SoC04 Mwongozo wa Maendeleo: Njia ya Tanzania kuelekea Uchumi Endelevu na Usawa

SoC04 Mwongozo wa Maendeleo: Njia ya Tanzania kuelekea Uchumi Endelevu na Usawa

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
May 24, 2023
Posts
12
Reaction score
5
Kwa kuwa maendeleo ni mchakato wa pamoja kati ya serikali na wananchi, hapa kuna hoja kadhaa ambazo zinaweza kuchangia maendeleo makubwa Tanzania ndani ya miaka 5 hadi 25
Ila katika kila point ntakayotoa ELIMU ni kipaumbele changu

1. Elimu Bora na Endelevu: Kuwekeza katika elimu ya msingi, sekondari, na elimu ya juu kwa kuzingatia ubora na ufikiaji unaowezeshwa na teknolojia.Na elimu hizo zinapaswa kuendana na vipaji na vipawa vya wanafunzi hao kama kilimo, biashara, na hata sanaa na sayansi wanapaswa kufundishwa kuanzia ngazi ya msingi jambo ambalo wanafunzi watakua wanakua nalo tangia level ndogo ya elimu yao(msingi) mpaka kufikia level kubwa katika elimu yao(vyuo vikuu) na vitu watakavyo fundishwa ni vile ambavyo vipo katika maisha ya kawaida na hata wakimaliza shule wanauwezo wa kufanya kitu wakiwa mtaani hivo wanafunzi wanakua na elimu, maarifa pamoja na ujuzi katika sekta fulani ambayo wameipata shuleni na sio kumkaririsha mtoto kua sauti ya paka ni nyau sijui mdudu kagawanyika katika sehemu tatu dogo anakariri ili ajibu mtihani afaulu baada ya hapo wasomi ni feki ila vijana wakifundishwa kulingana na vipawa/shauku zao kua kilimo kinakuwaje au biashara kama za mtandaoni nk hata wakirud mtaan wanaweza wakapatiwataji na kufanya kitu wasisubiri kuajiliwa tuu. Elimu endelevu itahakikisha vijana wanakuwa na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira la baadaye na kuwa na biashara binafsi.

Just assume mtaala wa taifa letu ungekuwa hivi

ELIMU YA AWALI
Hapa watoto wanaenda shule kunywa uji kucheza na walimu wao na mwendo wa alphabet 🔤 ,namba tu na kutambua passion ya mtoto (kumwandalia mandhari ya ndoto zake) kuwe na toys za fani mbalimbali apo kama mwalimu kweli ana elimu yake ya ku Hussle na kuzaliwa lazma ajue tu dogo anapenda nini lakin msaada wa wazaz lazma uwepo

ELIMU YA MSINGI
Darasa 1-3
Hapa ni kumkazania dogo sasa mpaka darasa la tatu anajua kusoma, kuandika na kuhesabu vyema lakini walimu waendelee kukiza vpawa vyao hata wakifundisha wawaite kwa majina ya ndoto zao kama engineer, daktari, mhasibu... Hii itaongeza shauku kwa madogo

Darasa la 4
Hapa ndio kuwagawa sasa watoto kulingana na fani zao ila wanapaswa kuoneshwa kuwa kila fani inamtegemea mwenzake hii itafa nya kusiwepo na dharau baina yao maana nlikuwa naona nlipokuw sekondari wale wa sayansi waliwadharau sana arts kwasababu ya kosa la walimu na hata jammii nzima na uongozi kwa kuruhusu baadhi ya watu waonekane hawana akili kisa walifeli mtihani kwa kukosea kujibu kua binadamu wa kwanza alikuwa nyani na mdudu kagawanyika katika sehemu tatu
Hivo basi walimu wanapaswa kuonesha madogo kua ili mwanasiasa aweze kuongea na raia na dunia nzima ikamsikia lazima kuwe na sayansi, sanaa na biashara apo kati ili siasa ifanye kazi lasivyo watengeneza mic,warusha matangazo, wanaochukua video wakigoma unaona huyu mwanasiasa ata pata tabu kufikisha ujumbe

