TANZIA Mwl. Ndosi aliyefundisha Shule ya Msingi Muhimbili afariki dunia

TANZIA Mwl. Ndosi aliyefundisha Shule ya Msingi Muhimbili afariki dunia

"MWAMBA" MWALIMU NDOSI KENDE MALAMU!

"Mwalimu Ndosi alikuwa mwalimu wa hesabu. Alikuwa si mchezo. Alikuwa akikohoa tu wanafunzi wote mnakufa"
.
Bi JOYCE, Aprili 18, 2023

1. Wiki iliyopita, wanafunzi waliofundishwa na MWALIMU NDOSI, Mwalimu pale Muhimbili Shule ya Msingi, walimwambia "Mzee wa Atikali" aandae "Atikali" ya MWALIMU NDOSI na wao watadhamini Mtanange.

2. Leo, "Mzee wa Atikali" amejuzwa kuwa MWALIMU NDOSI ameaga dunia asubuhi hii.

3.MWALIMU NDOSI ni mmoja wa waalimu bora kabisa wa shule za msingi kuwahi kutokea.

4. MWALIMU NDOSI alikuwa Mwalimu wa Hisabati. Hili ni somo ambalo "Bongolanderz" wengi huliogopa. Hapo ndo kimbembe kilipoanzia. Kutokana na uwezo wake mkubwa wa Hisabati alikuwa akifundisha "Tuition". Wanafunzi wa kutoka shule mbalimbali za Dsm walifurika kwake kujifunza Hisabati na mboko ilikuwa kama Kawa.

MWALIMU NDOSI alikuwa na staili kabambe ya kutembeza mboko; alikuwa anakuingiza kichwa ndani ya benchi afu makalio yanakuwa juu afu hapo mijeledi ndo inaanza. Ilikuwa si mchezo, mwanawane!

4.MWALIMU NDOSI alikuwa na uwezo mkubwa na alikuwa mkali na aliwatia adabu sana wanafunzi wa kishua wa shule ya Muhimbili. Alikuwa anatembeza mboko bakoraa si za kitoto! Siku akiwa zamu alipenda kuvaa jeans & t-shirt. Ukiona kavaa hivyo ujue mboko wiki hiyo zitatembea mwanzo-mwisho!

5. MWALIMU NDOSI alikuwa si tu anatembeza mboko bali alikuwa anatukana sana matusi. Ungeweza kufikiri ni Kuli wa bandarini. Matusi yake makubwa yakikuwa "Crocodile- nyoko, Ushuzi wa Mungu". Kwa hakika, MWALIMU NDOSI alikuwa si mtu wa "Spoti-Spoti"!

5. MWALIMU NDOSI amewafundisha wanafunzi wengi ambao wamekuja kuwa viongozi kwenye Taifa hili wakiwemo Mawaziri na Mabalozi.

PUMZIKA KWA AMANI, MWAMBA MWALIMU NDOSI

View attachment 2591988
Dah nimesoma muhimbili wakati wake, ila nashukuru sikuwahi kuzipata bakora zake. R.I.P mwalimu.
 
Alikuwa mwalimu wangu wa darasa, mwaka mzima kaingia darasani kama mara tatu tu hivi.

Watu walikuwa wanajaa tuition yake, yale aliyotakiwa kufundisha darasani, alikuwa anafundisha tuition.

Basi tu jamii yetu hatuko critical na mtu akifa hatupendi kusema mabaya yake.
Wewe itakuwa ulisoma darasa la 7A maana ndio lilikuwa darasa lake pale muhimbili. Nilikuwa namuogopa balaa
 
Ndosi alikuwa mfano wa failure katika mfumo wa elimu wa Tanzania.

Systemic failure.

Sasa mbona ume pay him tribute na kuchapisha matusi yake kwa watoto na ku reminisce kuhusu "so many stories'' zake, na kumtakia mema alikokwenda baada ya kufariki ?

Tanzania hatunaga skendo, jitu chafu chafu huwa haliwi condemned, disgraced and discredited, bado linakuwa maarufu na kupendwa kwa uchafu chafu huo huo.
 
Sasa mbona ume pay him tribute na kuchapisha matusi yake kwa watoto na ku reminisce kuhusu "so many stories' zake na kumtakia mema alikokwenda ?

