"MWAMBA" MWALIMU NDOSI KENDE MALAMU!
"Mwalimu Ndosi alikuwa mwalimu wa hesabu. Alikuwa si mchezo. Alikuwa akikohoa tu wanafunzi wote mnakufa".
Bi JOYCE, Aprili 18, 2023
1. Wiki iliyopita, wanafunzi waliofundishwa na
MWALIMU NDOSI, Mwalimu pale Muhimbili Shule ya Msingi, walimwambia
"Mzee wa Atikali" aandae
"Atikali" ya
MWALIMU NDOSI na wao watadhamini Mtanange.
2. Leo,
"Mzee wa Atikali" amejuzwa kuwa
MWALIMU NDOSI ameaga dunia asubuhi hii.
3.
MWALIMU NDOSI ni mmoja wa waalimu bora kabisa wa shule za msingi kuwahi kutokea.
4.
MWALIMU NDOSI alikuwa Mwalimu wa Hisabati. Hili ni somo ambalo
"Bongolanderz" wengi huliogopa. Hapo ndo kimbembe kilipoanzia. Kutokana na uwezo wake mkubwa wa Hisabati alikuwa akifundisha
"Tuition". Wanafunzi wa kutoka shule mbalimbali za Dsm walifurika kwake kujifunza Hisabati na mboko ilikuwa kama Kawa.
MWALIMU NDOSI alikuwa na staili kabambe ya
kutembeza mboko; alikuwa anakuingiza kichwa ndani ya benchi afu makalio yanakuwa juu afu hapo mijeledi ndo inaanza. Ilikuwa si mchezo,
mwanawane!
4.
MWALIMU NDOSI alikuwa na uwezo mkubwa na alikuwa mkali na aliwatia adabu sana
wanafunzi wa kishua wa shule ya Muhimbili. Alikuwa anatembeza
mboko bakoraa si za kitoto! Siku akiwa zamu alipenda kuvaa jeans & t-shirt. Ukiona kavaa hivyo ujue mboko wiki hiyo zitatembea mwanzo-mwisho!
5.
MWALIMU NDOSI alikuwa si tu
anatembeza mboko bali alikuwa anatukana sana matusi. Ungeweza kufikiri ni Kuli wa bandarini. Matusi yake makubwa yakikuwa
"Crocodile- nyoko, Ushuzi wa Mungu". Kwa hakika,
MWALIMU NDOSI alikuwa si mtu wa
"Spoti-Spoti"!
5.
MWALIMU NDOSI amewafundisha wanafunzi wengi ambao wamekuja kuwa viongozi kwenye Taifa hili wakiwemo Mawaziri na Mabalozi.
PUMZIKA KWA AMANI, MWAMBA MWALIMU NDOSI
View attachment 2591988