Darasa 5-6 au 7 kama bado itakuwepo
Hapa sasa kila mtu anaelewa kuhusu fani yake na anaipambania aielewe kwa kina kuhusu fani yake ili imletee tija miaka ya badae
Sasa hata mitihani ya wanafunzi iwe ya kalamu kama kawaida ila kuwe na maswali ya mantiki issue sio kumfanya mwanafunzi akariri notes nyingi maana kwa mtaala wetu mwanafunzi anayefaulu ina maana kichwa chake ni kizuri kuhifadhi notes za mwalimu na anaefeli ni kinyume chake huo ni ujinga ngazi ya MASTERS
Kinachotakiwa ni mwanafunzi kuulizwa vitu vilivyopo ndani ya fani yake kama biashara muulizeni akikopeshwa laki nane atafanya biashara gani, ni kwa namna gani ataweza kuanzisha mfumo wa kampuni binafsi ambazo utajiendeleza wenyewe na maswali mengi yahusuyo fani yake kama mitihani chuo ilivyo kwamba ulichofunzwa kulingana na course yako ndivo utakavo jibu lakini masomo 11 kichwa chenyewe ndo kile na akuna hata mwalimu anaefundisha masomo yote hayo

ORDINARY LEVEL NA ADVANCE
Kwakuwa kule msingi alikuwa ananyweshwa maziwa sasa huku ndio anakutana na vitu vyenyewe anaingia deep zaidi na kuelewa zaidi ni kwa namna gani Mifumo iliyopo hapa duniani katika fani yake ina fanya kazi
Sasa mtu atakuwa anajiuliza FANI ZIPO ZAIDI YA 10000 Walimu watafundishaje fani zote
Ndio maana kuna CLASSIFICATION
kua kuna Science hapa fani zote zilizopo ndani ya scence zinakuwa hapa na kwengine hivo hivo, Arts na Commercial
Na kuanzia chini wnafunzi wanakuwa katika mchepuo mmoja lakini mpak chuo kila mwanafunzi atakuwa yupo eneo lake makhsusi

HAPA LENGO LANGU KUBWA NI KUA VINAVYOFUNDISHWA VYUO VIKUU VIANZIWE NGAZI YA CHINI {PRIMARY} KWA MUKTADHA WA KUELEWEKA
Sio porojo za EVOLUTION OF MAN
2. Uwekezaji katika Miundombinu: Kuendeleza miundombinu muhimu kama vile barabara, reli, viwanja vya ndege, na nishati ili kuchochea ukuaji wa kiuchumi na kuvutia uwekezaji wa ndani na nje.Miundombinu hiyo ni faida kubwa sana katika usafirishaji wa malighafi, bidhaa, huduma mbalimbali tena kwa wakati ambazo zinaleta tija katika taifa letu

3. Kuimarisha Huduma za Afya: Kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wote na kuwekeza katika miundombinu ya afya, vifaa, na mafunzo ya wataalamu wa afya hii itasaidia vikubwa kuhakikisha kuwa nguvu kazi ya taifa letu inaimarika kwa kiasi kikubwa sana

4. Kukuza Sekta ya Kilimo:
Kutoa msaada kwa wakulima na kukuza kilimo cha kisasa na cha kibiashara ili kuongeza uzalishaji, kuboresha usalama wa chakula, na kujenga uchumi wa vijijini.
Kama inavyojulikana kuwa UTI WA MGONGO WA TAIFA LETU NI KILIMO kama serikali,NGOs pamoja na wananchi tunapaswa kuichangamkia kabisa sekta hii kwa maana taifa likiwa halina njaa basi KAZI LAZIMA ITAENDELEA TU hivo na MUNGU alivojalia nchi yetu kuwa na udongo ambao ni baraka kwa aina nyingi ya mimea tutumie baraka hiyo kwa kuhakikisha kua kama TANZANIA ndio nchi pekee inayotoa madini adimu ya TANZANITE basi tuhakikishe katika kilimo tunaongoza kwa kulisha nchi za jirani na mabara yote kwa ujumla kutokana na kilimo chetu na hii itatokea tu endapo serikali itaangilia sekta ya kilimo kwa jicho la nne ambako ni kuanzia ngazi ya elimu kule tupate ma expert wa kilimo tena kutoka nchi mbalimbali kwa kusomesha vijana wazalendo wa kitanzania wenye uchu wa maendeleo

