Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unasema Ukweli kabisa; mfano mzuri ni Mangi Marealle wao walikuwa wana chama chao ambacho sidhani walikuwa wanajua TANU - TANU kilikuwa cha Watu wa kanda ya DAR; Na Kanda ya ziwa walikuwa na Chama Chao na Makwaia alikuwa ni kiongozi na alikuwa msomi na Kagera hivyo hivyo Sir George Kahama na kusini pia; Hayo Maeneo yalikuwa yameendelea kivyake; na Kama Nyerere asinge amaua kutafuta na kuamua kimoja kiwa cha NCHI NZIMA sidhani UHURU ungepatikana; na kama Ungepatikana sidhani tungekuwa na AMANI na MUUNGANO TULIOKUWA nao WAKATI wa NYERERE
Wewe Angalia kuna Kisiwa kinaitwa HAITI nadhani ni kikubwa kidogo zaidi ya Zanzibar au the same size Wanazungumza lugha Moja CREOLE... Lakini kwasababu ya kuto-mingle kwenye hicho kakisiwa kuna zaidi ya 6 dialects; ni CREOLE wengine waongea kimkato hauwezi hata kuelewa ni ni kiinchi cha watu sio zaidi ya Milioni 3; Wamegawana KIJIMBO Walipata Mafuriko Unaona wenye Uwezo wanaoishi USA wanapeleka kwao kwanza... Wanasema sehemu nyingine hawazijui na ni kakisiwa kadogo...
Sasa Angalia sisi Nyerere alivyoifanya Tanganyika; wote hakutupa UHURU WETU alichukua kimoja au viwili ili kutufanya angalau tuwe sawa... lakini sisi ni wanadamu haturidhiki tunadhani kuna alivyofanya kwa CHUKI...
Nyerere alianzisha chama chake pamoja na wenzake wakiwa Makerere katikati ya miaka ya 1940. Walikuwa wanapanga kukileta Tanganyika ili kukifanya kiwe chama cha kitaifa na kuongoza harakati za Uhuru. Bahati nzuri/mbaya mmoja wa wanafunzi wenzake pale (nadhani ni wa kina Mwapachu) alimwambia kuwa tayari kulikuwa na chama ambacho kilikuwa na matawi ya kitaifa (TAA). Wakakubaliana kuwa watakapomaliza masomo waende kujiunga nacho na kukibadilisha kuwa chama cha siasa. Akatumwa Dr. Kyaruzi (walikuwa wote na Nyerere Makerere) pamoja na wengine kwenda kutakeover TAA ambayo ilikuwa inasuasua ikiwa imepitia vikwazo vingi. Hivyo, Nyerere aliporudi kutoka Edinburgh mwanzoni mwa miaka ya 1950 alikuta wenzie tayari wameshatake over kama walivyokuwa wamekubaliana (Dr. Kyaruzi akiwa rais wa TAA). Nyerere aliwaongoza wenzie kuichukua TANU na kuibadilisha kuwa chama cha siasa cha kupigania Uhuru na kushika uongozi wa chama hicho kama walivyokuwa wamepanga miaka karibu kumi nyuma.
Kinyongo kikubwa cha baadhi ya wazee wa Dar ilikuwa ni hili la Nyerere kuchukua uongozi wa TAA na kubadilisha kuwa TANU akishirikiana na wenzake na hatimaye kuongoza harakati za Uhuru. Baadhi ya wazee hawa hawakumsamehe Nyerere kwa hilo. Wazee wengine hata hivyo wa Dar na wa Tanganyika walifurahia kuwa na Nyerere kama kiongozi wa harakati za Uhuru na muda wote wa kupigania Uhuru alikuwa ndiye kinara wa harakati hizo akiongoza kundi la mashujaa wetu wa Uhuru.
