app-facebook
Wanjiro Njango
13 hours ago
UKWELI ULIOUCHI (The Naked Truth)
Serikali ya awamu ya 5 imewavuruga Watanzania, Imewaondoa kwenye Umoja na Mshikamano.
_____________________________________
WATANZANIA tangu wanapata Uhuru walikuwa wana siri kubwa sana ya UMOJA NA MSHIKAMANO. Yaani hapa jambo kubwa lilikuwa ni kushirikiana kwa namna zote katika majonzi, raha na shida zote bila kujali kabila, dini, chama, jinsia wala anatokea kaunti gani.
Kila Rais anayeingia madarakani huapa kuyalinda mambo haya yote ya utamaduni huu na kuyaimarisha kupitia katiba...ambapo Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayatambua kwa jina la "UMOJA WA KITAIFA" Hiki kitu kimevurugwa kabisa na ccm mpya, Umoja wa Kitaifa umebaki Skeleton ni Kitu pia ambacho Kinaogopwa kuzungumzwa.
Naitwa Wanjiro Muhiru Njango, andamana nami.
___________________________________________
Awamu ya 5 ambayo ndio yenye ccm mpya ndio msingi ulioharibu mshikamano wa WATANZANIA na Umoja wa Kitaifa. Tunaposema Umoja na Mshikamano ni ule ushirikiano katika masuala ya Kijamii kati ya raia na raia, raia na taasisi, raia na kiongozi, raia na serikali n.k
UMOJA WA KITAIFA ni pale raia wa nchi moja wanapokuwa ni kitu kimoja dhidi ya nchi nyingine. Kwa mfano pale inapotokea taifa kutoka nje linalishambulia taifa lenu sio tu kwa vita hata kwa maneno, kwa kutoa data za kulishushia hadhi taifa lenu n.k. mnakuwa kitu kimoja kujibu mapigo ya taifa hilo dhidi ya nchi yenu. (Naamini nimeeleweka)
AWAMU YA 5 chini ya ccm mpya ndio MCHAWI Mkuu wa kuharibu Umoja wa Kitaifa na Mshikamano. Tangu serikali ya awamu ya 5 iingie madarakani imekuwa serikali isiyojali uhai wa watu na kuchukulia Matukio ya vifo na yanayotishia uhai kuwa ni ya kawaida hasa pale watu wanaotoa maoni dhidi ya serikali ama wanaoikosoa serikali wakipotea ama kupotezwa ama kuumizwa. (Kuikosoa serikali na Kuipinga Serikali ni vitu viwili tofauti nitafafanua siku zijazo)
Kuna viongozi tangu mwaka 2016, kuna viongozi wa vyama vya upinzani waliouawa kikatili mathalani Alfonce Mawazo (Chadema Shinyanga) alikatwakatwa mapanga mchana kweupe, Katibu wa Chadema kata ya Hananasifu (Kinondoni-Dar) aliuawa kwa kunyongwa. Madiwani wawili mkoa wa morogoro (wote Chadema) walikatwakatwa mapanga. Msaidizi wa Mwenyekiti Chadema Taifa, Ben Saanane alipotezwa mpaka leo hajaonekana, waandishi waliopatwa na Madhira haya wapo kama Azory Gwanda na wengine waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka yasiyo kuwa na mbele wala nyuma. Waliotishiwa na walioumizwa kama Tundu Lissu. Kuna hata viongozi wa vyama vingine waliopotezwa kama Mwenyekiti wa Halmashauri Kigoma kwa ACT Bw. Kanguye na wengine wanaccm wenye mtazamo tofauti na ccm mpya wametafutiwa kesi za kipimbipimbi.
Sasa mambo yapo hivi, Wakati WATANZANIA wakilia na kuomboleza katika matukio hayo mabaya kabisa Tanzania...kuna vilaza, nyumbu wa ccm mpya na viongozi wao walikuwa wanafurahia kwa shangwe nderemo na vifijo mpaka sasa hakuna anayejutia. Wapo wengi wamesikika wakisema na bado mkileta mdomomdomo tutawamaliza, wapo waliosema "Mtu msaliti Kwenye utawara wangu hatasavaivu" na mtu msaliti kwake ni yule anayemkosoa.
Waathiriwa wa matukio hayo mabaya walipoiomba serikali ya wanyonge kwamba tunaomba uchunguzi ufanyike...serikali ikawa inarukaruka hadi sasa inaruka ruka mithili ya maharage yanayochemka. Serikali ilipoombwa kwamba mashirika ya Kijasusi yahusikayo na upelelezi wa matukio kama haya yapo tayari kuisaidia Tanzania, serikali ikakataa.
Mawaziri wameendelea kujichanganya na kauli, wapo walioulizwa ile miili iliyokuwa inaokotwa fukwe za bahari ya Hindi ni ya nani walisema wahamiaji wametoka somalia miili imepeperushwa na upepo hadi Tanzania, wapo mawaziri waliosema raia waliotoweka walikimbia tu ugumu wa maisha na kutelekeza familia zao, wapo mawaziri waliosema raia waliotoweka ni walitoweka na kufa/kuuawa.
Haya yote yameleta chuki isiyokuwa ya kawaida dhidi ya serikali awamu ya 5. Imefanya kila inachofanya serikali kionekane kibaya. Wapinzani wanaonekana kama swala mbele ya Simba. Mpinzani hana thamani na uhai wake. ccm mpya kila kitu kinachofanywa na serikali kwa kodi za wananchi wote wanaweka chata ya maneno kuwa ni cha ccm kama vile ndege za ccm, SGR ya ccm n.k.
Sasa wewe umefurahia viongozi wangu kuumizwa au kuuawa na unajisifu kuwa ndege umenunua wewe, kwanini ndege inayokupa kiburi inapopata hitilafu au mgogoro Mimi nisishangilie?
Haya yote yamepandwa sio bure Tanzania haikuwa hivi. Siku hizi Kiongozi wa ccm akifa wapinzani (Chadema) wanasema afadhali wapungue, kiongozi wa Chadema akifa, ccm wanashangilia bora limekufa. Mpaka kuna wakati wanaandika kusingizia fulani (kiongozi mkubwa) amekufa. Sio hawana akili ila ni chuki imepandwa. Umoja na Mshikamano wetu vimevurugwa na awamu ya 5, viongozi wapo wala hawakemei ama kuchukua hatua za makusudi kurejesha hali ikae sasa. Wanachokisubiri kitakuja.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.