5. Kupambana na Rushwa: Kuanzisha mifumo imara ya kisheria na kimaadili ya kupambana na rushwa ili kuhakikisha uwajibikaji na uwazi katika serikali na sekta binafsi.
Kama TAKUKURU ilikuwa inafanya kazi kwa effiency ya 65% hapa inapaswa kufanya hima juu chini kufikia 95% ya kutokomeza Rushwa nchini maana Rushwa ni moja katika adui wa maendeleo hususan katika seka za ajira, ufadhili wa masomo na sekta nyinginezo unakuta raia wananyimwa haki zao kabisa mfano halisia unakuta updates za ajira kutoka serikalini na taasisi binafsi, ukifanya application haupati mirejesho yoyote mpk miezi na masiku inaisha na ukifatilia utakuta kabla ya deadline nafasi zilishajaa na taarifaili upate ajira fulani lazima uwe na connection jambo ambalo sio zuri kiukweli MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI kama mtu anastahili nafasi fulani ni anastahili tu ni ujinga uliokithiri mtu kujifunza kazi kazini wakati kuna wenye experience kutoka katika mashirika ya kujitolea na hawapati hizo chance

6. Kuwekeza katika Teknolojia na Ubunifu:
Kukuza ujasiriamali na uvumbuzi kwa kuwekeza katika teknolojia na kuanzisha mazingira wezeshi kwa makampuni ya ndani na wawekezaji wa kigeni.
Ivi unajua kua vijana wa kitanzania ni wabunifu sana nilishangaa sana kukutana na kijana mchepuo wa art ambae kaikimbia physics kisa ngumu lakini alifanya wiring katika dormitory wakati huo wenye physics yao ya maandishi wanaduwaa ipo hivi kama kweli tunahitaji maendeleo katika sekta ya teknolojia basi serikali iwekeze MASHULENI maana huko ndo kuna bongo zinazo kua mtoto wa shule ya msingi akiweza kuelewa na kufanya codes za html na css akifika chuo huyo katika upande wa computer science haumwambii kitu

7. Kulinda Mazingira: Kuchukua hatua za kuhifadhi mazingira kwa kudhibiti uchafuzi wa mazingira, kukomesha uharibifu wa misitu, na kukuza matumizi ya nishati mbadala.

8. Kuendeleza Utalii: Kuwekeza katika sekta ya utalii kwa kukuza vivutio vya utalii, kuboresha huduma za utalii, na kuhakikisha utunzaji wa maliasili na utamaduni.

9.Kukuza Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa: Kushirikiana na nchi jirani na washirika wa kimataifa katika biashara, usalama, na maendeleo ili kujenga jumuiya imara na kuongeza fursa za kiuchumi.

10.Kuwekeza katika Vijana: Kutoa fursa za ajira, elimu, na mafunzo ya ujuzi kwa vijana ili kuwawezesha kuchangia katika maendeleo ya nchi.

11.SERIKALI KUIPA NAFASI KILA SEKTA MAENDELEO NCHINI
Moja ya dhima kuu ya serikali ni kutoa nafasi kwa raia wake inatakiwa ifikie hatua kua serikali inatoa gwanda na silaha bandia pamoja na jeshi ili tu kuigizwa filamu inayohusiana na harakati za kiserikali sio kila siku mapenzi na uchawi hebu tuoneni hata wivu kwa wenzetu ona india waandishi wanaikosoa serikali yao na wakati huohuo serikali inaunga mkono 🤝 na kusapoti filamu hizo.

Kinachopaswa hapa ni serikali kuunga mkono hawa walioko katika sekta za filamu maana filamu inafikisha ujumbe fulani kwa urahisi sana na hata kuitambulisha miji ya nchi husika,utamaduni wetu kwani hamuoni india ilivojitambulisha utamaduni wake mpk karibia dunia nzma inaelewa kuhusu india na vivutio vyake sasa hauoni utalii apo sio vijana kupata vibali vya kuigiza na ni wachanga wanapigwa mamilioni hapo kwenyewe wanaanza sio vizuri tutabaki kuskia maendeleo kwa wenzetu

Kwa kuzingatia hoja hizi na kujenga ushirikiano imara kati ya serikali na wananchi, Tanzania inaweza kufikia maendeleo makubwa ndani ya miaka 5 hadi 25.
 
