Mythology: Mjue Malaika Azrael(Malaika mtoa roho)

Venus Star

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2018
Posts
26,519
Reaction score
78,311
images (6).jpeg
images (7).jpeg

Ndugu zangu wana JF Leo nimeamua kuanza kutoa masomo ya mythology. Iwe kweli au siyo kweli lakini tupate kutambua namna wengine wanavyo iendesha dunia hii.

Leo nitaongelea malaika mtoa roho aitwae Azrael. Huyu anaongelewa sana katika imani za Judaism na uislam. Kwa wakristo yaani biblia wanawaongelea Michael, Gabriel na Raphael.

Ukipata kukisoma kitabu (The book of Enoch) utawatambua baadhi ya hawa malaika na baadhi ya kazi zao.

Malaika huyu unaweza kumwita ili aweze kufanya kazi kwa mujibu was taratibu za kuwaita malaika na kuongea nao.

Katika mfululizo wa masomo yangu haya ya mythology nitafundisha namna ya kuongea na viumbe vingine katika ulimwengu wa roho.

Karibuni sana.
 
Kutokana na Mythology ya dini nilizozitaja hapo juu, inaelezwa kwamba Azrael kazi yake kuandikisha kwenye kitabu cha wanaoishi duniani pindi wanapozaliwa, vile vile hufuta watu katika kitabu hicho cha kuzaliwa na kuwaandikisha katika kitabu cha kifo.

Yeye ndiye aliyepewa ufunguo wa kifo. Sasa basi kama unataka kuishi miaka mingi hapa duniani, jaribu kupata na malaika huyu.

Vilevile malaika huyu anakaa katika bingu ya tatu(Paradise aka paradiso). Mbingu ya tatu, inaelezwa kwamba baada ya mtu kufa akiwa na matendo mema ndiyo sehemu anaenda kujituliza.
 
Katika imani ya wakristo, mbingu ya tatu imeelezwa kidogo na Paul.

Namjua mtu mmoja katika Kristo, yapata sasa miaka kumi na minne, (kwamba alikuwa katika mwili sijui; kwamba alikuwa nje ya mwili sijui; Mungu ajua). Mtu huyo alinyakuliwa juu mpaka mbingu ya tatu.
2 Wakorintho 12:2
 
View attachment 2067317View attachment 2067318

Ndugu zangu wana JF Leo nimeamua kuanza kutoa masomo ya mythology. Iwe kweli au siyo kweli lakini tupate kutambua namna wengine wanavyo iendesha dunia hii.

Leo nitaongelea malaika mtoa roho aitwae Azrael. Huyu anaongelewa sana katika imani za Judaism na uislam. Kwa wakristo yaani biblia wanawaongelea Michael, Gabriel na Raphael.

Ukipata kukisoma kitabu (The book of Enoch) utawatambua baadhi ya hawa malaika na baadhi ya kazi zao.

Malaika huyu unaweza kumwita ili aweze kufanya kazi kwa mujibu was taratibu za kuwaita malaika na kuongea nao.

Katika mfululizo wa masomo yangu haya ya mythology nitafundisha namna ya kuongea na viumbe vingine katika ulimwengu wa roho.

Karibuni sana.
El alikua ni caananite deity(mungu wa wacaanan),, wenyewe wanaita pagan god,,
Hivyo inakuwa ngumu kuamini eti malaika mkuu, michael apewe jina la mungu wa kipagani,
Wote michael, daniel Rafael, israel, ezekiel, emanuel, wote wanaoishia na El,. Wanabeba jina la mungu wa kipagani wa wacaanan.
Hivyo ni wazi kuwa tumelishwa hekaya tangu zamani mno

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
 
Kutokana na Mythology ya dini nilizozitaja hapo juu, inaelezwa kwamba Azrael kazi yake kuandikisha kwenye kitabu cha wanaoishi duniani pindi wanapozaliwa, vile vile hufuta watu katika kitabu hicho cha kuzaliwa na kuwaandikisha katika kitabu cha kifo.

Yeye ndiye aliyepewa ufunguo wa kifo. Sasa basi kama unataka kuishi miaka mingi hapa duniani, jaribu kupata na malaika huyu.

Vilevile malaika huyu anakaa katika bingu ya tatu(Paradise aka paradiso). Mbingu ya tatu, inaelezwa kwamba baada ya mtu kufa akiwa na matendo mema ndiyo sehemu anaenda kujituliza.
Huyo malaika anatumia kitabu au computer kuhifadhi majina
 
Back
Top Bottom