MX Carter ni Nani? Na Kwanini Wasanii Wanalalamika Kuhusu Dhuluma Zake?

MX Carter ni Nani? Na Kwanini Wasanii Wanalalamika Kuhusu Dhuluma Zake?

itakiamo

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2014
Posts
1,096
Reaction score
1,909
Habari za wakati huu wadau wa JamiiForums,
Kumekuwa na gumzo kubwa mitandaoni kuhusu mtu anayejulikana kwa jina la MX Carter. Inaonekana kuwa jina hili limehusishwa sana na masuala ya usambazaji wa kazi za wasanii kwenye majukwaa ya kidijitali kama YouTube, Spotify, na mengineyo.
Kinachoshangaza ni idadi kubwa ya malalamiko kutoka kwa wasanii mbalimbali wakidai kudhulumiwa naye. Wengi wanasema hawapati malipo wanayostahili, na kuna uvumi kwamba MX Carter anamiliki haki za kazi za wasanii bila idhini yao.
Maswali yangu kwa wadau ni haya:
MX Carter ni nani hasa?
Je, ni kampuni, mtu binafsi, au ni kundi la watu?
1. Ni kwa nini wasanii wengi wanahusisha jina lake na dhuluma kwenye majukwaa ya kidijitali?
2.Kuna yeyote mwenye uzoefu wa moja kwa moja na mtu au taasisi hii?
3. Ni hatua gani wasanii wanaweza kuchukua ili kujilinda dhidi ya matatizo kama haya?
Naamini kuwa JamiiForums ni jukwaa lenye watu wenye uelewa mpana kuhusu masuala mbalimbali, hasa ya muziki na hakimiliki.
Ningependa kufahamu zaidi kutoka kwa wale wenye taarifa sahihi au uzoefu kuhusu hili suala.
 
Simfahamu huyo ila nachojua
kuna WAZUNGU fulani miyeyusho wakiona ACCOUT YAKO inapata VIEW na Adsense inanona kila mwenzi
wanakufuata wanakutungoza wakupe mtaji ili utengeneze CONTET nzuri zaidi uzidi kuoata view na ADsense inone zaidi

wanakupa ela nzuri sana mwanzo
ila sharit utakula 30% ya mapato 70% wanakula wao
mwanzo 7bu ya ile walokupa nyingi na hata hiyo 30% inakuwa nyingi sana kwako 7bu hujawahi kuishika
kimbembe pale kazi zinavyoanza kuchanganya
na unashangaa ile ela walokupa unaipata tu kwa mwenzi mmoja
lakini wao wanachukua nyingi wewe ndogo na kazi yote wewe ndo unaifanya na jamaa hawatoi chochote tena si washakupa msingi na huyo msingi walokupa umerudi ndani ya miezi kadhaa tu
baada ya hapo ndo dizain hiyo wanalalamika na ACCOUT wameishikilia wao

hawa CONTET CREATOR wengi wa bongo haswa youtube wameingia huo mtego
waliwahi kumfata PARTINER wangu nikausoma mchezo tukawaambia mkitaka sisi tuwe 60 nyinyi 40 wakakataa wakasema watakachofanya labda kuongeza dau
bado niliona mchezo wa kijinga yaan watoe ela mara moja tu then hawahusiki tena

ila kwa namna moja au nyingine nao wanatake RISK kwa maana wanaweza fanikiwa au wakapata hasara pia
ndio mana wanakupiga PINI hutakiwi kuanzisha ACCOUNT nyingine yoyote zaidi ya hiyo ndio urushe CONTET zako ukienda kinyume na hilo unakutana warinng ya copyright issue kari sana tena sana kabisa ya mwanaukome
 
MX amekimbia nchi yupo maandishi matatu.

Mali zake nyingi zipo kwenye mnada ikiwemo nyumba ya mikocheni.

Mali za dhulma uwa hazidumu.


Huwezi kuishia la saba alafu ukawa msukuma na ukaendesha biashara zinazohitaji big brain.
Aisee
 
MX amekimbia nchi yupo maandishi matatu.

Mali zake nyingi zipo kwenye mnada ikiwemo nyumba ya mikocheni.

Mali za dhulma uwa hazidumu.


Huwezi kuishia la saba alafu ukawa msukuma na ukaendesha biashara zinazohitaji big brain.
Nasikia jamaa ni ngumbaru tu kaishia la saba ila mjanjamjanja na anayejipendekeza sana kwa wakubwa ni kama chawa pro anajifanya photographer mzuri na kubemba tenda kwa hao vigogo marafiki zake, hapo nyuma alipona ajali ya pori kwa pori akiwa na yule mhuni Kingwangwala.
 
Hivi huyu ndie yule alikuwa mpiga picha?
 
MX amekimbia nchi yupo maandishi matatu.

Mali zake nyingi zipo kwenye mnada ikiwemo nyumba ya mikocheni.

Mali za dhulma uwa hazidumu.


Huwezi kuishia la saba alafu ukawa msukuma na ukaendesha biashara zinazohitaji big brain.
Wanae kina Bruno na Gilsant wameshindwa kumsaidia kifedha kweli.
 
MX ni tapeli kitambo sana hata wafanyakazi wake huwaga halipi.

Anaishi Masaki. Apartment anayokaaa ni wasanii wachache sana bongo wanaweza kuafford

Inshort jamaa ni fraud
 
Wasanii wanafeli kutokujifunza kuhusu masuala ya kidigitali, msomi kama Billnas anafeli vipi kujipa darasa la Apple Music, Boomplay na kwingineko? Waendelee kupigwa wanadeka sana!
 
Back
Top Bottom