Mwl. Nyerere aliitabiria mema CHADEMA, Ndugai na Bashiru msihuzunike

Mwl. Nyerere aliitabiria mema CHADEMA, Ndugai na Bashiru msihuzunike

Ndugai na Bashiru ,Polepole wanakubalika ile mbaya huku mtaani
Wameachana na agenda zao baada ya kupewa vibuyu vya asali. Nyerere aliwaachia maadui wa taifa tofauti na adui wanaemjadili kwenye vikao vyao. Mwl amewaachia maadui wa ujinga, umaskini, maradhi, ukabika, udini na rushwa lakini wao wanamhubiri adui mmoja TU ambae ni watanzania wenzao ambao wako kwenye vyama vya siasa vya upinzani.
 
Kwetu sisi tunaamini kuwa watu hawafi bali wanageuka kuwa kitu kingine bora na chenye nguvu zaidi kuliko walivyokuwa. Makosa makubwa ya Rais Ben Mkapa yaliyomkasirisha Mwl kule aliko sasa ni kuyauza mashirika yake ya umma na kuwaita wapinzani malofa. Kuita wapinzani malofa ni sawa na kumuita Mwl lofa pia, maana Mwl alichangia sana kuvileta vyama vya upinzani. Hivyo hasira ya Mwl juu yake haiwezi ndogo.

Rais Kikwete yeye amepata baraka zote za Mwl na ndiyo maana yuko kama alivyo sasa. Huyu jamaa alitii maagizo ya mwl ya kuvilea vyama vya siasa, chadema na cuf vilinawili wakati wa JK, amepata baraka zote za Mwl kwa kutimiza hili.

Kosa la Rais JPM ilikuwa kuvinyonga kabisa vyama vya upinzani nchi visiwepo kabisaaa. Jambo hili halikubaliki kwa Mwl kabisa na hawezi kukusamehe uishi, hasira yake kwake ingekuwa kubwa kabisa kwakuwa unataka kumkosoa kwa kuvileta vyama vingi. Mwl aliitaka CCM ivillee vyama vya siasa vya upinzani hadi viwe na uzoevu, vikubwa na vichache ili vimudu kupokezana na CCM katika kuiongoza nchi, badala yake JPM alitaka kuviua kinyume na maagizo ya Mwl ambayo iliiagiza CCM hadharani mchana kweupe.

Hebu msikilizeni Mwl alichowaagiza CCM kuhusu vyama vya siasa vya upinzani


Rais Samia lazima nae awe makini kuhusu agizo hili la baba wa taifa kwa CCM.
Nyerere alikuwa na akili za ziada sana zilizochanganyika na unabii, alijua kuwa ndani ya CCM watu wenye mawazo mbadala na watawala hawatasikilizwa wala kukubalika hata kama wana mawazo mazuri, alijua pia watu wenye mawazo mbadala hawaruhusiwa kusajili chama kikapitishwa, ndio maana alitaka vyama vya upinzani viwepo.
 
Hizi shangwe sio za bure,
View attachment 2446449

Mkutano Mkuu wa CCM umekwisha, mengi tumeyaona na mengi tumeyasikia. Sasa tunafahamu ni nani kasema nini na nani anataka nini.

Tumejitoa ufahamu watanzania wote kukubali kuogopa kuiadhibu CCM hata kama inafanya makosa tusiyoyataka. CCM imegeuka Mungumtu, hakuna anaeihoji akabaki kuwa na amani yake, atabezwa na kudhihakiwa. Kila mtu na kila kundi linaitumia CCM kama kichaka TU kufanikisha kile anachokikusudia kukitekeleza hata kama kiwe kinaiumiza Tanganyika, Zanzibar au Tanzania yote na watu wake.

Hata wenye akili timamu wanageuka kuwa wendawazimu wakifika kwenye vikao vya CCM, wanazisahau na kuzidharau agenda zao ndani ya vikao vya CCM, wanabaki wanakenua tu wapende wasipende.
Ndani ya vikao vya CCM mashetani wanageuka malaika na malaika wanageuka mashetani kwa kutumia silaha ya kudumisha umoja ndani ya CCM na kutesa kwa zamu na kulamba asali kwa zamu kwa kuwaamina wajumbe wote wa mkutano kuwa adui Yao namba moja ni watanzania wenzao ambao wako kwenye vya upinzani.

