TANZIA Mwl. Ndosi aliyefundisha Shule ya Msingi Muhimbili afariki dunia

TANZIA Mwl. Ndosi aliyefundisha Shule ya Msingi Muhimbili afariki dunia

Angekuwepo leo asingeweza kufanya kazi...

Angepangiwa viboko vya kupiga na watu wangemuita mdhalilishaji na hata kufunguliwa kesi...; No wonder kizazi kijacho kinaweza kikawa mayai..., hizi pilikapilika za kukimbia viboko na ku-dodge matusi ndio preparation tosha ya maisha..., sababu viboko vya kitaa ni hatari maradufu.... (Political Correctness na watu kuingilia kazi za watu kumezidi)

RIP Mwalimu ingawa sikuwahi kupita anga zako.....

Now Your Walk has Ended - We Shall Never See the Likes of You Again - Especially in this Day and Age
 
Ndosi: Kama wewe ni mtoto wa ticha, mimi ndiye ticha sasa.

Wanafunzi wasio watoto wa walimu: Weeeeeeeeeeeeeeeee.

Wanafunzi walimfurahia Ndosi kwa kuondoa matabaka kati ya wanafunzi wenye nasaba na walimu, na wanafunzi wengine.

That was the positive side of Ndosi.

Ila usiombe akupige fimbo za mgongo.

Siku moja nilimpiga mtoto mmoja Muarabu alinizingua. Akaenda kunisemea kwa Ndosi.

Sasa Ndosi akawa na kazi nyingi akawa kanisahau.

Siku hiyo bahati haikuwa yangu. Akaja Shangazi yangu alikuwa mkaguzi wa shule wa wilaya or something like that, akamwambia Ndosi kuna huyu kijana wangu Kiranga niangalizie. Ndosi akasema Kiranga gani, huyu mtundu anafanya fujo sana, tena umenikumbusha nina kesi yake hapa kuna mtu kampiga leo hii hii.

Akatuma mtu kuniita darasani.

Nilipata fito juu ya fito, tena zile za kutaka sifa mbele ya shangazi yangu.

Kuanzia hapo Ndosi kila akiniona akawa ananjua mimi simpendi.
 
Jamani zamani kulikuwa Kuna walimu miamba hasa !! Aisee nakumbuka Mr Ngoliga Dodoma mlimani primary school ,Mipilimi Makole primary daaa
 
Angekuwepo leo asingeweza kufanya kazi...

Angepangiwa viboko vya kupiga na watu wangemuita mdhalilishaji na hata kufunguliwa kesi...; No wonder kizazi kijacho kinaweza kikawa mayai..., hizi pilikapilika za kukimbia viboko na ku-dodge matusi ndio preparation tosha ya maisha..., sababu viboko vya kitaa ni hatari maradufu.... (Political Correctness na watu kuingilia kazi za watu kumezidi)

RIP Mwalimu ingawa sikuwahi kupita anga zako.....

Now Your Walk has Ended - We Shall Never See the Likes of You Again - Especially in this Day and Age
Hao ambao walilelewa kwa viboko bila umayai wamelifikisha wapi taifa? Si ndiyo wameishia kuwa wezi wa mali za umma. Maana wao hawafanyi kitu sahihi ila mpaka kiwepo kitisho cha adhabu. Wakijua hawawezi kufanywa kitu wanafanya fujo zote.
 
"MWAMBA" MWALIMU NDOSI KENDE MALAMU!

"Mwalimu Ndosi alikuwa mwalimu wa hesabu. Alikuwa si mchezo. Alikuwa akikohoa tu wanafunzi wote mnakufa"
.
Bi JOYCE, Aprili 18, 2023

1. Wiki iliyopita, wanafunzi waliofundishwa na MWALIMU NDOSI, Mwalimu pale Muhimbili Shule ya Msingi, walimwambia "Mzee wa Atikali" aandae "Atikali" ya MWALIMU NDOSI na wao watadhamini Mtanange.

2. Leo, "Mzee wa Atikali" amejuzwa kuwa MWALIMU NDOSI ameaga dunia asubuhi hii.

3.MWALIMU NDOSI ni mmoja wa waalimu bora kabisa wa shule za msingi kuwahi kutokea.

4. MWALIMU NDOSI alikuwa Mwalimu wa Hisabati. Hili ni somo ambalo "Bongolanderz" wengi huliogopa. Hapo ndo kimbembe kilipoanzia. Kutokana na uwezo wake mkubwa wa Hisabati alikuwa akifundisha "Tuition". Wanafunzi wa kutoka shule mbalimbali za Dsm walifurika kwake kujifunza Hisabati na mboko ilikuwa kama Kawa.

MWALIMU NDOSI alikuwa na staili kabambe ya kutembeza mboko; alikuwa anakuingiza kichwa ndani ya benchi afu makalio yanakuwa juu afu hapo mijeledi ndo inaanza. Ilikuwa si mchezo, mwanawane!

4.MWALIMU NDOSI alikuwa na uwezo mkubwa na alikuwa mkali na aliwatia adabu sana wanafunzi wa kishua wa shule ya Muhimbili. Alikuwa anatembeza mboko bakoraa si za kitoto! Siku akiwa zamu alipenda kuvaa jeans & t-shirt. Ukiona kavaa hivyo ujue mboko wiki hiyo zitatembea mwanzo-mwisho!

5. MWALIMU NDOSI alikuwa si tu anatembeza mboko bali alikuwa anatukana sana matusi. Ungeweza kufikiri ni Kuli wa bandarini. Matusi yake makubwa yakikuwa "Crocodile- nyoko, Ushuzi wa Mungu". Kwa hakika, MWALIMU NDOSI alikuwa si mtu wa "Spoti-Spoti"!

5. MWALIMU NDOSI amewafundisha wanafunzi wengi ambao wamekuja kuwa viongozi kwenye Taifa hili wakiwemo Mawaziri na Mabalozi.

PUMZIKA KWA AMANI, MWAMBA MWALIMU NDOSI

View attachment 2591988
Kweli ushuzi wa Mungu

Ahhahaaaaa
 
Ndosi: Kama wewe ni mtoto wa ticha, mimi ndiye ticha sasa.

Wanafunzi wasio watoto wa walimu: Weeeeeeeeeeeeeeeee.

Wanafunzi walimfurahia Ndosi kwa kuondoa matabaka kati ya wanafunzi wenye nasaba na walimu, na wanafunzi wengine.

That was the positive side of Ndosi.

Ila usiombe akupige fimbo za mgongo.

Siku moja nilimpiga mtoto mmoja Muarabu alinizingua. Akaenda kunisemea kwa Ndosi.

Sasa Ndosi akawa na kazi nyingi akawa kanisahau.

Siku hiyo bahati haikuwa yangu. Akaja Shangazi yangu alikuwa mkaguzi wa shule wa wilaya or something like that, akamwambia Ndosi kuna huyu kijana wangu Kiranga niangalizie. Ndosi akasema Kiranga gani, huyu mtundu anafanya fujo sana, tena umenikumbusha nina kesi yake hapa kuna mtu kampiga leo hii hii.

Akatuma mtu kuniita darasani.

Nilipata fito juu ya fito, tena zile za kutaka sifa mbele ya shangazi yangu.

Kuanzia hapo Ndosi kila akiniona akawa ananjua mimi simpendi.
Aahaaaaaa

Kumbe mna historia ndefu ya pamoja
 
Kuna video yake nadhani ipo ya namna mwalimu ndosi anapofundisha huwa hapendi disturbances [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom