Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 26,519
- 78,311
Ndugu zangu wana JF Leo nimeamua kuanza kutoa masomo ya mythology. Iwe kweli au siyo kweli lakini tupate kutambua namna wengine wanavyo iendesha dunia hii.
Leo nitaongelea malaika mtoa roho aitwae Azrael. Huyu anaongelewa sana katika imani za Judaism na uislam. Kwa wakristo yaani biblia wanawaongelea Michael, Gabriel na Raphael.
Ukipata kukisoma kitabu (The book of Enoch) utawatambua baadhi ya hawa malaika na baadhi ya kazi zao.
Malaika huyu unaweza kumwita ili aweze kufanya kazi kwa mujibu was taratibu za kuwaita malaika na kuongea nao.
Katika mfululizo wa masomo yangu haya ya mythology nitafundisha namna ya kuongea na viumbe vingine katika ulimwengu wa roho.
Karibuni sana.