alifunuliwa TU mambo ya Mbinguni,siku ukajiona uko Mbinguni au ukaona USO wa Mungu ujue umelala na hauwezi kurudi duniani ukiwa na mwili wa nyama na damu.Ni waongo.
 
Mtume alitoka msikiti mtakatifu wa Makkah Hadi msikiti mtakatifu wa Jerusalem, Quran ipo hadhiri na Hilo,hayo ya kwenda mbinguni mnajua mmetoa kwa Mungu gani
Yani wewe ni mwislam lakini hujui safari ya isra.hujielewi
 
Hakumuuliza sababu ya kifo cha mwanae kwa kuachwa kimapenzi.au karidhika na dada wa pilot
 
Yani wewe ni mwislam lakini hujui safari ya isra.hujielewi
Safari ya kwenda mbinguni ni uwongo, kwenye Qur'an haipo,ni uzushi wa watu Kama kawaida yao,yaani mtume aende mbinguni na kurudi Qur'an isiseme!?
 
Wadau kwema?

Nipo hapa nafuatilia Semina ya Neno la Mungu - Dodoma mubashara kabisa kupitia Upendo TV (Huduma ya Mana)

Mwalimu Mwakasege naye anasema eti eti alienda Mbinguni akakutana na Musa, na pia akakutana na Yesu na akapiga nao story. Na kasema eti Yesu kamwambia yuko njiani anarudi.

Dah! Hii kitu imekaaje wadau?

Alianza Nabii Mkuu Geordavie then Zumaridi na sasa Mwl. Mwakasege.

Mbinguni hiyo vipi wadau, mbona sielewi mapichapicha haya!!!

Mbinguni dah! Aloo mbinguni!!!

(Mmh!..hahahaha ...mhhh!...hahaha) Twibhwa nabazenganwa! Ehenao yaya gete....bagoshaaaaa!!!! Alichene!
!View attachment 2593179
Kama magwiji wa kichawi wanaweza kwenda kuzimu kuonana na Shetani na kufanya naye mazungumzo, basi si ajabu na watu wa Mungu waliozama rohoni kwenda Mbinguni na kuonana na walio huko na kufanya nao mazungumzo. Muhimu tu ujue kuwa hawaendi na miili yao ya damu na nyama, bali miili yao ya kiroho.

Ni roho zao ndizo zinazoenda, na siyo miili yao ya kawaida.

Kwa watu wanaotembea kwa ukaribu sana na Mungu, kuna mambo wanayoyafahamu ambayo wakiwashirikisha watu wa kawaida hawawezi kuwaelewa. Ndiyo maana wengi wa waliofikia hatua hiyo huamua kujinyamazia kwa sababu akisema hataeleweka, sana sana, wengine wanaweza wakawafikiria ndivyo sivyo.

Hakuna la ajabu kwa Mwakasege kushuhudia kuwa alishawahi kufika Mbinguni na kuonana na Musa. Wapo na watumishi wengine wengi tu, walio "genuine", wenye shuhuda zinazoendanan na ushuhuda wa Mwakasege.

Kwa watoto wa Mungu, Mbinguni si ugenini, ni kwa baba yao. Si ajabu kwa watoto kupatembelea kwao wangali bado wanaishi ugenini.

Kwani haukusikia ushuhuda wa Jenerali David Msuya, jinsi alivyokufa na siku ya nne akafufuka, wakati huo maandalizi ya mazishi yake yakiwa yameshaanza?

Nafikiri alifia nchini Uingereza, alikokuwa ameplekwa na Serikali kutibiwa. Alishuhudia kuwa alipokufa, alikutana na Yesu na akamwambia kuwa hakuwa ameifanya kazi aliyokuwa amemtaka aifanye angali hai, kwa hiyo akamwamuru arudi duniani. Ni baada ya agizo hilo ndipo Jenerali Msuya alipofufuka, akiwa mzima wa afya.

Usishangazwe na huo ushuhuda. Mungu hana mipaka, ni zaidi ya uwezo wako wa kufikiri. Kama anaweza kusababisha punda kuongea kama mtu, kama anaweza kusababisha fimbo kavu kuota na kutoa matunda ndani ya masaa ishirini na nne, kama anaweza kumhamisha mtu kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine, tena ya mbali, kwa "sekunde", usishangazwe unaposikia shuhuda wa watu waliowahi kwenda Mbinguni wangali hai.

Ingawa kuna shuhuda za "kubumba", lakini si kila ushuhuda ni wa kubumba.

Kwa hiyo , si kosa kuuchunguza kabla ya kufanya maamuzi ya kuukubali au kuukataa.
 
Back
Top Bottom