GS...Umesema kitu cha maana.Kupenda kunatofautiana baina ya mtu na mtu.Kuna kupenda umuonapo mtu mara moja..Love at first sight; Kuna kupenda kunakotokana na mchakato fulani - huku huja pole pole..... kuna ulafi/matamanio ya muda mfupi..infatuation - haya ni mapenzi ya nguvu ya soda na utafanya makosa sana kuoana na mtu ukiwa umekumbwa na penzi hili utajuta sana.
Mapenzi huweza kuishia kwenye ndoa au kuisha tu bila ndoa.Kama nia ni ndoa basi mtu nadhani huna budi uwe na vipimo vya yule unayetaka kuishi naye maisha yako yote.Kuanzia tabia za mtu, na hulka nyingine.Tabia ni kitu muhimu sana maana kama mtu ana tabia zisizokubalika kama malaria ujue mwisho wake ni mbaya.
Huyu Bibie Tausi, japo kaja na mada yenye mzaha ndani yake, huenda ana kitu anataka kutufundisha.Hebu tuendelee kusoma labda tutakielewa.Namtakia kila la kheri kwenye zoezi hili la kujipatia mwenza wa maisha.