Kosa ambalo naamini Nyerere alilifanya ni kuiacha CCM kama chama tawala baada ya kurudisha mfumo wa vyama vingine. Kulitakiwa kuwa na serikali ya mpito baada ya mabadiliko ya Katiba ya 1992 na kulazimisha vyama vyote kuanza moja. Kuiacha CCM kama a 'de facto' political party ambacho hakikuhitaji hata kutafuta wanachama lilikuwa kosa kubwa la kisiasa la Baba wa Taifa.
Mkuu,
Mantiki ya hoja yako imekaa kinyume,
Huenda hujaichambua kwa undani filosofia ya AA iliyoanzishwa 1929 chini ya uasisi wake Mwalimu Cesil Matola,
Pia huenda hujaichambua na kuitambua filosofia ya TAA iliyoasisiwa mwaka 1948 chini ya Klest Sykes,
Vivyo hivyo huenda hujaichambua filosofia ya TANU iliyoasisiwa mwaka 1954 chini ya Mwalimu Julius Nyerere,
Na mwisho hujachambua filosofia ya CCM iliyoasisiwa na Mwalimu Julius Nyerere!
Kwanza nikuleze kuwa kabla Mwalimu hajajiunga na TAA, tayari 1948 akiwa pale Makelele Uganda alisha chama chake cha siasa kilichoitwa TAWA,
Mwaka huo huo akaombwa na baashi ya wanachama wa TAA waliokuwa Tanganyika kuwa aachane na chama chake cha TAWA na kisha ajiunge na TAA, hivyo alikubali ombi hilo na TAWA ikabadilika kuwa tawi la TAA hapo Makerere!
1953 baada ya uchaguzi wa Arnautoglo mnazi mmoja uliompata Julius Nyerere na kuwa rais wa TAA, mwalimu aliingia na filosofia yake ya TAWA ambayo ndiyo hasaaa iliyozaa uhuru na sera za Tanganyika/Tanzania ya Mwalimu Nyerere ambayo dunia wanaifahamu!
Mkuu yapo mengi sana ambayo ni muhimu kuyafahamu ndipo ujenge hoja hiyo!
Ningekushauri tembelea mjadala wetu unaosema, "Uchochezi wa Mohamed Said na Dhihaka kwa wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar"
Mjadala upo hapa jf jukwaa la siasa!
Nikijaribu daka vitu vichache naweza pata hivi:
1.kuwepo kwa vyama vingine ktk sehemu za nchi.-Hii ni kweli wachaga walikuwa na vyao,na marealle was nothing but kibaraka wa mzungu na baadaye kuwauza wenzake ambo walimchagua kuwa mangi mkuu na kuingiza kilimanjaro ktk makubaliano binafsi na TANU..na hivyo wenzake wakavunja umangi mkuu.Pia kulikuwa na vyama vilivyokuw avikubwa tuu na vilitaka kuwepo bila kuvinja uchifu.
2.suala la pili ni muunganiko wa nchi kupitia chama kimoja.Kweli ni jambo sahihi ila haikuwa sahihi kutumia TANU ambayo tayari ilianza na miba ya U -Dar ..Kitu kilihcoleta Zimwi la taabu hadi leo.Unafiki wa waanzilishi wengine baada ya Mwl Kuwekeza kwa mawazo na juhudi na uwezo binafsi,haukuishia ktk glory walizopata baadaye.Bado walitaka Glory zote hata zile za Nyerere.Hayo magugu ndio yameingia na kuota mizizi ktk CCM ya leo.
Chama kimoja si wazo baya,ila haikuwa sahihi kuwa TANU.
Binafsi huwa sielewi ni nini kilimfanya nyerere kuingia maamuzi ya watanzania na kuingia miguu yote miwili kwenye kampeni za 1995?