Upvote 2
Moja ya dhima kuu ya serikali ni kutoa nafasi kwa raia wake inatakiwa ifikie hatua kua serikali inatoa gwanda na silaha bandia pamoja na jeshi ili tu kuigizwa filamu inayohusiana na harakati za kiserikali sio kila siku mapenzi na uchawi hebu tuoneni hata wivu kwa wenzetu ona india waandishi wanaikosoa serikali yao na wakati huohuo serikali inaunga mkono 🤝 na kusapoti filamu hizo.
Kinachopaswa hapa ni serikali kuunga mkono hawa walioko katika sekta za filamu maana filamu inafikisha ujumbe fulani kwa urahisi sana na hata kuitambulisha miji ya nchi husika,utamaduni wetu kwani hamuoni india ilivojitambulisha utamaduni wake mpk karibia dunia nzma inaelewa kuhusu india na vivutio vyake sasa hauoni utalii apo sio vijana kupata vibali vya kuigiza na ni wachanga wanapigwa mamilioni hapo kwenyewe wanaanza sio vizuri tutabaki kuskia maendeleo kwa wenzetu
Bora wewe umeliweka wazi. Good.

Sema nina swali kwako, mbona kama unaipondea sana elimu. Kuna ubaya gani mtoyo akizitambua sehemu za panzi na mageuko ya binadamu?

Kwa yeyote mwenye kiwango fulani cha akili anatambua kuwa hata injinia ana kitu cha kumsaidia akijifunza tu lugha. Mfano mambo ya 'grammar' na upangiliaji wa aya na sentensi lazima yatamsaidiaga kwenye kuandaa mipangokazi yake. Elimu yoyote ya kitu cha kweli inafaa kwa mafundisho. Kujua mambo mengi kunasaidia hata kuchagua ni kipi mtu ajikite kwacho bro
 
Bora wewe umeliweka wazi. Good.

Sema nina swali kwako, mbona kama unaipondea sana elimu. Kuna ubaya gani mtoyo akizitambua sehemu za panzi na mageuko ya binadamu?

Kwa yeyote mwenye kiwango fulani cha akili anatambua kuwa hata injinia ana kitu cha kumsaidia akijifunza tu lugha. Mfano mambo ya 'grammar' na upangiliaji wa aya na sentensi lazima yatamsaidiaga kwenye kuandaa mioangokazi yake. Elimu yoyote ya kitu cha kweli inafaa kwa mafundisho. Kujua mambo mengi kunasaidia hata kuchagua ni kipi mtu ajikite kwacho bro
Hasara za Wanafunzi Kufundishwa Maisha ya Panzi na Revolution of Man Badala ya Fani na Niche Zao za Ndoto:
Kuna hasara kadhaa za wanafunzi kufundishwa maisha ya panzi na 'Revolution of Man' badala ya kufunzwa fani na niche zao za ndoto au fursa zilizopo baada ya kutoka mashuleni:
1. Kukosa Ujuzi wa Kazi:
* Maisha ya panzi hayatoi ujuzi wa vitendo unaohitajika kwa ajili ya kazi nyingi.
Wanafunzi wanaweza kujikuta wakikosa ujuzi unaohitajika kupata ajira nzuri baada ya kuhitimu.Badala wafundishwe biashara za mtandaoni kama forex , ubunifu wa maudhui na mambo mengine kedekede
2. Kukosa Mwelekeo:
*Masomo hayo wasomayo hayatoi mwelekeo wazi kwa wanafunzi kuhusu mustakabali wao.
Wanaweza kujikuta wakihangaika kutafuta njia yao maishani baada ya kuhitimu.
3. Kushindwa Kufikia Malengo ya Kibinafsi:
* Maisha ya panzihayasaidii wanafunzi kufikia malengo yao ya kibinafsi.
* Wanaweza kukosa fursa za kufanikiwa katika taaluma zao walizochagua.
4. Kupoteza Muda:
Muda unaotumika kufundisha wanafunzi maish ya panz ni muda unaopoteza ambao unaweza kutumika vyema kufundisha ujuzi wa vitendo na kuwapa mwelekeo kuhusu mustakabali wao.
5. Kuongeza Ukosefu wa Ajira:
Kukosa ujuzi wa kazi na mwelekeo kunaweza kusababisha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.
Hii inaweza kusababisha matatizo ya kijamii na kiuchumi kwa nchi.ivi kijana akimaliza form four na kapata one ya saba tena A PLUS zote na tu assume huyo kapata 100% zote somo alilofeli ana 99% ina maana ubongo wake ni mzuri sana kukariri notes za walimu na tena muambie aaply kanuni za maaomo aliyosoma karika maisha ya kawaida hawezi si bora hata wazee wetu waliofunzwa kilimo
Mbadala Bora:
Badala ya kufundisha wanafunzi maisha ya panzi sijui mbu na ni bora kuwapa mafunzo ya fani na niche zao za ndoto au fursa zilizopo baada ya kutoka mashuleni. Hii itawasaidia kupata ujuzi unaohitajika kupata ajira nzuri, kufikia malengo yao ya kibinafsi, na kuchangia kwa maendeleo ya nchi yao.
Ni muhimu kutambua kuwa wanafunzi wanapaswa pia kufundishwa kuhusu umuhimu wa kazi ngumu, nidhamu, na ujasiriamali. Hii itawasaidia kufanikiwa katika maisha yao ya kibinafs
i na ya kitaaluma.
 
