Mzalendo Nasogea Golgota, Je huyu ndo mrithi wa ROMA? Je hatafungiwa!

Nimeuimbisha Jana kwenye sikuku ya pasaka mpaka amekata sauti ngoja Leo tena nione kama sauti imemrudia
 
Roma anaimba vibamia sikuhizi na nimeskia anataka kuingia ccm, huko ndio atapotea kabisa.
Kama anakosa hata ada ya kumlipia mwanae unategemea akimbilie wapi,akafate tu kupotea kama walivopotea original comedy walipoanza kuwagawa mashabiki wao Kwa tamaa ya hela ya leo, badala ya kuangalia brand zao walizozipigania miaka,afatae kupotea ni milard ayo baada ya cloud fm, kuanza kupoteza mvuto,kwa kushabikia upande mmoja Kwa mkate wa siku moja tu.
 
Humu kila anayechangia anawasiwasi na maisha ya huyu msanii halafu kutwa mnahamasisha maandamano tar 26, mtayaweza kweli? Acheni unafiki kijana kaamua kujilipua lolote na liwe
 
Sasa tusishangilie kabla, tungoje kwanza "akishabebwa" na Wazeya, akirudi tumpe muda kidogo, kama hakutokuwa na mabadiliko ndio tumfanyie tathmini.

Roma alianza hivi hivi ila sasa wenyewe mnaona.
 
Amenifurahisha kule mwisho eti wakiniua msisahau kunipost[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
mwenzake ROMA kwenye wimbo wake wa Tanzania alisema babu yake kamchinjia ng'ombe akambless aje mjini kutetea wanyonge,najiuliza cjui ile damu ya kafara ya ng'ombe toka kwa babu ndo imeisha makali au vipi...sasa cjui huyu kawablessed na nani na cjui kachinjiwa kitu gn!

Ila jamaa katoa kitu hadi mwenyewe nimefrahi na kutabasamu moyoni...ameonesha maana ya uzalendo kwa vitendo kupitia muziki wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…