Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mahakama nchini Myanmar imemhukumu jela aliyekuwa kiongozi wa kiraia Aung San Suu Kyi miaka mingine minne, kwa kosa la kumiliki na kuingiza vifaa vya mawasiliano- walkie-talkies kinyume cha sheria lakini pia kuvunja masharti ya kupambana na Covid-19.
Hukumu hii ya pili inakuja, baada ya Suu Kyi kupewa hukumu nyingine mwezi Desemba mwaka uliopita, iliyopunguzwa hadi miaka miwili na sasa hukumu zote mbili, ni miaka sita jela, huku kukiwa na wasiwasi kuwa huenda hatimaye akafungwa akapewa kifungo cha maisha jela.
Hukumu dhidi ya kiongozi huyo wa zamani wa Myanmar, kumeendelea kushutumiwa na mataifa ya Magharibi kwa kile wanachosema yamechochewa kisiasa.
Mwezi Februari mwaka uliopita, Aung San Suu Kyi baada ya chama chake cha National League for Democracy kushinda uchaguzi wa wabunge, alikamatwa na wanajeshi na kuzuiwa nyumbani, kabla ya kufunguliwa mashtaka mbalimbali.