Tanzania hatunaga skendo yani, jitu chafu chafu haliwi condemned, disgraced and discredited, bado linakuwa maarufu na kupendwa kwa uchafu chafu huo huo.
Hakuna mtu mbaya kabisa, hakuna mtu mzuri kabisa.

Hii idea ya kwamba mtu fulani ni mbaya tu, au mzuri tu ni fiction.

Nimeeleza uzuri wake pia kama alivyoweka usawa kwa wanafunzi wote na kuondoa matabaka ya wanafunzi watoto wa walimu na wanafunzi wengine.

“The line separating good and evil passes not through states, nor between classes, nor between political parties either – but right through every human heart…even within hearts overwhelmed by evil, one small bridgehead of good is retained. And even in the best of all hearts, there remains…an uprooted small corner of evil.​

-Aleksandr Solzhenitsyn, Russian Nobel Laureate in Literature, 1970.
 
Alisifika zaidi kwa kuwatia watoto discipline.

Hiyo sio sifa kwa Mwl. Ndosi.

Hujui kama watoto waliobamizwa walikuwa hawana discipline. Na ambao walikuwa hawana discipline hujui kama mafimbo na matusi yaliwasaidia. Hiyo "sifa ya kuwapa watoto discipline" walimpa watoto, wewe sasa ni mtu mzima, sitegemei mtazamo wako ushabihiane na ule wa ulipokuwa mtoto wa msingi.

Mjomba anaejulikana mtaani kwa ukali na kubamiza watoto ovyo ovyo huwezi kumpa outright accolades kwamba ana sifa ya kuwawatia watoto discipline. Inawezekana ni child abuser tu. Discipline gani ya kuwafundisha watoto kutukana "ushuzi wa Mungu," wakati kwenye Madrassa na Sunday School wanafundishwa kumcha Mungu ndio msingi wa wema, upendo na kuheshimiana ?

Mwl. Ndosi na sifa za kupiga na kutukana watoto amepeta nazo kwenye jamii isiyo na utamaduni wa professional and social accountability, wala critical thinking. Hatunaga skendo, wala udadavuzi wa mambo.
 
Unaelewa maana ya neno sifa?
 
Yeye alikuwa mfano wa failure katika mfumo wa elimu Tanzania.

Mwalimu haingii darasani, anafundisha tuition yake tu, anatukana wanafunzi "msenge baridi" halafu hafanywi kitu.

Kulikuwa hakuna oversight.
Umenikumbusha F.M MANANE kichwa Cha hesabu Huyu ticha,
Alikua ana tu fevor sana wanafunzi tulio soma Tution kwake......

Katika UMRI wangu huu wa kukimbiza sungura....
Today for the first time ever....NDIO nasikia haya matusi ya mwalimu ndosi ni mapya masikioni mwangu.....🤣🤣🤣😂😂

R.I.P Teacher ndosi
 
Shule niliyosoma Mimi kulikuwa na mwalimu anaitwa NgoloNgolo alikuwa anazitembeza stick hatari.

Na alikuwa mwamba wa hesabu kweli kweli.
 
Umenikumbusha F.M MANANE kichwa Cha hesabu Huyu ticha,
Alikua ana tu fevor sana wanafunzi tulio soma Tution kwake......

Katika UMRI wangu huu wa kukimbiza sungura....
Today for the first time ever....NDIO nasikia haya matusi ya mwalimu ndosi ni mapya masikioni mwangu.....🤣🤣🤣😂😂

R.I.P Teacher ndosi
Inategeea ulipita hapo mwaka gani, pengine alivyozeeka aliacha.
 
Ndosi alikuwa mfano wa failure katika mfumo wa elimu wa Tanzania.

Systemic failure.
Imagine ...
Walikuwa Kaka wa 3...
Muhimbili, Upanga, na Zanaki primary school..
Wote walikuwa na same profile....yaani bakora za kutosha....
 
sikuwahi kumfahamu enzi za ujana
mi
ungesema mwl kondo ewaaaa
 
Hao ambao walilelewa kwa viboko bila umayai wamelifikisha wapi taifa? Si ndiyo wameishia kuwa wezi wa mali za umma. Maana wao hawafanyi kitu sahihi ila mpaka kiwepo kitisho cha adhabu. Wakijua hawawezi kufanywa kitu wanafanya fujo zote.
Umenena maneno ya maana na ya kutafakarisha
 
Back
Top Bottom