Nimependa topic yako, reforms inahitajika kwenye elimu yetu,kuwe na practical education inayoendana na mazingira yetu...mimi naona bado sana kufuata standard syllabus, elimu iwe tailored kuendana na mazingira yetu. Hii itatoa msomi anayeweza kukabiliana na changamoto za mtaani, sio kutoa msomi ana theories ambazo ziko too general anashibdwa kuzi apply mtaani. Kutunga syllabus inayoendana na mitaa yetu ndio naona changamoto kubwa. You have my vote.
 
Hasara za Wanafunzi Kufundishwa Maisha ya Panzi na Revolution of Man Badala ya Fani na Niche Zao za Ndoto:
Kuna hasara kadhaa za wanafunzi kufundishwa maisha ya panzi na 'Revolution of Man' badala ya kufunzwa fani na niche zao za ndoto au fursa zilizopo baada ya kutoka mashuleni:
1. Kukosa Ujuzi wa Kazi:
* Maisha ya panzi hayatoi ujuzi wa vitendo unaohitajika kwa ajili ya kazi nyingi.
Wanafunzi wanaweza kujikuta wakikosa ujuzi unaohitajika kupata ajira nzuri baada ya kuhitimu.Badala wafundishwe biashara za mtandaoni kama forex , ubunifu wa maudhui na mambo mengine kedekede
2. Kukosa Mwelekeo:
*Masomo hayo wasomayo hayatoi mwelekeo wazi kwa wanafunzi kuhusu mustakabali wao.
Wanaweza kujikuta wakihangaika kutafuta njia yao maishani baada ya kuhitimu.
3. Kushindwa Kufikia Malengo ya Kibinafsi:
* Maisha ya panzihayasaidii wanafunzi kufikia malengo yao ya kibinafsi.
* Wanaweza kukosa fursa za kufanikiwa katika taaluma zao walizochagua.
4. Kupoteza Muda:
Muda unaotumika kufundisha wanafunzi maish ya panz ni muda unaopoteza ambao unaweza kutumika vyema kufundisha ujuzi wa vitendo na kuwapa mwelekeo kuhusu mustakabali wao.
5. Kuongeza Ukosefu wa Ajira:
Kukosa ujuzi wa kazi na mwelekeo kunaweza kusababisha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.
Hii inaweza kusababisha matatizo ya kijamii na kiuchumi kwa nchi.ivi kijana akimaliza form four na kapata one ya saba tena A PLUS zote na tu assume huyo kapata 100% zote somo alilofeli ana 99% ina maana ubongo wake ni mzuri sana kukariri notes za walimu na tena muambie aaply kanuni za maaomo aliyosoma karika maisha ya kawaida hawezi si bora hata wazee wetu waliofunzwa kilimo
Mbadala Bora:
Badala ya kufundisha wanafunzi maisha ya panzi sijui mbu na ni bora kuwapa mafunzo ya fani na niche zao za ndoto au fursa zilizopo baada ya kutoka mashuleni. Hii itawasaidia kupata ujuzi unaohitajika kupata ajira nzuri, kufikia malengo yao ya kibinafsi, na kuchangia kwa maendeleo ya nchi yao.
Ni muhimu kutambua kuwa wanafunzi wanapaswa pia kufundishwa kuhusu umuhimu wa kazi ngumu, nidhamu, na ujasiriamali. Hii itawasaidia kufanikiwa katika maisha yao ya kibinafs
i na ya kitaaluma.
Ebhanaa, una juhudi sana kufafanua hoja, ninakupa hilo 👏
 
Back
Top Bottom