Habari za wakati huu wadau wa JamiiForums,
Kumekuwa na gumzo kubwa mitandaoni kuhusu mtu anayejulikana kwa jina la MX Carter. Inaonekana kuwa jina hili limehusishwa sana na masuala ya usambazaji wa kazi za wasanii kwenye majukwaa ya kidijitali kama YouTube, Spotify, na mengineyo.
Kinachoshangaza ni idadi kubwa ya malalamiko kutoka kwa wasanii mbalimbali wakidai kudhulumiwa naye. Wengi wanasema hawapati malipo wanayostahili, na kuna uvumi kwamba MX Carter anamiliki haki za kazi za wasanii bila idhini yao.
Maswali yangu kwa wadau ni haya:
MX Carter ni nani hasa? Je, ni kampuni, mtu binafsi, au ni kundi la watu?
1. Ni kwa nini wasanii wengi wanahusisha jina lake na dhuluma kwenye majukwaa ya kidijitali?
2.Kuna yeyote mwenye uzoefu wa moja kwa moja na mtu au taasisi hii?
3. Ni hatua gani wasanii wanaweza kuchukua ili kujilinda dhidi ya matatizo kama haya?
Naamini kuwa JamiiForums ni jukwaa lenye watu wenye uelewa mpana kuhusu masuala mbalimbali, hasa ya muziki na hakimiliki.
Ningependa kufahamu zaidi kutoka kwa wale wenye taarifa sahihi au uzoefu kuhusu hili suala.