Hata kwa maslahi mapana ya taifa hakuna anaekubali kutofautiana na walamba asali wa zamu kwa kuhofia asiyoyajua kumfika. Sisi wote wanaCCM na wasio wanaCCM, wenye elimu na wasiokuwa na elimu wa dini zote na jinsia zote na makabila yote tunabaki kuangalia tu hata kama tunajkiua kile wanachokikosea, kile wanachokiharibu, kile wanachokiiba, na kile wanachogawana kwa maslahi yao binafsi, familia zao, koo zao na kanda zao wanakotoka.

Hata Ndugai pale sio kama yuko shwali, bali anafikiria atafanya nini sasa mbele yao, amuombe nani wafanye nini, aseme nini ambacho ni tofauti na wao na itakuwaje kwake kama akisema nini.

Mwalimu Nyerere aliyajua haya ya kulamba asali kwa zamu kuwa yatakuja kutokea wakati yeye hayupo duniani, na yatamkosa mtu madhubuti wa kuyakemea. Hii ndio sababu ya msingi kabisa ya yeye kuishinikiza CCM kukubali uwepo wa vyama vingi vya siasa nchini hata kama wananchi kwakutumia kura ya maoni walikataa vyama vingi. Nyerere alitaka vyama vingi ili visimame badala yake kuikosoa CCM atakapokuwa hayupo duniani.

Na Nyerere hakutaka kuwepo na utitiri wa vyama vya siasa, bali alitaka CCM ishindane kwa haki na chama kingine kikubwa cha upinzani. Bahati nzuri hicho chama cha upinzani alikitaja kabisa kwa jina kutokana na kuwa na sera safi. Kwakuwa chama hiki cha upinzani kilipata baraka kamili za baba wa Taifa hivyo nawaomba wale wote ambao ni wana CCM kindakindaki wasioridhishwa na namna mambo yanavyoendeshwa ndani ya CCM wahamie CHADEMA ili kukipa nguvu ambayo Mwl Nyerere aliikusudia chadema iwe nayo.

Mwl. Nyerere aliendelea kusema, mpinzani wa kweli wa CCM atatoka CCM, hivyo ni muda wa unabii wa Mwl Nyerere kutimia. Na kila mwanasiasa au mtu yeyoteambae ataihujumu chadema ajue hataishi kwa amani kwakuwa chadema ina mkono, ndoto na wosia wa Mwl Nyerere mwenyewe kwa wanaCCM wenzake na watanzania wote. Aliyasema yote kuhusu chadema hadharani hakuna ambaye hakumsikia akisema juu ya chadema.

Ni bahati mbaya tu chadema ya sasa nayo ina viongozi ambao wanaochumia tumbo zao ingawa ina sera safi ambazo mwl Nyerere alizikubali na kuzisifia hadharani mchana kweupe. Ni muda wa wanaCCM kuhamia chadema ili unabii wa baba wa Taifa utimie.
mlitabiliwa ndio lakini hamna lolote mliloliwekeza kwenye siasa , mlikuwa na ruzuku kubwa mkawa mnagawana mkashindwa kujenga sehemu za kufanyia mikutano yenu ya chama, ni mwendo wa kukodi tuu. kisa ati mlengo wa kati.mnashida nyinyi mpaka basi
 
KWA hiyo wakivaa gwanda za makamanda Hapo 2025 utawapigia kampeni sio!!?
Mimi nafahamu kuwa ile roho ya kundi la G55 ya akina Njelu Kasaka ingali ipo ndani ya CCM, ni muda tu haujafika. Hata paka ukicharaza sana ndani ya chumba kilichofungwa pande zote anageuka kuwa chui na kufanya mambo anayofanya chui kwa binadamu. Kundi linaloramba asali haliruhusu CCM watu wanaofikiria tofauti ndani ya chama. WanaCCM wote wanatakiwa wafyate mikia yao hadi zamu ya wanaoramba asali ipite kwanza. yaani wasubiri zama yao nao ije.
 
Back
Top Bottom