You are Definately RIGHT... Mangi Marealle yeye hakutaka UHURU; Walikuwa wameendelea Wanapata pesa za kigeni; Wanasomesha Wanachama wao Nje ya NCHI; Wana Magazeti yao; Chama chao CHA USHIRIKA kilikuwa kinasaidia Wananchi wao... Na Ukiangalia Upande wa MACHAME pia walikuwa na Powerful wanamwita nadhani SHANGALI wao walijenga hadi HOSPITALI - Machame Hospital Walikuwa na barabara ya lami... yaani walikuwa wameendelea
Sasa uwaambie tunataka tumwondoe MWINGEREZA; Hawawezi kukusikia... kwahiyo NYERERE alifanya vya ajabu wao kumsikiliza kuwaambia watu wao kuipigia kura TANU halafu baada ya UHURU kuondoa UCHIFU ili tu kuondoa hizo nguvu zao na kufanya nchi iwe na AMANI na MOJA; sasa hapo sio kuwa waislamu ndio waliokuwa wamekosa baadhi ya haki zao ni wengi; na NYERERE akapiga marufuku Maendeleo KILIMANJARO mpaka Mikoa Mingine ifikie angalau hayo Maendeleo...
Sasa ukikaa chini na kuanza kuorodhesha nani walinyimwa haki ili tu kuleta AMANI na MSHIKAMANO NCHINI kila mtu; HADI Mama zetu walioachwa na BABA ZETU Mama yangu alikwenda kusoma nje ya nchi; Baba hakuvumilia akapata kimada wakazaa nyumba ilikuwa ya Mama yangu; Mama yangu karudi... Mahakama zetu kwa Makubaliano wakati wa UHURU bado kuna sheria za kiislamu zinafuatwa; Baba ndie mwenye uamuzi wa Mwisho... Kwahiyo BABA yangu akachukua NYUMBA sisi tukakaa na Mama kulikuwa hakuna any CHILD SUPPORT ni mama katusomesha mpaka VYUO VIKUU; Yeye bada kaendelea na kaoa mara nyingine tena na furaha kwake... na hana responsibility...
Sasa hapo Nami natakiwa pia kulalamika nilionewa na hiyo SYSTEM ya NYERERE?
Duh!
Mada imejaa maoni yasiyo na mashiko ya muanzisha sredi.
Lakini at least matusi yamepungua maana hawezi kujitukana!!
Kosa ambalo naamini Nyerere alilifanya ni kuiacha CCM kama chama tawala baada ya kurudisha mfumo wa vyama vingine. Kulitakiwa kuwa na serikali ya mpito baada ya mabadiliko ya Katiba ya 1992 na kulazimisha vyama vyote kuanza moja. Kuiacha CCM kama a 'de facto' political party ambacho hakikuhitaji hata kutafuta wanachama lilikuwa kosa kubwa la kisiasa la Baba wa Taifa.
Kwame Nkurumah wa Ghana alisema sababu ya kuwa na single party system ni kwakuwa wasomi walikuwa wachache ilikuwa rahisi kukusanya wasomi wale kwenye chama kimoja na kuongeza nguvu kwenye elimu, raia watakapokuwa na elimu ya kutosha watakuwa na uwezo wa kuwa na multi party system. Nyerere na Nkurumah walikuwa maswahiba wazuri, na ninaona mantiki hiyo ilikuwa kwa Tanzania pia.
Kwanini usijaribu kuwa human being kidogo.Wengine tunaongelea Choices za taifa ambazo zilikuwepo na nini kingechaguliwa ili taifa liwe na matokeo tofauti na haya tuyaonayo kwa CCM.Unasahau kuwa babiyo ni shikaji la wengi, kwa hiyo sikushangai nawe waiga, homoism is hereditary.
Fuatilia watu wa kwenu walioishia Mombasa.
You started it , kama kwenu wanaume ni "mamsapu" basi inaelezea makuzi yako.Kwanini usijaribu kuwa human being kidogo.Wengine tunaongelea Choices za taifa ambazo zilikuwepo na nini kingechaguliwa ili taifa liwe na matokeo tofauti na haya tuyaonayo kwa CCM.
wewe unaongelea mambo ya "haki sawa" ktk nchi yenye watu wenye staha,na wenye vitu vya maana zaidi kuchukua nafasi ktk ubongo kuliko,choo unachokomaa nacho hapa.