TANZIA Mwl. Ndosi aliyefundisha Shule ya Msingi Muhimbili afariki dunia

Yeye alikuwa mfano wa failure katika mfumo wa elimu Tanzania.

Mwalimu haingii darasani, anafundisha tuition yake tu, anatukana wanafunzi "msenge baridi" halafu hafanywi kitu.

Kulikuwa hakuna oversight.
Hapo nimekusoma
 
Vipi lakini,alikuwa competent kwenye somo lake!?
 
Alikuwa vizuri, hesabu za Primary. Alisifika zaidi kwa kuwatia watoto discipline.

Watu wanaweza kuwa wanapiga kelele, Ndosi akitokea nje anatembea tu kimyaa.
Aaaahajajaa

Basi apumzike mahala pema
 
Nakumbuka miaka hio kuna jamaa yangu wa kuitwa sudi tulivo fika darasa la sita alikacha kuja shule kama miez kazaaa kwa kuogopa ukali wa mwalimu ndosi.
 
We ulimaliza mwaka gan pale muhimbili primary school????
 
Hao ambao walilelewa kwa viboko bila umayai wamelifikisha wapi taifa? Si ndiyo wameishia kuwa wezi wa mali za umma. Maana wao hawafanyi kitu sahihi ila mpaka kiwepo kitisho cha adhabu. Wakijua hawawezi kufanywa kitu wanafanya fujo zote.
You Miss the Point.....

Sijasema Watu wapigwe nimesema Mwalimu aachiwe mandate ya kufundisha hayo sijui ya kumtunza mtoto mpaka mwalimu mkuu ndio anamchapa ni kupangia shule kazi; hata zamani kulikuwa na choices, Peleka mtoto kule unapoona panafaa kwako, kama sehemu fulani wanalima sana peleka ambapo hawalimi, sio kuwaambia shule fulani waache kulima....

Kuhusu wizi unadhani unafundishwa shule ? Hio ni Jamii nzima, zamani ukimpelekea zawadi mzazi wako ya vitu beyond your means anakuuliza umevitoa wapi, ukila mali ya UMMA hadi watoto wako shule wanaona aibu baba yao mwizi..., leo hii ukiwa mbunge usipobadilika ghafla hata mzazi wako anakushangaa kwamba kwanini mwenzako ana ghorofa nne kwamba ule ndio ujanja kumbe ni wizi tu....;

Kwahio hii has nothing to do with schooling au uzalendo bali wizi umehalalishwa..., umimi umekuwa the norm..., and since its a rat race hata mtu aibe kiasi gani hawezi kuridhika and it will get worse mpaka mwisho wake kila mwenye nacho anakuwa branded mwizi (wasionacho watakapozidi wizi hautaonekana ujanja tena bali kama ukoma - and by then it will be too late, a higher price will have to be paid to return things to normality)
 
Huyu mzee alinifundisha (briefly) Upanga Primary. Wakati niko Std 7 katikati ya mwaka hivi, alihamishiwa hapo Upanga primary. Walihamishiwa kwa pamoja hapo yeye na Mwalimu mwingine aliitwa Salum. Salum alihamishiwa kama mwalimu mkuu, na yeye Ndosi kama mwalimu wa hesabu. Wote walikua wanatokea Muhimbili Primary, na walionekana kuwa ni marafiki pia. Aisee jamaa alikua sio wa kispoti spoti. Aliwahi kunipiga mbata moja kichwani siwezi lisahau, niliona maluweluwe kwa dakika kadhaa.
Alivyohamia pale shuleni, ujio wake ulitingisha sana. Alikua anachapa balaa kabisa. Akaanzisha speed tests za hesabu za asubuhi kwa darasa la saba. Maswali 25 ndani ya lisaa limoja, ukikosa tu hesabu hata moja unachezea mboko balaa, tulizichezea sana stiki zake ile mwisho mwisho. Jamaa alikua na matusi balaa, moja la tusi lake pendwa lilikua, "Seng.e la mungu wewe". Ila jamaa alikua anapenda sana hesabu.
May his soul RIP.
 
mwalim ndosi, ana mtoto maarufu anaitwa carol
 
May his soul rest in eternal peaceπŸ™
Alikua anatunyoosha vema
Leo nimejua Kumbe wewe ni wa kishua. Huku mtaani tunawaita kuku wa kizungu,maana hamkupata shida.

Watoto waliosoma muhimbili,oysterbey na shule za pande zile ni washua.

R.I.P Mwalimu.
 
Leo nimejua Kumbe wewe ni wa kishua. Huku mtaani tunawaita kuku wa kizungu,maana hamkupata shida.

Watoto waliosoma muhimbili,oysterbey na shule za pande zile ni washua.

R.I.P Mwalimu.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
Mimi wa uswazi pro max
 
R.I.P mzee wetu! Nilionana nae kama miaka 3 iliyopita kuna jamaa aliniunganisha nae alikuwa na changamoto ya Kisukari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…