Mwl. Nyerere aliitabiria mema CHADEMA, Ndugai na Bashiru msihuzunike

Ndugai na Bashiru ,Polepole wanakubalika ile mbaya huku mtaani
Wameachana na agenda zao baada ya kupewa vibuyu vya asali. Nyerere aliwaachia maadui wa taifa tofauti na adui wanaemjadili kwenye vikao vyao. Mwl amewaachia maadui wa ujinga, umaskini, maradhi, ukabika, udini na rushwa lakini wao wanamhubiri adui mmoja TU ambae ni watanzania wenzao ambao wako kwenye vyama vya siasa vya upinzani.
 
Kwetu sisi tunaamini kuwa watu hawafi bali wanageuka kuwa kitu kingine bora na chenye nguvu zaidi kuliko walivyokuwa. Makosa makubwa ya Rais Ben Mkapa yaliyomkasirisha Mwl kule aliko sasa ni kuyauza mashirika yake ya umma na kuwaita wapinzani malofa. Kuita wapinzani malofa ni sawa na kumuita Mwl lofa pia, maana Mwl alichangia sana kuvileta vyama vya upinzani. Hivyo hasira ya Mwl juu yake haiwezi ndogo.

Rais Kikwete yeye amepata baraka zote za Mwl na ndiyo maana yuko kama alivyo sasa. Huyu jamaa alitii maagizo ya mwl ya kuvilea vyama vya siasa, chadema na cuf vilinawili wakati wa JK, amepata baraka zote za Mwl kwa kutimiza hili.

Kosa la Rais JPM ilikuwa kuvinyonga kabisa vyama vya upinzani nchi visiwepo kabisaaa. Jambo hili halikubaliki kwa Mwl kabisa na hawezi kukusamehe uishi, hasira yake kwake ingekuwa kubwa kabisa kwakuwa unataka kumkosoa kwa kuvileta vyama vingi. Mwl aliitaka CCM ivillee vyama vya siasa vya upinzani hadi viwe na uzoevu, vikubwa na vichache ili vimudu kupokezana na CCM katika kuiongoza nchi, badala yake JPM alitaka kuviua kinyume na maagizo ya Mwl ambayo iliiagiza CCM hadharani mchana kweupe.

Hebu msikilizeni Mwl alichowaagiza CCM kuhusu vyama vya siasa vya upinzani

Rais Samia lazima nae awe makini kuhusu agizo hili la baba wa taifa kwa CCM.
Nyerere alikuwa na akili za ziada sana zilizochanganyika na unabii, alijua kuwa ndani ya CCM watu wenye mawazo mbadala na watawala hawatasikilizwa wala kukubalika hata kama wana mawazo mazuri, alijua pia watu wenye mawazo mbadala hawaruhusiwa kusajili chama kikapitishwa, ndio maana alitaka vyama vya upinzani viwepo.
 
mlitabiliwa ndio lakini hamna lolote mliloliwekeza kwenye siasa , mlikuwa na ruzuku kubwa mkawa mnagawana mkashindwa kujenga sehemu za kufanyia mikutano yenu ya chama, ni mwendo wa kukodi tuu. kisa ati mlengo wa kati.mnashida nyinyi mpaka basi
 
KWA hiyo wakivaa gwanda za makamanda Hapo 2025 utawapigia kampeni sio!!?
Mimi nafahamu kuwa ile roho ya kundi la G55 ya akina Njelu Kasaka ingali ipo ndani ya CCM, ni muda tu haujafika. Hata paka ukicharaza sana ndani ya chumba kilichofungwa pande zote anageuka kuwa chui na kufanya mambo anayofanya chui kwa binadamu. Kundi linaloramba asali haliruhusu CCM watu wanaofikiria tofauti ndani ya chama. WanaCCM wote wanatakiwa wafyate mikia yao hadi zamu ya wanaoramba asali ipite kwanza. yaani wasubiri zama yao nao ije.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…