Hehehehe Huu mji huu, hapana tabidi niukimbie na kwenda kwa kamji kadogo kwingine, haya mavitu nawaachia vijana wageuze geuze magari na kujimwaya mwaya, kwanza mimi mwoga wa kuendesha gari kwa mwendo wa kasi, barabara ya Thika superhighway yenyewe husababisha niingiwe kiwewe ikitokea nimejikuta katikati magari mengi na sote tunakwenda kwa kasi.
Enzi nikiwa kijana tena hustler ilikua nafuu, nilikua siogopi chochote, ila kwa sasa bora niwaachie tu, niwe nayaona kwenye TV, haswa barabara zinazopitia juu kwa juu.